Mnadhani wananchi wa Iran na Venezuela wanajali Marekani kuchukua mafuta ? wananchi ni maskini, wanauawa, wamekimbia nchi, watakataaje msaada ?

Mnadhani wananchi wa Iran na Venezuela wanajali Marekani kuchukua mafuta ? wananchi ni maskini, wanauawa, wamekimbia nchi, watakataaje msaada ?

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
1,910
Reaction score
5,451
Hakuna free lunch hapa duniani.

Lakini afadhali kusaidiwa na mtu wa mbali unajua kabisa atachukua sehemu flani ya rasilimali kisha awaache muendelee na maisha mengine kwa uhuru kuliko kuongozwa na ndugu yako mlafi, kakuacha katika umasikini, Mbaya zaidi ukimhoji, mnapigwa risasi au kufungwa jela.

mnadhani wananchi wa Iran wanawaza tu kwamba Donald Trump atawaibia sehemu ya mafuta yao ? Wananchi wanauliza swali lingine kabisa: hayo mafuta yamewasaidia nini hadi leo ? Nchi ina mafuta mengi lakini bado watu wanakosa umeme, maji na maisha yanazidi kuwa magumu, hakuna uhuru wa kujielezam watu zaidi ya elfu 40 wameuawa.

Kumekuwa na maandamano mara kwa mara kwa sababu ya umaskini, mfumuko wa bei na ukandamizaji wa kisiasa.

Kwa hiyo kwa baadhi ya wananchi, wanaona hoja si nani atachukua mafuta. Hoja ni kama kuna njia yoyote ya kupata uhuru na maisha bora kuliko wanayopitia sasa.

Ni sawa pia na Venezuela. Unafikiri wananchi wanaoteseka na umaskini mkubwa na waliolazimika kukimbia nchi yao wataweka mbele suala la nani anachukua mafuta, au wataweka mbele tumaini la mabadiliko?

Kwa watu wanaoishi kwenye mfumo ulioshindwa, wakati mwingine swali linakuwa rahisi sana:
ni nani anaweza kubadilisha hali yao ya maisha.
 
Dah kweli man ndio maana kila mwanamke mzuri mcheza video za ngono anatoka venezuela...
Adult model wote wanapiga naked photo wanatoka venezuela...maisha magumu mno venezuela
 
Ndio unaona bora shetani anayekusaidia kuliko malaika anayekukaushia.
 
Ndio unaona bora shetani anayekusaidia kuliko malaika anayekukaushia.
mgeni anakuwa na afadhali mara 100 kuzidi

ndugu yako mlafi anaekuacha kwenye umasikini na kukupiga risasi ukimhoji, huyo ni shetani kabisa
 
Back
Top Bottom