Mmiliki IPTL akataa mitambo kubadilishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mmiliki IPTL akataa mitambo kubadilishwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Nov 17, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,389
  Likes Received: 5,670
  Trophy Points: 280
  Na Margareth Kinabo, Maelezo

  KAMISHNA wa Nishati na Madini, Bashir Mrindoko amesema haitawezekana kwa mitambo ya kuzalisha umeme ya kampuni ya IPTL, ambayo inaendeshwa kwa kutumia dizeli, kuigeuza ili ianze kutumia gesi asilia kutokana na kutopata ridhaa ya mwenye mali.

  Rais Jakaya Kikwete aliagiza kuwa kazi hiyo ya kuigeuza mitambo hiyo ili itumie gesi na hivyo kupunguza gharama za nishati ya umeme kwa watuamiaji, ifanywe kwa haraka baada ya kuona zoezi hilo likisuasua.

  Lakini agizo la Kikwete la kuibadili mitambo hiyo ya IPTL, ambayo inamilikiwa na Mechmar Sorporation BhDd (asilimia 70) ya Malaysia na VIP Engineering & Marketing Ltd ya Tanzania, inaonekana halitawezekana kwa mujibu wa Mrindoko.

  Akizungumza na waandishi kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam, Mrindoko alisema wamiliki wa mitambo hiyo hawajatoa ridhaa ya kuibadili ili iendeshwe kwa kutumia gesi asilia.

  "Mitambo ya IPTL inaweza kutumia gesi ikiwa Serikali itafikiana na mwenyemali ili atoe ridhaa," alisema Mrindoko akizungumzia jenereta hizo za IPTL ambayo ina uwezo wa kuzalisha megawati 100 za umeme na ambayo ilikuwa inasemekana inatafuna Sh3.67 bilioni kwa mwezi ikiwa ni gharama za uzalishaji umeme.

  Mrindoko alifafanua kwamba kutopatikana kwa ridhaa ya mwenye mali kumesababishwa kwa kiasi kikubwa na kesi iliyo mahakamani baada ya IPTL kulishtaki Shirika la Umeme (Tanesco) kwenye mahakama ya usuluhishi wa kibiashara ya Paris, Ufaransa.

  Pia alisema mfumo wa miundombinu ya kusafirisha gesi hiyo jijini Dar es salaam haitoshelezi mahitaji.

  Tukikamilisha miundombinu ya gesi na kupata ridhaa ya mwenyemali, tutaweza kubadilisha mtambo huo ili utumie gesi badala ya mafuta, alisema Mrindoko.

  Alisema matumizi ya gesi sasa yameongezeka kwani kuna viwanda 36 vinavyotumia nishati hiyo.

  Alisema mahitaji ya umeme nchini kwa sasa yamefikia megawati 700 na kwamba tatizo hilo limetafutiwa suluhisho lake katika mpango kabambe wa mfumo wa Umeme wa mwaka 2007- 2031.

  Alisema mpango huo unahitaji dola 8 hadi 10 bilioni za Kimarekani bilioni nane hadi 10, hivyo wawekezaji binafsi wanakaribishwa kushirikiana na serikali.
   
 2. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Hawa IPTL wanajua kuwa hatua uwezo wa kukataa umeme wao, wanajua udhaifu wetu katika kufanya maamuzi.
   
 3. M

  Magezi JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  wasubiri tu magufuli awe waziri wa nishati na madini cha moto watakiona. Hivi kwa nini wewe Kikwete haumpi Magufuli wizara hiyo tukaona maendeleo?? naakawafunga akina rostam???
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Nov 18, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Ni vizuri siku nyingine uonyeshe source ya bandiko lako.
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Nov 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,389
  Likes Received: 5,670
  Trophy Points: 280

  misamaha ya madini ataipata wapi jamani;mawaziri ndio dili zake uweke huyu dk 3 mbele kwa madudu ya wizara ya madini si anakimbia ofisi baada ya wiki...kaka ile wizara ya mlo masha akuwekwa pale bahati mbaya...kabla ya kuamishwa
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Nov 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,389
  Likes Received: 5,670
  Trophy Points: 280
  aiseeeee

  basi ni habarileo.co.tz
   
Loading...