Mnaomshambulia Spika Ndugai someni katiba ya nchi

Mnaomshambulia Spika Ndugai someni katiba ya nchi

Umekosea mkuu. Chama kina mpata taarifa spika kisha naye anaijulisha NEC
Kumezuka wimbi la watu kukurupuka na kumshambulia Ndugai bila kwanza kujua katiba inasemaje, kwa kifupi Ndugai yuko sahihi na Chadema wako sahihi. Nianze na Chadema, Chadema haijamfukuza mtu yoyote ubunge kwani haina mamlaka hayo, ilichofanya ni kuwafukuza uanachama na jukumu lao litaishia hapo baada ya kuijulisha tume ya uchaguzi ambayo inataka kila mbunge awe mwanachama wa chama cha siasa.

Spika Ndugai hapokei maelekezo toka kwenye chama cha siasa, baada ya chama husika kuijulisha tume ya uchaguzi, tume hiyo itamjukisha Spika juu ya mbunge husika kukosa sifa ya kuwa mwanachama wa chama cha siasa, hapo ndipo Spika atatakiwa kutekeleza kulingana na matakwa ya katiba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na malizia kusema na nikiungana na watu wengi hapa, Kwa namna ya katiba ilivyo kama kweli Iko hivyo, basi Chama hiki kiliundwa kimaslahi zaidi na si vinginevyo,

Ni ishara ya kuwa upo mzizi uliojichimbia zaidi ukisaidiwa na katiba, na niseme pia, siku akiondoka huyo aliyejichimbia akisaidiwa na katiba ya Chama, Katiba hii iliyojaa mapungufu itafumuliwa na kuungwa mkono na wote wenye akiri timamu hapo chamani

Kwa SASA fanyeni mtakavyo Kwa vile na ninyi mpo ili mkono uende kinywani
CCM imejichimbia na kuing'ang'ania katiba iliyopo kwa maslahi ya chama na viongozi wake kwa kutumia dola, vyama vingine na wananchi hatuna usemi wowote, kura yangu siyo haki yangu.
 
CCM imejichimbia na kuing'ang'ania katiba iliyopo kwa maslahi ya chama na viongozi wake kwa kutumia dola, vyama vingine na wananchi hatuna usemi wowote, kura yangu siyo haki yangu.
Tunapoikataa CCM tuikatae na vitendo vyake huku tukionyesha mambo yetu Safi Kwa vitendo, sio kuikataa midomoni tu lakini vitendo vyake na Sisi tunafanya, na huo ndio upumbavu tunaoukemea kutoka kwenye Vyama mbadala
 
Back
Top Bottom