Mmiliki wa Tella Maande Hotel Arusha afariki ajalini

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2007
Posts
5,554
Reaction score
2,160
Chris Maeda ambaye ni mmiliki mwenza na Edmund Maeda wa Hotel ya TELLA MAANDE iliyopo Sakina amefariki kwa ajali ya gari usiku wa kuamkia leo maeneo ya Sakina.Inasemekana wakati anaelekea nyumbani kwake Ngaramtoni alikutana na Land Cruiser iliyokuwa ina-overtake ikamfuata upande wake marehemu alikuwa kwenye gari ndogo ambapo alifariki papo hapo. RIP Chris
 
Mungu amlaze anapo stahili huyu billionaire wetu....watu wa Arusha tunaendelea kupata mapigo kila leo mabillionaire wetu wanaondoka.

Poleni sana wafiwa.

cc Mungi Crashwise Arushaone
 
Last edited by a moderator:
Bilionea mwingine katutoka, Dar change of lifestyle inahitajika huko chugga, mabilionea wataisha sasa. Mbona Marekani mabilionea wanakufa na miaka tisini. Sasa chugga unakuta bilionea anaendesha gari bila hata kufunga mkanda na viroba juu. Bilionea ajiri dereva.

Anyway Rest in Peace bilionea mmiliki wa hotel
 
Nyoosha maelezo ajali ziko zaidi aina nyingi ndugu
 
Sasa chugga unakuta bilionea anaendesha gari bila hata kufunga mkanda na viroba juu. Bilionea ajiri dereva.

Anyway Rest in Peace bilionea mmiliki wa hotel

Shida la matajiri wa Arusha wengi ni Elimu na ustaraabu cimewapita pembeni sana na wanaamini kuvunja sheria kama kutofunga mkanda kwenye magari yao ndio ujanja/ubabe yaani kana kutomwogopa polisi/traffic kumbe sheria hz ni for their benefits.
 
Tangazo LA kifo ilo LA billionea.
 
Aliyefariki ni Cristopher Maeda kwenye ajali. Mbia mwenza wa Hotel ya Tellar Mande ni Edwin Tarimo Nimeweka sawa tu Poleni wafiwa
 
I hope sio Chris Maeda wa regional! Anyway this is a common name anyways!
 
Huyu ni Chris Maeda wa Regional kumbe! Very bad! Ila Muache kuwabandika watu Majina ya mabilionea! Ni Mtu tu anayejiweza na aliyefanikiwa!
 
Chris Maeda ambaye ni mmiliki mwenza na Edmund Maeda wa Hotel ya TELLA MAANDE iliyopo Sakina amefariki kwa ajali ya gari usiku wa kuamkia leo maeneo ya Sakina.Inasemekana wakati anaelekea nyumbani kwake Ngaramtoni alikutana na Land Cruiser iliyokuwa ina-overtake ikamfuata upande wake marehemu alikuwa kwenye gari ndogo ambapo alifariki papo hapo. RIP Chris

Mkubwa.......Edwin Tarimo ndiyo mwenye Tellamande Hotel

Habari hii siyo ya kweli............acha kupotosha umma wewe na kama kitu haujui subiria uambiwe.

Christopher Maeda alikuwa ni rafiki yake mkubwa sana na Mr Edwin Tarimo ambaye ndiyo mmliki wa Tellermande Motel.

Na ile muda alipoondoka pale hotelini Christopher alikuwa na rafiki yake mmoja jina limenitoka aliyekuja naye pale wakawa wanakunywa ila ghafla tu hajawaaga hata na katika dk yapata kumi ndipo Edwin akapigiwa simu ya kwamba rafiki yako amepata ajali na wakatoka na huyo rafiki yake Christopher aliyekuja naye na walipofika eneo la tukio mita yapata 300 hotel ilipo ndipo hawajaamini kilichotokea na Mwenyenzi Mungu ampe Marehemu pumziko la milele shambani mwa Bwana!
 
Mkubwa.......Edwin Tarimo ndiyo mwenye Tellamande
Hotel

Habari hii siyo ya kweli............acha kupotosha umma wewe na kama
kitu haujui subiria uambiwe.

Christopher Maeda alikuwa ni rafiki yake mkubwa sana na Mr Edwin Tarimo
ambaye ndiyo mmliki wa Tellermande Motel.

Na ile muda alipoondoka pale hotelini Christopher alikuwa na rafiki yake
mmoja jina limenitoka aliyekuja naye pale wakawa wanakunywa ila ghafla
tu hajawaaga hata na katika dk yapata kumi ndipo Edwin akapigiwa simu ya
kwamba rafiki yako amepata ajali na wakatoka na huyo rafiki yake
Christopher aliyekuja naye na walipofika eneo la tukio mita yapata 300
hotel ilipo ndipo hawajaamini kilichotokea na Mwenyenzi Mungu ampe
Marehemu pumziko la milele shambani mwa Bwana!

Mnampangia Mungu mahali pa kumlaza marehemu siyo? Mlevi, jambazi, fisadi
nk. walazwe pema peponi pasipo wao kutubu dhambi zao kabla
mauti kuwakuta. Kataeni kudanganywa na viongozi wenu wa dini
waliofilisika kiroho! Viongozi hao wa dini wamekwisha hukumiwa kwenda
jehanamu tayari kwa kupotosha maandiko, sasa wanawadanganya ili mwende wote jehanamu. Baada ya kifo ni hukumu! Mbona hamshitukii??
 
Mungu amlaze anapo stahili huyu billionaire wetu....watu wa Arusha tunaendelea kupata mapigo kila leo mabillionaire wetu wanaondoka.

Poleni sana wafiwa.

cc Mungi Crashwise Arushaone

Si bure pana mkono wa mtu haiwezekani ndani ya miaka miwili mabilionea waliokufa kwa vifo vya kizembe na vya kushangaza vinafika hata ishirini hela inaongezeka matatizo nayo yanaongezeka R.I.P bilionea
 
Last edited by a moderator:
Mnampangia Mungu mahali pa kumlaza marehemu siyo? Mlevi, jambazi, fisadi
nk. walazwe pema peponi pasipo wao kutubu dhambi zao kabla
mauti kuwakuta. Kataeni kudanganywa na viongozi wenu wa dini
waliofilisika kiroho! Viongozi hao wa dini wamekwisha hukumiwa kwenda
jehanamu tayari kwa kupotosha maandiko, sasa wanawadanganya ili mwende wote jehanamu. Baada ya kifo ni hukumu! Mbona hamshitukii??

Umenikuna sana hapo mwisho hawakawii kukuambia unahukumu watu wa ajabu sana hawa.
 
Mkubwa.......Edwin Tarimo ndiyo mwenye Tellamande Hotel

Habari hii siyo ya kweli............acha kupotosha umma wewe na kama kitu haujui subiria uambiwe.

Christopher Maeda alikuwa ni rafiki yake mkubwa sana na Mr Edwin Tarimo ambaye ndiyo mmliki wa Tellermande Motel.

Na ile muda alipoondoka pale hotelini Christopher alikuwa na rafiki yake mmoja jina limenitoka aliyekuja naye pale wakawa wanakunywa ila ghafla tu hajawaaga hata na katika dk yapata kumi ndipo Edwin akapigiwa simu ya kwamba rafiki yako amepata ajali na wakatoka na huyo rafiki yake Christopher aliyekuja naye na walipofika eneo la tukio mita yapata 300 hotel ilipo ndipo hawajaamini kilichotokea na Mwenyenzi Mungu ampe Marehemu pumziko la milele shambani mwa Bwana!

sasa badala ya kutueleza hali halisi mnaanza tena kushindana kuonyesha nani ana mjua nani. je tushike lipi na la nani? wabongo bhana!
 
Chris Maeda ambaye ni mmiliki mwenza na Edmund Maeda wa Hotel ya TELLA MAANDE iliyopo Sakina amefariki kwa ajali ya gari usiku wa kuamkia leo maeneo ya Sakina.Inasemekana wakati anaelekea nyumbani kwake Ngaramtoni alikutana na Land Cruiser iliyokuwa ina-overtake ikamfuata upande wake marehemu alikuwa kwenye gari ndogo ambapo alifariki papo hapo. RIP Chris

Kila eneo kifo bas makubwa magari binaf s rip
 
Ama kweli majanga ni mengi huku tunakoelekea!

Pumzika kwa Amani Christopher!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom