Mnada wa korosho wasitishwa baada ya kukosekana mnunuzi

Kila mtu aliona wizi tena wa kishamba kabisa wa kura ulivyofanyika, swala la mahakamani labda uchaguzi ungefanyika leo lakini kwa wakati ule mahakama ilikuwa imeminywa na haikuwa huru kabisa.
Baasi punguza kulialia tutamchapa aliyekukanyaga ati! Basiiii nyamaza mtoto waache wakulima wajadiri mambo ya korosho.
 
Dah, yaani jamaa anabwabwaja sjui hata mti wa korosho kama anaujua, shortly aliyeharibu zao biashara ya korosho ni JPM a.k.a JIWe
Kwa taarifa yako Jiwe ndio ameipa korosho thamani. Labda ukisema kuharibu korosho ni jiwe naweza kukubaliana na wewe sababu wakati Jiwe anaingia common price ya korosho ilikuwa 1700 tu bei ya juu..alipoingia ikaenda 4200. Kuanzia hapo wakulima wakashtuka kuwa kumbe inawezekana. Kama uliisikia wakulima wa korosho walikuwa wananywesha soda mbuzi kwa kushangilia bei.

Enzi hizo si shinyanga wala kigoma wanaijua korosho. Leo nenda shinyanga utakuta wanalima korosho. Huko kusini watu wanamiminika kulima korosho.
 
Jaribu kuwa na kumbukumbu kidogo, tozo zimeongezwa, sasahivi imeongezeka sh 40 kwa kila kilo, enzi za JPM utaratibu wa ununuzi haukuwa mzuri, mpaka uonyeshe shamba la korosho, likaguliwe ndo utauza, haikukaa vema sana
Sio kweli. Ishu ya shamba ilijitokeza mara moja tu wakati wa kampeni ya kuzuia kangomba. Hata hivyo badae iliendelea. Mimi ni mnufaika mmojwapo wa kangomba kwa mwaka jana.
 
Kwa taarifa yako Jiwe ndio ameipa korosho thamani. Labda ukisema kuharibu korosho ni jiwe naweza kukubaliana na wewe sababu wakati Jiwe anaingia common price ya korosho ilikuwa 1700 tu bei ya juu..alipoingia ikaenda 4200. Kuanzia hapo wakulima wakashtuka kuwa kumbe inawezekana. Kama uliisikia wakulima wa korosho walikuwa wananywesha soda mbuzi kwa kushangilia bei.

Enzi hizo si shinyanga wala kigoma wanaijua korosho. Leo nenda shinyanga utakuta wanalima korosho. Huko kusini watu wanamiminika kulima korosho.
Baada ya bei kupanda akaona donge akaharibu biashara yenyewe yote alianza kwa kuwadhulumu korosho zao na baadae bei ikashuka kuliko aliyoikuta,usimtetea muharibifu na dhulumati.
 
Siasa imehusika vipi na kukosekana wanunuzi kwenye mnada??
Soko huwa linatafutwa na linalindwa. Ukilivuruga, huwezi kuamka na kulipata tena maana siku zote wapo wanaotafuta masoko. Na hicho ndicho viongozi wengi wa serikali hawajui. Unakuta mara waziri mkuu anainuka na kusema, kuanzia leo marufuku kupeleka mahindi nje ya nchi, halafu baada ya muda utasikia, tumeruhusu mahindi kuuza nje! Hopeless kabisa. Watu wanahangaika kutafuta soko, unavuruga, halafu baadaye unasema eti wauze nje. Huko nje walikuwa wamekaa wanakusubiria wewe? Ukisikia hivyo, unakuwa huna shaka kuwa wajinga wamejikusanya, wapo huko serikalini kwaajili ya kuwaharibia wenye uelewa.

Soko la korosho alilivuruga marehemu, itachukua muda mpaka kuwa na soko la uhakika tena maana wanununuzi wakubwa waliokuwa wanapokea korosho toka TZ walikwishapata suppliers wengine.

Kwenye katiba mpya, iwekwe kabisa sheria kuwa kiongozi akitoa amri inayoathiri uchumi wa wananchi au nchi, ashtakiwe kwa kosa la uhujumu uchumi.
 
Baada ya bei kupanda akaona donge akaharibu biashara yenyewe yote alianza kwa kuwadhulumu korosho zao na baadae bei ikashuka kuliko aliyoikuta,usimtetea muharibifu na dhulumati.
Sasa ye ndio aliyeipandisha kwa kuondoa mtu kati kwa nini aone donge. Labda wewe usiojua kuwa hata kukodi shamba la korosho ilikuwa 100000 tu na watu hawakodi, wakati sasa hivi hata mill 2 mkulima hakupi shamba.
 
Gazeti la Nipashe la leo limeripoti kwa masikitiko makubwa kuwa mnada wa korosho umesitishwa baada ya kampuni za wanunuzi kukosekana! .

Hii inatokea huku Nape Nnauye na Zito Kabwe waliojipambanua kama watetezi wa wakulima wa korosho na wakapiga kelele sana miaka yote mitano ya Serikali ya awamu ya tano wakiwa kimya kabisa kana kwamba hawajui kinachowatokea wakulima wa korosho mwaka huu.

Je, wakulima wa korosho watetewe na nani?

Nguvu ya Nape, Zitto, Membe kulisemea zao la korosho imeenda wapi?

View attachment 1994504
Hili ni gazeti la lini?
Na huo mnada umefanyika wapi na ni lini? Kwa sababu leo ni Jumatatu na minada huwa inafanyika Ijumaa ya kila Wiki.

Mnada wa mwisho ulifanyika tarehe 29/10/2021 ambapo; Bei ya juu ilikuwa 2,170 na bei ya chini ni 2100/=
 
Asante
 
Maamuzi ya Magufuli yamechangia zaidi ya 80% kuharibu biashara ya Korosho hapa nchini.

Tangu afanye yale maamuzi ya ki-Jiwe bei ya Korosho imekuwa ikiporomoka siku hadi siku. Nakumbuka mwaka uliofuata baada ya Serikali kudhulumu wakulima, korosho bei ya Juu ilikuwa 2600 na sasa hivi bei ya imefika 2400.

Baada ya Magufuli kusema atanunua korosho kwa 3500 na badala yake akaanza kudhulumu kwa kuchukua korosho za watu ambapo alikuja kuwalipa Tzs 2640 na wengine kutokulipwa kabisa ndipo mambo yalipoanza kuharibika. Leo hii hakuna mkulima atakayekubali kuuza korosho zake kwa Serikali. Never.

Magufuli alipayuka majukwaani na kusema atafufua viwanda, ila hakuna kiwanda cha Korosho kimefulfuliwa chini ya Utawala wake na hakuna korosho ilibanguliwa.

Ila wakulima wa Korosho walishamlilia MUNGU wao na kumuachia yeye kwani yeye ni Alfa na Omega.
 
Mbwembwe zote pamoja na kuondoa vikwazo na tozo kadhaa lakini wapi; mlimshambulia sana JPM alipoamua kununua ili wananchi wapate chochote, sasa hawa watawala wana la kusema kutokana na aibu hii?

Wanasiasa wabaya sana kuhusika kwenye ustawi wa biashara
Hakuna Mwananchi alikuja kufurahia utekelezaji wa kauli za huyo JPM. Watu wamedhulumiwa korosho zao na waliolipwa wamelipwa kwa bei ya 2640 wakati yeye majukwaa i anatangaza 3500.

We ulikuwa hushangai kila siku alikuwa anatoa maagizo kwa BOT zitoke hela na bado wakulima walikuwa hawapati fedha zao? Jiwe na watu ndio wanajua yale mabilioni wameyapeleka wapi
 
Mtoa maada kinukuu chanzo chako vizuri ili ueleze ni wapi hasa wanunuzi wamekosekana
 
Hakuna Mwananchi alikuja kufurahia utekelezaji wa kauli za huyo JPM. Watu wamedhulumiwa korosho zao na waliolipwa wamelipwa kwa bei ya 2640 wakati yeye majukwaa i anatangaza 3500.

We ulikuwa hushangai kila siku alikuwa anatoa maagizo kwa BOT zitoke hela na bado wakulima walikuwa hawapati fedha zao? Jiwe na watu ndio wanajua yale mabilioni wameyapeleka wapi
Mnada wa juzi hayati JPM amezuiaje wanunuzi kuja?
 
Maamuzi ya Magufuli yamechangia zaidi ya 80% kuharibu biashara ya Korosho hapa nchini.

Tangu afanye yale maamuzi ya ki-Jiwe bei ya Korosho imekuwa ikiporomoka siku hadi siku. Nakumbuka mwaka uliofuata baada ya Serikali kudhulumu wakulima, korosho bei ya Juu ilikuwa 2600 na sasa hivi bei ya imefika 2400.

Baada ya Magufuli kusema atanunua korosho kwa 3500 na badala yake akaanza kudhulumu kwa kuchukua korosho za watu ambapo alikuja kuwalipa Tzs 2640 na wengine kutokulipwa kabisa ndipo mambo yalipoanza kuharibika. Leo hii hakuna mkulima atakayekubali kuuza korosho zake kwa Serikali. Never.

Magufuli alipayuka majukwaani na kusema atafufua viwanda, ila hakuna kiwanda cha Korosho kimefulfuliwa chini ya Utawala wake na hakuna korosho ilibanguliwa.

Ila wakulima wa Korosho walishamlilia MUNGU wao na kumuachia yeye kwani yeye ni Alfa na Omega.
Kumbe marehemu anaweza kuporomosha bei ya korosho?

Basi huyu marehemu atakuwa na akili kuliko wewe kilaza unayetembea
 
Gazeti hili limeandika kikanjanja na limeongopa hawajajiridhisha sababu za kusitishwa kwa minada ya korosho.

Kimsingi wakulima waligomea bei kuwa ndogo ambapo wafanyabiashara walilalamika kuwa walilazimika kununua kwa bei hizo kutokana na gharama za kusubiri mzigo hadi kuusafirisha kuwalalia

Kuna hoja zinashughulikiwa na serikali kuhusu kutumia bandari ya mtwara au dsm ambayo ilikuwa inalalamikiwa na wafanyabiashara na serikali imeshawaruhusu wanunuzi wa korosho kutumia bandari ya dsm kutokana na bandari ya mtwara kutokuwa na makontena ya kutosha hali iliyokuwa inapelekea mzigo kukaa mda mrefu na kuongeza gharama ya kuhifadhi kabla ya kusafirishwa (storage charge) jambo ambalo tayari limetatuliwa

Tutarajie hivi karibuni minada kuendelea na bei kuwa nzuri zaidi kwa wakulima. Wanunuzi wa korosho wako wengi na mahitaji ni makubwa ila wakulima walikuwa hawajaridhika na bei kutokana na changamoto zilizopo.

Kongole kwa serikali kwa kushughulikia changamoto hii
 
Back
Top Bottom