Vodacom yazindua kupiga simu kwa bei nafuu, na ofa ya ujumbe mfupi/SMS na intaneti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vodacom yazindua kupiga simu kwa bei nafuu, na ofa ya ujumbe mfupi/SMS na intaneti

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by danione, May 7, 2012.

 1. danione

  danione Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  • ¼ shilingi kwa sekunde kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi kutoka Vodacom kwenda Vodacom
  • Punguzo la SMS la 45% hadi Tsh. 25 kwa SMS kwenda mtandao wowote Tanzania.
  • Kurambaza mitandao ya Facebook na Twitter bure
  • Simu za wateja wa Vodacom wa malipo ya kabla zitajisajili moja kwa moja kwenye ofa hii

  Dar es Salaam, Mei 7, 2012: Vodacom leo imezindua ofa mpya ya kusisimua iliyoandaliwa hususan kukidhi mahitaji ya mawasiliano ya umma wa soko la vijana ili kuendelea kukuza idadi yake ya wateja kwa kutoa huduma za mawasiliano ya simu yanaomudika kwa Watanzania wote.

  Katika kampeni mpya iitwayo Wajanja wateja wa Vodacom wa malipo ya kabla watatozwa kiwango cha chini kabisa cha robo shilingi kwa simu za Vodacom kwenda Vodacom kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi. Ofa hii mpya vile vile itawatoza bei ya chini kabisa ya ujumbe mfupi ya Tsh 25 kwenda mtandao wowote Tanzania, pamoja na kurambaza tovuti ya Facebook na Twitter bure.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza alisema ofa hii mpya imeandaliwa kukidhi mahitaji ya walio wengi katika soko la mawasiliano la simu za mkononi, hususan vijana- na itawawezesha kuwa na taarifa motomoto kila wakati na kuwawezesha kuwasiliana kwa simu za sauti, ujumbe mfupi na Intaneti kwa bei wanazozimudu. Hakika vijana si vijaba tu watakaofurahia ofa hii mpya bali wateja wote wa Vodacom wa huduma ya kulipia kabla watafaidika na huduma pamoja na viwango hivi vipya vya chini.

  “ Vodacom imenuia kutoa huduma kwa bei ambazo Watanzania wote wataweza kuzimudu. Kwa kuwawezesha Watanzania kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi na kutumia Intaneti kwa bei nafuu, tunaamini kwamba wateja wa simu za mikononi wa Tanzania sasa wataweza kuwa sehemu ya dunia ya kisasa kupitia simu zao za mkononi, “ alisema Meza.

  Ofa hii haihitaji wateja wa huduma za kulipia kabla kujisajili. “ Hakuna haja ya wateja kujisajili kwenye ofa hii. Watafaidika ili mradi wako hewani kwenye mtandao wa Vodacom”, Meza alisema.
   
 2. The Genius

  The Genius Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kuanzia sio mbaya sana. Ila wapunguze gharama za internet, maana matumizi ya internet sio FB na Twitter tu.
   
 3. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Ntafurahi na JF ikiwa bure; ingawa ni kama ndoto!
   
 4. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Ofa ya kupiga simu usiku ni danganya toto,
  kama wapo siriaz na hizo ofa waweke kuanzia mchana,
  otherwise hiyo offer ni mateso tu!
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Na unaweza mtu kujiachia usingizi wako ili upige halafu ukakutana na problems za networking
   
 6. ney kush

  ney kush JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 1,195
  Likes Received: 377
  Trophy Points: 180
  hamna kitu hapo... kwa leo na kesho after hapo sahauni
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ni wazo zuri sana, wangetamtabua tovuti za nyumbani kwanza kabla ya hizo za nje.

  Natumai Mwamvita ataliona hili.
   
 8. iron2012

  iron2012 JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 358
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  hawa vodacom wanadhani sisi tunafanya kazi za ulinzi usiku? kama wanawajali watanzania watoe ofa hizo wakati wote mchana na usiku
   
 9. The Genius

  The Genius Member

  #9
  May 7, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata hivyo hiyo offer ya kupiga ilikuwepo kama 2-3 months ago(kama sijakosea), mpaka inaisha hata sikumbuki kama niliitumia. Mimi naami hii offer inalenga kundi fulani la watu, sidhani kama mtu mzima na heshima yako utasubiri usiku ufike ndio upige simu. Mazumgumzo gani hayo ya kusubiri usiku tu? Wanataka kutuharibia watoto hawa.

  They cant be serious, huh!
   
 10. Parata

  Parata JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 3,119
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  na vijana wataharibikiwa kweli si mchezo hapo utaskia usiku kata basiiiii........ kata weweweeee.... vituko vitupu ila sie watu wazima aaagh muda huo ukipiga simu utakuwa una matatizo yaani mia tano ikutese ivoooo
   
 11. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,581
  Likes Received: 848
  Trophy Points: 280
  kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi, hizo ni :blah: :blah: tu!
   
 12. Parata

  Parata JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 3,119
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  tena ni pruuuuuuu
   
 13. Amina Thomas

  Amina Thomas JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 272
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  vodacom waboreshe kwanza huduma zao badala ya kutoa ofa. Mtandao una mikwaruzo na mikatako kiasi hamsikilizani. Ni bora nilipe pesa nyingi nipate huduma nzuri kuliko rahisi yenye adha. Hata south afrian news kupitia e. News walisema vodacom is in hot soup hasa drc, tanzania na kenya kwa ubovu sa mawasilianmo.
   
 14. deojames

  deojames JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 323
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Wangekuwa wamaana kama wangeshusha bei za vifurushi sio kutudanganya na hizo facebook na twitter halafu wanadai ndio wamepunguza gharama za net.
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  May 7, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kwa internet afadhali nijikalie ttcl broadband au 3g ya airtel. Inalipa na ni nzuri! Hawa wengine wezi kiaina tu! kifurushi cha 750mb wanauza 15,000 wakati wenzao airtel wanauza 1gb kwa pesa hiyo hiyo. Sidangayiki maana mie sio shabiki wa twitter na Fb tu. Afadhali kama wangesema na JF hapo ningefikiri upya uamuzi wangu!
   
 16. ARV

  ARV JF-Expert Member

  #16
  May 7, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 311
  Trophy Points: 180
  750MB wanauza 10,000/= inaitwa BOMBA 7.Unatumia hizo 750mb kwa spidi kali ajabu, zikiisha unaendelea kula net kawaida mpaka hizo siku saba ziishe.
  MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE......

   
 17. Arvin sloane

  Arvin sloane JF-Expert Member

  #17
  May 7, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 963
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  safi sana Vodacom na mitandao mingine iige mfano huo.
   
 18. Eddy M

  Eddy M Member

  #18
  May 7, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 60
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Hakuna lolote hapo, hofa usiku! Kwanza mlikuwa wapi muda wote hou? kama nyie wababe fanya mchana tuone.Kitu airtel bana unaongeo unamaliza lugha zote unazozijua kwa jero tu tena mchana Duh.Voda jipange upya
   
 19. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #19
  May 8, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,486
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Kwa soko la Tanzania kama unataka kusaidia jamii kiukweli ofa kama hiyo wangeitoa JF.
   
 20. Paje

  Paje JF-Expert Member

  #20
  May 9, 2012
  Joined: Apr 24, 2010
  Messages: 1,198
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  sssshhhhhhhhhhh!!!!! silence!!!!!
   
Loading...