Mmoja wa Mawakili wa Erick Kabendera aeleza kinachoendelea

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,562
10,883
TAARIFA KUHUSU KUKAMATWA, KUWEKWA MAHABUSU NA KUHOJIWA KWA MWANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI ERICK KABENDERA

Tarehe 29 Julai 2019, majira ya saa 11 jioni, watu wasiojulikana na waliovaa kiraia, walifika nyumbani kwa Erick Kabendera eneo la Mbweni Mpigi Dar, wakitaka kumkamata.

Hata hivyo, ushirikiano wa marafiki wa Erick na majirani waliofika katika eneo la tukio, ulilazimisha watu hao kujitambulisha kuwa ni askari Polisi.

Baada ya kujitambulisha, watu hao walifanikiwa kumchukua Erick na kwenda naye kusikojulikana, wakachukua simu yake na kuifunga kiasi kwamba hakuweza tena kuwasiliana tena na wenzake.

Kufikia leo, Erick Kabendera amefikisha siku tano akiwa mikononi mwa Polisi.

Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, Polisi inatakiwa kukaa na mtu kwa muda usiozidi saa 24 kabla ya kumfikisha mahakamani. Kama itataka kukaa na mtu kwa zaidi ya muda huo, inatakiwa kupata kibali cha Mahakama.

Katika jambo hili la Kabendera; taratibu zote hizi hazijafuatwa -kwamba Polisi imekaa naye kwa zaidi ya saa 24 na haijapata ruhusa ya Mahakama kufanya hivyo.

Katika siku yake ya kwanza kushikiliwa, Kabendera alihojiwa kwa zaidi ya saa nne na maofisa wa Idara ya Uhamiaji kuhusu Uraia wake.

Ni Idara hiyohiyo ya Uhamiaji iliwahi kusema huko nyuma kwamba suala la uraia wa Kabendera halina utata.

Agosti Mosi, 2019, Kabendera alichukuliwa na askari wa Kituo cha Polisi cha Kati kitengo cha Makosa ya Mtandaoni na kuhojiwa kwa zaidi ya saa tatu kwa tuhuma za uchochezi kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari kifungu cha 52 na 53.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kumshitaki Erick Kabendera kwa makosa ya uchochezi kwa madai kwamba mnamo Julai 31 mwaka huu, alichapisha habari katika jarida la The Economist yenye kichwa cha habari kisemacho “John Magufuli is bulldozing Tanzania’s Freedom”.

Erick amenyimwa dhamana na Jeshi la Polisi ingawa dhamana ni haki yake kikatiba.

Mchana huu, Jeshi la Polisi limetuma maofisa wake kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwa Kabendera.

Kama Wakili wake, nalifuatilia jambo hili kwa karibu na nitakuwa nikitoa kwa Watanzania na Jamii ya Kimataifa kila itakapohitajika kufanya hivyo.

Imetolewa na

Jebra Kambole
Law Guards Advocates
2nd August 2019.

Kwa maelezo zaidi, tunaweza kuwasiliana kupitia

Phone: +255 717334032
Email: jebrakambole@gmail.com

PIA, SOMA:
- Mwanahabari Erick Kabendera akamatwa na Polisi nyumbani kwake; yadaiwa anaendelea na Mahojiano
 
Pole zake.Kama kweli ni yeye, basi hakutenda sawa ktk uandishi wake. Tulisoma makara zake bila kujua nani anaandika. Aliandika kwa kujifichaficha, jambo ambalo lilimpa uhuru wa kusema mawazo yake. Pamoja na haya ya wakili, sielewi kazi ya wanasheria ni nini? Je, ni kuwaokoa wenye makosa? Au kuwahakikishia hukumu wanayostahili. Naona mara nyingi mafaikio yao na majivuno ni kuona muharifu akiachiwa!

Uandikaji wa mwandishi huyu, haukuwa na staha kwa rais, hata kama anaamini rais aliyepo ni bwege. Alistahili kuheshimu nafasi hiyo.
 
Pole zake.Kama kweli ni yeye, basi hakutenda sawa ktk uandishi wake. Tulisoma makarazakr lakini bila kujua nani anaandika.Aliandika kwa kujifichaficha, jamboa ambalo lilimpa uhuru wa kusema mawazo yake. Pamoja na haya ya wakili, sielewi kazi ya wanasheria ni nini? Je, ni kuwaokoa wenye makosa? Au kuwahakikishia hukumu wanayostahili. Naona mara nyingi mafaikioa yao namajivuno ni kuona muharifu akiachiwa!

Uandikaji wa mwandishi huyu, haukuwa na staha kwa rais, hata kama anaamini rais aliyepo ni bwege. Alistahili kuheshimu nafasi hiyo.
Pata kesi mahakamani au polisi ndio utajua umuhimu na kazi ya mwanasheria
 
Hapa anahojiwa kwa uchochezi kwa sababu tu alimtaja mtu fulani. Je, haya magazeti yanayosimamiwa na musiba hayachochei? au ni kwasababu hayo magazeti yanawasema watu wenye mrengo tofauti na huyo aliyetajwa na Erick.
 
Kwa uandishi ule uliochapishwa kwenye makala kadhaa za gazeti hilo la kigeni ambazo, nilipata kuzisoma na baadhi kuzipuuza, sidhani kama anapaswa kulilia watu au Dola imhurumie.... Janga hili kalitengeneza mwenyewe kama kweli ndiye aliyeandika au kushiriki kwa namna yoyote ile.😠😠
 
Unajua kuna jambo linanitatiza:Kama Jiwe anatendea mema taifa lake kwanini ni mwoga sana wa critics? Nimekuwa nikimfuatilia Trump harakati zake. Siku zote hujibu hoja kwa hoja dhidi ya critics wake. Na mara nyingi amekuwa akiwashinda. Sasa huyu wa kwetu anaziba watu midomo aongee yeye tu. Sasa kama anajiamini hayo anayoyafanya ni kwa ajili ya watanzania basi awaache na watanzania nao watoe maoni yao!
 
Kwa uandishi ule uliochapishwa kwenye makala kadhaa za gazeti hilo la kigeni ambazo, nilipata kuzisoma na baadhi kuzipuuza, sidhani kama anapaswa kulilia watu au Dola imhurumie.... Janga hili kalitengeneza mwenyewe kama kweli ndiye aliyeandika au kushiriki kwa namna yoyote ile.
Kweni aliandika nini? Tupeni angalau link/copy nasi tuchangie
 
TAARIFA KUHUSU KUKAMATWA, KUWEKWA MAHABUSU NA KUHOJIWA KWA MWANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI ERICK KABENDERA

Tarehe 29 Julai 2019, majira ya saa 11 jioni, watu wasiojulikana na waliovaa kiraia, walifika nyumbani kwa Erick Kabendera eneo la Mbweni Mpigi Dar, wakitaka kumkamata.

Hata hivyo, ushirikiano wa marafiki wa Erick na majirani waliofika katika eneo la tukio, ulilazimisha watu hao kujitambulisha kuwa ni askari Polisi.

Baada ya kujitambulisha, watu hao walifanikiwa kumchukua Erick na kwenda naye kusikojulikana, wakachukua simu yake na kuifunga kiasi kwamba hakuweza tena kuwasiliana tena na wenzake.

Kufikia leo, Erick Kabendera amefikisha siku tano akiwa mikononi mwa Polisi.

Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, Polisi inatakiwa kukaa na mtu kwa muda usiozidi saa 24 kabla ya kumfikisha mahakamani. Kama itataka kukaa na mtu kwa zaidi ya muda huo, inatakiwa kupata kibali cha Mahakama.

Katika jambo hili la Kabendera; taratibu zote hizi hazijafuatwa -kwamba Polisi imekaa naye kwa zaidi ya saa 24 na haijapata ruhusa ya Mahakama kufanya hivyo.

Katika siku yake ya kwanza kushikiliwa, Kabendera alihojiwa kwa zaidi ya saa nne na maofisa wa Idara ya Uhamiaji kuhusu Uraia wake.

Ni Idara hiyohiyo ya Uhamiaji iliwahi kusema huko nyuma kwamba suala la uraia wa Kabendera halina utata.

Agosti Mosi, 2019, Kabendera alichukuliwa na askari wa Kituo cha Polisi cha Kati kitengo cha Makosa ya Mtandaoni na kuhojiwa kwa zaidi ya saa tatu kwa tuhuma za uchochezi kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari kifungu cha 52 na 53.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kumshitaki Erick Kabendera kwa makosa ya uchochezi kwa madai kwamba mnamo Julai 31 mwaka huu, alichapisha habari katika jarida la The Economist yenye kichwa cha habari kisemacho “John Magufuli is bulldozing Tanzania’s Freedom”.

Erick amenyimwa dhamana na Jeshi la Polisi ingawa dhamana ni haki yake kikatiba.

Mchana huu, Jeshi la Polisi limetuma maofisa wake kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwa Kabendera.

Kama Wakili wake, nalifuatilia jambo hili kwa karibu na nitakuwa nikitoa kwa Watanzania na Jamii ya Kimataifa kila itakapohitajika kufanya hivyo.

Imetolewa na

Jebra Kambole
Law Guards Advocates
2nd August 2019.

Kwa maelezo zaidi, tunaweza kuwasiliana kupitia

Phone: +255 717334032
Email: jebrakambole@gmail.com
Pata kesi mahakamani au polisi ndio utajua umuhimu na kazi ya mwanasheria
Kwa nini unaombea kupata kesi?
 
Back
Top Bottom