Mna maoni gani kuhusu hili suala la uvamizi wa Al-Shababu hapa Palma?

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Habari wadau!

Kutokana na vyanzo mbalimbali vya vyombo vya habari inasemekana kikundi cha watu wajulikanao kama Al-shababu wamevamia mji wa Palma.

Lakini kuna nadharia mbalimbali zimeenea mitaani kwamba watu hao waliovamia Msumbiji au jamhuri ya watu wa Mozambique sio Al-shabab bali ni siasa za mabeberu na uvamizi wa mabeberu baada ya ugunduzi wa gesi eneo la kaskazini mwa mji wa Maputo zenye reserve estimate ya 425Billion Cubic meter na hule ugunduzi wa gesi 40km kutoka pwani ya mji wa Calbo Delgado

Wataaramu wa mambo mnasemaje kuhusu hili? Je ni ishu ya Al-shababu au Al-shababu ndio mabeberu?

IMG_20210314_155044.jpg
 
Viongozi wa Africa wanatamaa,wabinafsi,wakiwa madarakani hujifanya kama ni wamiliki wa nchi kifupi ni hopeless tu wachache hunufaika na rasilimali za nchi huku wakiwataka wengine waendelee kuwa wazalendo kitu ambacho hakipo....kisha wakishaharibu husingizia mabeberu wanawatumia raia.

Sisi watu weusi hatujielewi kabisa mimi hushangaa ninapoambiwa Nigeria ni nchi tajiri Africa,halafu nikizoom maisha yao na maisha ya nchi kama Morocco,Tunisia,Algeria, Misri etc.

Hata hiyo South ukiwatoa wale kaburu wale raia wao hakuna kitu mule. Mtu mweusi ni mtu mweusi tu,kila mtu anajikomboa na familia,ukoo na jamaa zake kwenye kula keki ya taifa the rest endeleeni kuwa wazalendo.
 
Mkuu labda mie sielewi kwamba mabeberu wanapigana na mabeberu wenzao ama waafrika? Sababu nachojua huko tyr kuna kampuni za magharibi zinachimba rasilimali sasa kwanini tena watumie waasi wkt wameshamilikishwa madini?

Unajua hata DRC wanasemaga mabeberu yanaleta vita ili wapore madini lakini cha kushangaza hata maeneo walipoondoa waasi mfano then- Katanga province walipoondoa waasi bado wenye mkataba wa kuchimba walikuwa Total!! Same to Cabinda walitimua waasi ila bado wanaochimba off shore mafuta ni mabeberu!!

So mnaposema mabeberu wanaleta vita ili wachimbe almasi naomba mtusaidie je kukiwa na amani kma Tanzania ni nani anayechimba madini tena kwa mikataba ya kiwizi kabisa? Ama kukiwa na vita inawaongezea nni ambacho wanakikosa kukiwa na amani?

Cc Gerald .M Magembe
 
Mkuu labda mie sielewi kwamba mabeberu wanapigana na mabeberu wenzao ama waafrika? Sababu nachojua huko tyr kuna kampuni za magharibi zinachimba rasilimali sasa kwanini tena watumie waasi wkt wameshamilikishwa madini?...
Kuwa tyr kuna kampuni za kizungu(mabeberu) zinachimba ndio sababu ya kutokuoa na conflict of interest?

Unajifanya hujui nini kilifanya vita isiishe upesi Cabinda? Hujui kuwa ni baada ya vita baridi ndio Savimbi mabeberu walimtosa? Acha porojo zako.
 
Kuwa tyr kuna kampuni za kizungu(mabeberu zinachimba ndio sababu ya kutokuoa na conflict of interest?

Unajifanya hujui nini kilifanya vita isiishe upesi Cabinda? Hujui kuwa ni baada ya vita baridi ndio Savimbi mabeberu walimtosa? Acha porojo zako.
Vita ya savimbi ilikua ideological zaidi kuliko maslahi.... Ilikua kipindi cha Cold War kwahyo Sauzi, US na Russia walikua ma strategic goals pale otherwise vita iwepo isiwepo hizo almasi wanachimba mabeberu miaka yote tena kwa mikataba mibovu kabisa.

Kwani Tanzania hapa wanaochimba dhahabu ni watu weusi? Kuna vita? Tunaambulia 30% ya Corporate Tax ila 70% inaenda kwa mabeberu ila je wamehitaji kikundi cha waasi ili wanufaike na madini? Hivi kule DRC unahitaji waasi ndio uchimbe madini ilihali mabeberu wanachimba kwa mikataba ya kinyonyaji miaka yote?

Hoja iwe waasi wanatumika na mabeberu ili kudhoofisha mababeru wenzao waliopewa mikataba halali ya kuchimba ila kusema beberu ategemee waasi ili avune rasilimali ni kupotosha ukweli.

Pengine histoeia hufahamu ila Kabila pamoja na kudai mabeberu ni wezi wa madini lakini ndio aliwatumia kuchimba almasi na dhahabu na yye aliambulia 20% pekee huku 40% ikienda kwa kina Munangagwa na Angola na 40% kwa Wafaransa!! Ssa hapo Beberu na waasi kuna correlation gani?
 
Lakini kuna nadharia mbalimbali zimeenea mitaani kwamba watu hao waliovamia Msumbiji au jamhuri ya watu wa Mozambique sio Al-shabab bali ni siasa za mabeberu na uvamizi wa mabeberu baada ya ugunduzi wa gesi eneo la kaskazini mwa mji wa Maputo zenye reserve estimate ya 425Billion Cubic meter na hule ugunduzi wa gesi 40km kutoka pwani ya mji wa Calbo Delgado .
Ukweli upo hapa. Hakuna watu wajinga duniani ukiwaondoa Wanafalsafa, Wanasayansi na Atheist kuliko hawa waitwao Mabeberu. Wanakuwa sababu ya kumwagika kwa damu za watu, huku wenyewe watakufa na kinachofata ni huzuni na majonzi milele.
 
Viongozi wa Africa wanatamaa,wabinafsi,wakiwa madarakani hujifanya kama ni wamiliki wa nchi kifupi ni hopeless tu wachache hunufaika na rasilimali za nchi huku wakiwataka wengine waendelee kuwa wazalendo kitu ambacho hakipo....kisha wakishaharibu husingizia mabeberu wanawatumia raia.

Sisi watu weusi hatujielewi kabisa mimi hushangaa ninapoambiwa Nigeria ni nchi tajiri Africa,halafu nikizoom maisha yao na maisha ya nchi kama Morocco,Tunisia,Algeria, Misri etc.
Hata hiyo South ukiwatoa wale kaburu wale raia wao hakuna kitu mule.
Mtu mweusi ni mtu mweusi tu,kila mtu anajikomboa na familia,ukoo na jamaa zake kwenye kula keki ya taifa the rest endeleeni kuwa wazalendo.
Weusi ni LAANA!
 
Vita ya savimbi ilikua ideological zaidi kuliko maslahi.... Ilikua kipindi cha Cold War kwahyo Sauzi, US na Russia walikua ma strategic goals pale otherwise vita iwepo isiwepo hizo almasi wanachimba mabeberu miaka yote tena kwa mikataba mibovu kabisa.

Kwani Tanzania hapa wanaochimba dhahabu ni watu weusi? Kuna vita? Tunaambulia 30% ya Corporate Tax ila 70% inaenda kwa mabeberu ila je wamehitaji kikundi cha waasi ili wanufaike na madini? Hivi kule DRC unahitaji waasi ndio uchimbe madini ilihali mabeberu wanachimba kwa mikataba ya kinyonyaji miaka yote?

Hoja iwe waasi wanatumika na mabeberu ili kudhoofisha mababeru wenzao waliopewa mikataba halali ya kuchimba ila kusema beberu ategemee waasi ili avune rasilimali ni kupotosha ukweli.

Pengine histoeia hufahamu ila Kabila pamoja na kudai mabeberu ni wezi wa madini lakini ndio aliwatumia kuchimba almasi na dhahabu na yye aliambulia 20% pekee huku 40% ikienda kwa kina Munangagwa na Angola na 40% kwa Wafaransa!! Ssa hapo Beberu na waasi kuna correlation gani?
Vita ya Savimbi ilikuwa ideological kuliko maslahi? Kwamba hakuna aliyetaka kunufaika na almasi ya Angola?

Hapa Tanzania kulaumu kuwa tunapata 30% corporate tax ni kutaka kuleta lawama zisizofaa. Tufanye nini wakati hatuna mtaji? Unadhani kuikamata dhahabu ya Bulyanhulu bila mtaji ni rahisi. Lakini muwekezaji anakuja kuchimba kwa kupata vibari na taifa linanufaika. Tofauti na kufanyiwa ubabe wa kibeberu.

Drc waaasi wanateka maeneo na kuchimba madini kwa manufaa yao huku wakisaidiwa na mabeberu. Ndio maana ili Kabila apate hata kiduchu aliamua apate backup ya Zim na Angola.
 
Ninakubali 100% vita ya Angola ni ideological kama ilivyokuwa kwa Korea na Vietnam.
 
Somalia kuna rasilimali? kaskazini mwa kenya kwenye lile jangwa kuanzia Mandera hadi Wajir kuna rasilimali?

Waafrika tuache kuwatupia lawama wazungu kwa internal failures zetu.
Mabeberu hupenda kuweka vita maeneo yenye kitu kinachoingiza pesa nyingi Maeneo hayo ni yale yenye madini,au mafuta na gesi au madawa ya kulevya

Somalia wanalima sana mirungi na kuuza ulaya osama kule kwake Afghanistan ndio kunaongoza duniani kwenye kilimo cha cocaine !!!

Rwanda na Burundi hawana vyote hivyo ndio maana walipoanza kuuana mauaji ya kimbari hakuna mzungu alijali waliacha wauane watakavyo

Kenya tu hapo zilitokea vurugu wakauana mzungu hakujali sababu hivyo vitu hawana!! lakini cheki somalia na congo mzungu anajali na vikosi vya umoja wa mataifa viko kule!!!! jiulize kwa nini hawakupeleka vikosi kuzuia mauaji ya kimbari Burundi na Rwanda!!!! Jibu waliona hawana kitu cha faida kwao kati ya hivyo vitatu
 
Back
Top Bottom