Mnamkumbuka Tola mchoyo?

Dah!!!Maisha yalikuwa tambarare sana sikutegemea kuja kukutana na haya ya ma~padlock.
 
Hadith za zamani zilitufundisha mengi ila siku izi baadhi ya wakina mama wanawafundisha watoto kusasambua na kucheza visingeli huku wakiwachukua kideo.

Sipati picha kizazi kijacho
Ohoooo!![emoji86] [emoji86] [emoji86] [emoji86]
 
Tola:njaa ipo muda mrefu
Watt:watu wanalala bila kula
Tola:mmmh mmmh.
Hahahahahaha uwiii jaman watt wa sasa hivi ni digital.zaman ilikuwa raha sana
 
Lakini hii stori ilitufunza mengi yaani tusiw wachoyo!!lakini nadhani ilikuwa na kauwongo ndani maana huwezi tafuna konokono alafu ummeze eti umtapike alafu atembee hapo hapo[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Zamani sana ingawa nilimaliza shule miaka ya 78 ila nilikuwa napenda kusoma vitabu vya watoto wakitoka shule
chitemo mimi masikini uvivu wangu nyumbani nikiwa huku njiani nakufa hapa kwanini Sadiki sasa ashiba chakula kingi kwa baba nirudi tena nyumbani chakula kingi kwa baba ila siku hizi watoto wa digital
 
Na tulivyokuwaga wajinga eti tulikua tunaamini kua hii kitu ilishatokea. mfano mua uliozamisha meli yaan unaanza kupiga picha halafu unaamini kuna siku kweli muwa ulizamisha meli
Elimu ya msingi kuna vitu vingi sana tulidanganywa
 
Watoto wageuka mawe.
sizitaki hizi mbichi.
Juma na uledi.
Siku ya gulio
Barua kutoka makole,
Utanikumbuka,
na vingine vingi ila safari ya maisha ni ndefu wish tungekuwa tunarudishwa tuanakumbuka tulikotoka.
 
Mr sikuelewi! Ilikuwa ni ya darasa la nne nafikiri..
 
[emoji3] [emoji3] kitambo sana izi hadithi
 
Umenikumbusha kale kawimbo

Tola: Njaa ipo muda mrefu.
Watoto: watu wanalala bila kula [emoji23][emoji23][emoji23] Darasa la pili hyo dah miaka hyo
Ahahahahaaaaa wakati anameza msosi tola alikuwa anaitikia "mh mh mh mh mmmmmmm" alikuwa mchoyo sana mpaka anawanyima watoto wake
 
Ktk vile vitabu kuna kijiji kiliitwa 'mtakuja'
 
Na ile ya chopeko na mnofu.
La sita pia kuna kile kina "sijielewi" yani "iji ng'ombe jose ni ja kweni"?
 
Jamani hii story ndio ilinifanya nisiwe mchoyo mpaka leo japo wife wangu ni mchoyo lakini nipo radhi nilale kavu kuliko mgeni yeyote aliekuja kwangu atoke kavu.
Pole mfundishe taratibu kuwa uchoyo sio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…