Mmh matatizo makubwa hudumisha ndoa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mmh matatizo makubwa hudumisha ndoa?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Aug 28, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,061
  Likes Received: 5,552
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Hata ndoa zenye afya njema bado hukutana na matatizo na tofauti kati ya ndoa imara na zile zisizo imara ni namna matatizo yanavyoshughulikiwa hasa matatizo madogomadogo.

  Pia wapo wana ndoa ambao mmoja wao (hasa mwanaume) hata kama kuna matatizo (problems) katika ndoa huendelea kukataa kwamba hakuna tatizo lolote, ukweli ni kwamba ku-ignore tatizo hakufanyi tatizo liondoke bali linazidi kuwa tatizo kubwa.

  Matatizo makubwa ya ndoa nyingi ni kushindwa kutatua tatizo lililopo wakat bado linaonekana dogo kama vile kukosa mawasiliano mazuri kati ya wanandoa.

  Utafiti mwingi unaonesha kwamba matatizo makubwa kama kufiwa mtoto, kupunguzwa kazi, kuuungua nyumba, ajali, kufilisika business, kuugua ugonjwa mzito nk kawaida huimarisha ndoa zaidi tofauti na wengi wanavyofikiria na matatizo madogomadogo kama vile kutomsikiliza mwenzako, kuwa mwongo, kutomjali mwenzako, kutomzungumzia mambo ya sex kama mmoja haridhiki na kuacha matatizo haya matatizo madogo kana kwamba hayapo huweza kuharibu ndoa na kuifikisha mahali ambapo wengi hawakutegemea.

   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,061
  Likes Received: 5,552
  Trophy Points: 280
  Iddi njema jamani
   
 3. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ni kweli haswa kwenye uongo ni janga la ndoa nyingi maana hakuna siri chini ya mbingu
   
Loading...