Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 33,615
- 40,161
Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linatoa taarifa ya tukio la mauaji lililotokea mnamo tarehe 16 mwezi wa 9 mwaka 2025 saa 12:50 jioni katika Kitongoji cha Ululu, Kijiji na Kata ya Idiwili, Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe.
Katika tukio hilo, Evaristo Zabroni Mwambogolo, mwenye umri wa miaka 28, Mkuliima Mkazi wa Ululu Wilaya ya Mbozi alichomwa kisu kifuani, eneo la moyo, na mtu anayefahamika kwa jina la Exavery Jamsoni Mwaweza, baada ya mabishano ya mpira wa miguu kati ya timu za Simba na Yanga.
Marehemu alijeruhiwa vibaya na alifariki dunia akiwa njiani akipelekwa kwenye Zahanati ya Iyula iliyopo Wilaya ya Mbozi kwa ajili ya matibabu.
Uchunguzi wa awali, umeonesha chanzo cha tukio hilo ni ushabiki wa mpira wa timu ya Simba na Yanga kati ya marehemu na mtuhumiwa, ambapo mtuhumiwa alitumia kisu alichokuwa nacho wakati wa ugomvi huo na mara baada ya kutenda kosa hilo, alitoroka kusikojulikana.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linaendelea na msako mkali wa kumtafuta mtuhumiwa huyo ili akamatwe na aweze kuhukumiwa kwa mujibu wa Sheria.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linatoa wito kwa wananchi kuepuka kujichukulia sheria mkononi, na kutokujihusisha na vitendo vya vurugu vinavyoweza kusababisha madhara makubwa, ikiwemo vifo pamoja na upotevu wa maisha, na linawataka kuendeleza kudumisha amani, mshikamano na utulivu, hasa wakati wa mijadala au mabishano ya kawaida, ikiwa michezo.
WATU WATATU WAFARIKI KATIKA AJALI YA GARI NA BAJAJI DEREVA ATAFUTWA-TUNDUMA-MOMBA-SONGWE
Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linatoa taarifa ya tukio la ajali ya barabarani iliyotokea mnamo tarehe 15 mwezi wa 9 mwaka 2025 saa 03:00 asubuhi, katika eneo la Nyerere, barabara kuu ya Tunduma – Sumbawanga, Kata ya Chipaka, Tarafa ya Tunduma, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Songwe.
Katika ajali hiyo, gari lenye namba T.525 ACB aina ya Canter, ikiwa inaendeshwa na dereva ambaye hajafahamika hadi sasa kwa kuwa alikimbia mara baada ya tukio hilo, baada ya kuigonga Bajaji yenye namba za usajili MC 308 EXE iliyokuwa ikiendeshwa na Silas Malongo, mwenye umri wa miaka 23, Mkazi wa Mwaka Mji wa Tunduma Wilaya ya Momba, ambaye ni dereva wa bajaji hiyo, na alifariki dunia hapo hapo katika ajali hiyo.
Katika ajali hiyo, ilisababisha vifo vya watu watatu ambao ni Ibrahim Kibanda, miaka 16, mwanafunzi na mkazi wa Malangali, majina ya marehemu wengine wawili bado hayajafahamika, na maiti zao zimehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Tunduma. Aidha, katika ajali hiyo pia imesababisha majeruhi wa watu wawili ambao ni Venance Jail, miaka 34, ambaye ameumia mguu wa kulia na Loyce Kandonga Jackson msichana, miaka 15, mwanafunzi ambaye ameumia mguu wa kushoto wote wakazi wa Mji wa Tunduma.
Baada ya uchunguzi wa ajali hiyo, unaonyesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari T.525 ACB aina ya Canter, ambaye aliigonga bajaji hiyo kwa uzembe kutokana na kutokuzingatia sheria na taratibu za usalama barabarani na kutojali watumiaji wengine wa barabara.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linaendelea na msako mkali ili kumkamata dereva wa Canter aliyekimbia mara baada ya kusababisha ajali hiyo, pia linaendelea kuhimiza madereva wote kuzingatia sheria za usalama barabarani, kuendesha kwa tahadhari, na kuwazingatia watumiaji wengine wa barabara kwa usalama wa kila mtumiaji wa barabara.
Imetolewa na:
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Songwe.