magode
JF-Expert Member
- Oct 2, 2014
- 2,204
- 3,337
Wana MMU Salaam,
Hapa jukwaani kwa siku za karibuni na tunakoelekea, jukwaa linakosa/litakosa ule msingi hasa wa uwepo wake.
Ni ukweli usiopingika kuwa,hili ni jukwaa huru kwa maana ya kuelimishana kuhusu, maisha, mapenzi, ndoa na urafiki. Mbali na kuelimishana jukwaa hili huleta pia burudani hasa kwa mada zenye msisimko.
Hapa nataka kuzungumzia zile thread zinazodhalilisha wengine. Kwa mfano mtu anapoleta mada ya makundi ya MAKAHABA anataja sifa zote mbaya zinazowahusu akina mama, unasoma mpaka mwisho huoni mahali kam ameongelea wanawake walio na tabia njema.
Unajiuliza huyu aliyeandika hana wazazi? Au hata wazazi wake ni wahanga wa hizo tabia!? Hapa duniani kila kitu hakipo kama unavyokitizama na kila kitu kina pande mbili. Haiwezekani wanawake wote wakawa kama unavyofikiri.
Hata kwa upande wa jinsi ya KE unakuta mdada amekutana wanaume wawili wenye boxer chafu, anakuja hapa kuzungumzia wanaume wote kuwa hawafui boxer! Unajiuliza ina maana huyu amechunguza mpaka boxer za wote ?
Binafsi nimefikiria kuwepo na siku maalumu ya kuelimisha baadhi ya watu namna ya kuwasilisha hoja. Mtu unaweza kuwa na hoja nzuri sana, lakini tatizo lipo katika uwasilishaji badala ya kupata suluhisho, unajikuta unaenea matusi mwili mzima!
Tuchague uongozi hapa hapa jamvini na kila ijumaa saa 4 usiku muda huo uwe wa mafunzo. Ni maoni yangu binafsi haya kama yatafaa yaungwe mkono.