Huawei waungana na vodacom kuhakikisha kila mtanzania ana simu ya kisasa

lyzbeth

Member
Mar 6, 2014
40
8
Katika mwendelezo wa kuhakikisha kuwa watanzania wanapata haki yao ya mawasiliano na kumiliki sio simu tu bali simu ya kisasa, Huawei imeendelea kuchanja mbuga katika kujiongezea soko la simu zake nchini na kuongeza bidii kuingiza simu bora za kisasa zenye gharama nafuu. Katika moja ya mpango wao wa kibunifu katika kuleta chaguo bora kwa wanunuzi wa simu wanaohitaji kupata simu bora na kwa gharama nafuu, Huawei imeshirikiana na Vodacom Tanzania kuleta simu ya Huawei Kishkwambi iliyounganishwa na kifurushi cha Vodacom cha muda wa maongezi na internet.

Promosheni ya Huawei Kishkwambi inaenda sambamba na uzinduzi wa maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Saba Saba. Simu hii inanunuliwa kwa sh. 100,000 tu, ikiwa na kifurusha cha bure cha internet cha GB6 na dakika 100 za bure za maongezi katika mtandao wa 3G wa Vodacom kwa mwaka mmoja. Simu hii pia huja na waranti ya miezi 12 kutoka Huawei.

Katika juhudi zake za kuongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa nchini Tanzania, Huawei imeona haja ya kuwawezesha watumiaji wa simu kuwa na chaguo bora la kununua simu halisi. Mara baada ya kuanza kwa utaratibu wa kuzima simu feki, simu nyingi sana zimezimwa na wengi wa watumiaji ambao walijibana ili kumudu kununua simu za gharama nafuu sasa hawana tena simu. Promosheni hii ni fursa adhimu kwa watumiaji ili kununua si tu simu mpya bali pia simu ambayo inaweza kuwa na data za internet, simu orijino, yenye waranti ya miezi 12 lakini pia ya gharama nafuu sana.

Mkurugenzi Mkazi wa Huawei Bw. Huxiangyang Jacko anasema, “Huawei imedhamiria kufikia maeneo yote ya soko la Tanzania kupitia bidhaa zao nyingi ambazo pia zimethibitika kufanya vema katika masoko mengine ulimwenguni. Lakini kwa Tanzania, tunataka kuweka mkazo kwa watu wa kipato cha kati na cha chini, wanafunzi na wafanyakazi vijana ambao wanathamini ubora na pia wanajali bei. Kwa sababu hiyo, Huawei Kishkwambi inaonesha kuwa ndio simu bora tunayoweza kuwapatia wateja wetu ambayo yaweza kuwa ndio simu ya kwanza au pia kwa wale wanaotaka kuongeza simu ya pili”.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Bw. George Rwehumbiza alisema ushirikiano wao na Huawei unaendana na nia ya Vodacom Tanzania ya kuwapatia wateja wao fursa ya kununua simu bora na za bei nafuu hususani baada ya zoezi la hivi karibuni la uzimaji simu feki lililotekelezwa na TCRA.

“Vodacom Tanzania imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wateja wake wanaendelea kuunganishwa hata baada ya uzimaji mkubwa wa simu uliofanywa na TCRA, hivyo basi ushirikiano wetu na Huawei unaongeza msukumo wetu kuhakikisha kuwa wateja wetu wanabakia wakiwa wameunganishwa na katika hilo pia tunawapatia motisha ya vifurushi vya internet na muda wa maongezi lukuki” alisema afisa huyo wa Vodacom Tanzania.

Huawei Kishkwambi ni simu iliyowezeshwa kwa 3G na inazo sifa zote za simu za kisasa, na kwa vifurushi vya gharama nafuu vya muda wa maongezi na internet wateja wanaweza kuperuzi mtandaoni, Facebook na hata Instagram. Simu hii ina kioo cha LCD cha inchi 4. Ili kuleta mvuto wa kipekee, Huawei Kishkwambi ina mgongo wenye mkunjo kwa mbali na kona zake nne zilizopinda bila ncha kali. Muundo wake huu wa kipekee unawapa watumiaji wake hisia nzuri wanapoishika na ni rahisi kuitumia hata kwa mkono mmoja. Ina megapikseli 0.3 katika kamera yake ya mbele na megapikseli 2 katika kamera ya nyuma. Huawei Kishkwambi ina prosesa 2 ambazo huipa uwezo wa kufanya kazi haraka sana katika kucheza michezo ya kwenye simu (game). Kadi yake ina ukubwa wa MB512 na ROM ya GB4 ambayo inaweza kuongezwa kwa kadi ya nje. Simu hii ina spidi ya hali ya juu na uwezo mkubwa wa kutunza chaji.

Ushirikiano huu wa kipekee wa miamba miwili ya kimataifa nchini Tanzania ni hatua ya kimkakati ya Huawei na Vodacom ya pamoja katika kuleta suluhisho kwa watumiaji wa simu. Kila simu ya kisasa inahitaji kuunganishwa na mtandao bora ili kuleta ubora halisi kwa mtumiaji wa simu. Hapa ndipo utendaji wa simu ya Huawei Kishkwambi unapoendana na mtandao wenye kasi wa Vodacom 3G kuleta nguvu Zaidi kwa watumiaji.

Katika kufanikisha wazo la serikali kuwa haki ya kuwasiliana inapaswa kumfikia kila mtanzania, Vodacom imekuwa ikifanya jitihada pasipo kuchoka katika kuwaunganisha watanzania na kuongeza uwekezaji katika sekta ya mawasiliano ya simu. Ushirikiano na Huawei katika promosheni ya Huawei Kishkwambi ni moja ya namna nyingi ya ofa zinazotolewa kwa wateja. Promosheni hii maalum ya Huawei Kishkwambi inatolewa katika maduka yote ya Huawei na Vodacom nchini kote. Huawei na Vodacom kwa pamoja zinawahimiza watanzania kuitumia vilivyo fursa ya promosheni hii na kufurahia kuendelea kuunganishwa kimawasiliano.
DSC_0006.jpg
DSC_0006.jpg
DSC_0019.JPG
DSC_0126 (2).jpg
DSC_0130.JPG
DSC_0130.JPG
DSC_0136.jpg
DSC_0139 (2).JPG
DSC_0152.JPG
DSC_0154 (2).jpg
 
....Huawei siwaamini kabisa,toka ninunue simu yao guarantee ilipoisha baada ya mwaka mmoja na simu ikafa!, sina hamu nao.
 
Back
Top Bottom