Mna-save vipi pesa?

Gawa mshahara wako kwa kanuni ya asilimia​

Wengi wanatumia kanuni ya 50-30-20 kama msingi mzuri
  1. 50% = 325,000 kwa mahitaji ya lazima
    (Chakula, kodi, nauli, vocha, maji, umeme)
  2. 30% = 195,000 kwa anasa na starehe / matumizi binafsi
    (Mavazi, outing, vinywaji, movie, n.k.)
  3. 20% = 130,000 kwa kujiendeleza na akiba
    (Kuweka akiba, biashara ndogo, au kujifunza kitu kipya)
  4. Kama huwezi kujiamini, fungua akaunti tofauti au tumia mobile banking lock savings (kama NMB Mshiko, CRDB Wakala wa Akiba, M-Pawa Lock Savings n.k).
    Weka lazima angalau 100,000 kila mwezi mara tu mshahara ukiingia.
    Usiweke pesa iliyobaki β€” weka kwanza kabla hujatumia.
 

Hongera sana mkuu.

Vipi kuhusu breakfast, matunda, mbogamboga, maji, juice?
 
Huwa unakuwa wapi kila weekend? Hili litakupa jibu namna gani fedha zako zinaisha. Maana ndio siku za kuspend na totoz, pombe na starehe.

Unatumia usafiri gani kila siku? Hii ni muhimu sana as kwenda na kurudi kazini kunaweza kumaliza pesa zako hasa kama unatumia usafiri binafsi au ku-request.

Unakulaje, wapi na vyakula gani? Kama ni sehemu za gharama, hupiki lazima pesa iishe.

Unavaaje, bajeti yako ya kununua nguo ikoje. Kuna watu kila mwezi lazima nguo mpya, tena maduka yale sijui ni huko sinza nk.

Unatoaje kwa wengine, kuna pipo akiambiwa naomba 100k anatoa u, yeye anatoa tu.

Utazeeka huna hata mia bank, huna hata kiwanja, huna hata kauwekezaji kokote
 
Hongera sana mkuu.

Vipi kuhusu breakfast, matunda, mbogamboga, maji, juice?
Breakfast Mimi nina routine ya mazoezi so una weza shangaa nakunywa ginger tea iliyo mixiwa na kitunguu maji, swaumu na tangawizi yenyewe tu.

Maji nabeba ya home, aidha nachemsha au kuweka kwenye fridge ili yapate ubaridi.

Kuhusu matunda nilipo ni bei ndogo sana imagine kwa buku 1 napata kimoja wapo hapa tikiti, ndizi 15, maparachichi 5.

so jibu la juice liko hapo, kuhusu mboga ndio kabisa nina vi bustani uchwara na sokoni pia viko available kwa afforded price.
 
Wewe haupendi hela Ndio maana unashindwa kuziweka
Zipende hela ziongezeke
La sivyo utazidi kuzichezea na kuzimaliza mpaka mwisho wa maisha
 
Hii nimeielewa mkuu
Hakuna kitu hapo, anasema mchele kilo 25, unga kilo 25 je huo mchele unaiweka mafuta tu unakula? Au huo unga unakorogea uji tu? Hakuna bajeti ya mboga hapo,matunda hakuna, mimi nanunua vyote hivyo ulivyovitaja na ambavyo hajavitaja, kama tambi,sausages,maharage nk, na bado nalazimika kuacha si chini ya 5000 daily, kiufupi hesabu yake haijakamilika
 
Sasa nipande daladala 500, nispend 4hrs wakati bolt buku 2 dakika chache nimekamilisha safari.

Katika kitu mi sipendi na siwezi ni kuspend masaa barabarani kisa jero hapana
 
Kwa kuanzia, fungua account au tumia account ambayo hauna access nayo kwa haraka, kajaze ile huduma ya kukatwa salary huko huko inaingia kwenye hiyo account.....mengine angalia kwenye hiki kitabu
 

Attachments

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…