Mkuu CodeR GodivA inamaana unacheza na brands au unacheza na specs?
Tigo walitikisa sana kwa series yao ya ascend y200 (Tsh 165,000)mwaka juzi na y300 (Tsh 175,000 na 195,000)ndio ikawa hatari zaidi kuanzia mwaka jana. Hizi simu zote nimezijaribu, ziko poa sana tu kwa bei hizo.
Voda nae naona kaleta hii simu Vodacom Smart Mini V875 kwa Tsh 100,000 tu. Kwa wasioiona au kuikuta mahala mtandaoni, Sifa zake baadhi ni hizi:
- Kioo: LCD Capacitive Touch screen, 3.5" (According to GSM Arena wanasema kioo ni TFT sio LCD kama Vodacom wanavyosema)
- Processor: Media Tek MT6575 1Ghz
- RAM: 512MB
- Internal Memory 4GB
- Camera: 2MP
- OS: Android 4.1 (Jelly Bean)
Hizo ndio baadhi ya sifa zake wakuu. kama kuna mtu ameshaijaribu anasemaje? Maana naona bei yake ni nzuri tu na affordable.
View attachment 141932
Nime LIKE kaka. Naomba nifundishe jinsi ya kukuza picha...
For those whom they know how and in what kind SMART PHONE looks like, that is not the best choice but if your aim ni kufanana na those with smart phones just take it.
bei inaendana na specs, i even think its a bargain.
hivi kuna simu mpya ya android yenye bei ndogo zaidi ya hii!?
hapa hata ''watoto'' wa xi jinping wamepigwa bao.
Jamani wengine siye huwa si wajuzi wa haya mambo, hivi ninatakiwa kuangalia nini ili nijue hii smartphone inafaaa na sitajuta kuwa nimepoteza pesa, maana wengine "akina maimuna" huwa tunaangalia, je ina redio, kamera,blue tooth, memory kadi basi
bei inaendana na specs, i even think its a bargain.
hivi kuna simu mpya ya android yenye bei ndogo zaidi ya hii!?
hapa hata ''watoto'' wa xi jinping wamepigwa bao.
Hata hii naimani inatoka hukohuko, ukiifungua chini ya battery utapata majibu, kama siyo ZTE.....
Duh. Mkuu vipo vitu ni vingi so ngumu kugeneralize.
mhh,kazi kweli! haya ngoja ntakua nanunua kwa vigezo vyangu "radio,camera,bluetooth" ili maisha yaende
umesahau infared