Zitto
Former MP Kigoma Urban
- Mar 2, 2007
- 1,562
- 10,880
TAARIFA KUHUSU KUKAMATWA, KUWEKWA MAHABUSU NA KUHOJIWA KWA MWANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI ERICK KABENDERA
Tarehe 29 Julai 2019, majira ya saa 11 jioni, watu wasiojulikana na waliovaa kiraia, walifika nyumbani kwa Erick Kabendera eneo la Mbweni Mpigi Dar, wakitaka kumkamata.
Hata hivyo, ushirikiano wa marafiki wa Erick na majirani waliofika katika eneo la tukio, ulilazimisha watu hao kujitambulisha kuwa ni askari Polisi.
Baada ya kujitambulisha, watu hao walifanikiwa kumchukua Erick na kwenda naye kusikojulikana, wakachukua simu yake na kuifunga kiasi kwamba hakuweza tena kuwasiliana tena na wenzake.
Kufikia leo, Erick Kabendera amefikisha siku tano akiwa mikononi mwa Polisi.
Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, Polisi inatakiwa kukaa na mtu kwa muda usiozidi saa 24 kabla ya kumfikisha mahakamani. Kama itataka kukaa na mtu kwa zaidi ya muda huo, inatakiwa kupata kibali cha Mahakama.
Katika jambo hili la Kabendera; taratibu zote hizi hazijafuatwa -kwamba Polisi imekaa naye kwa zaidi ya saa 24 na haijapata ruhusa ya Mahakama kufanya hivyo.
Katika siku yake ya kwanza kushikiliwa, Kabendera alihojiwa kwa zaidi ya saa nne na maofisa wa Idara ya Uhamiaji kuhusu Uraia wake.
Ni Idara hiyohiyo ya Uhamiaji iliwahi kusema huko nyuma kwamba suala la uraia wa Kabendera halina utata.
Agosti Mosi, 2019, Kabendera alichukuliwa na askari wa Kituo cha Polisi cha Kati kitengo cha Makosa ya Mtandaoni na kuhojiwa kwa zaidi ya saa tatu kwa tuhuma za uchochezi kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari kifungu cha 52 na 53.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kumshitaki Erick Kabendera kwa makosa ya uchochezi kwa madai kwamba mnamo Julai 31 mwaka huu, alichapisha habari katika jarida la The Economist yenye kichwa cha habari kisemacho “John Magufuli is bulldozing Tanzania’s Freedom”.
Erick amenyimwa dhamana na Jeshi la Polisi ingawa dhamana ni haki yake kikatiba.
Mchana huu, Jeshi la Polisi limetuma maofisa wake kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwa Kabendera.
Kama Wakili wake, nalifuatilia jambo hili kwa karibu na nitakuwa nikitoa kwa Watanzania na Jamii ya Kimataifa kila itakapohitajika kufanya hivyo.
Imetolewa na
Jebra Kambole
Law Guards Advocates
2nd August 2019.
Kwa maelezo zaidi, tunaweza kuwasiliana kupitia
Phone: +255 717334032
Email: jebrakambole@gmail.com