Mmetangaza nia ya kuanza mikutano. Je, mna nini cha kutushawishi?

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Kamanda mkuu Chadema amesema ataanza mikutano ya kunadi sera za chama chake kwa wananchi sababu zuio aliloliweka mkuu wa nchi limewafanya wakose nguvu na ushawishi.

Ameenda mbali na kusema kuwa hawaogopi risasi wala mabomu (nafikiri anajua lazima zitapigwa maana anasema kule shambani ziliwaka)

Kwa namna Chama tawala kilivyojitahidi kusafisha makosa yake kwa kudhibiti rushwa, ubadhilifu, kurejesha nidhamu kwa watumishi wa umma na kujenga miundombinu ikiwemo miradi kama Sgr, JNHHP n.k

Nauliza hawa Chadema watakuwa na sera gani ya kuwashawishi wananchi ili wawe na imani nao kama zamani? Maana ilipotoka ile orodha ya mafisadi pale Mwembe Yanga chini ya Dk. Slaa, Chadema ilipata kick na ikaonekana kama chama cha ukombozi.

Leo hii wananchi hawana imani nao tena. Hasa lilipotokea lile tukio la kubadili gia angani na Dk akaamua kujiengua(wanaonekana kama wahuni tu)

Isiwe ikawa ni hulka tu ya kamanda mkuu kuwa anafurahi watu wakipigwa risasi (walalahoi) maana kwa amri aliyoitoa mkuu wa nchi na yeye anasema ataingia kwa lazima kumwaga sera huenda damu za watu ambao hata hawanufaiki na siasa za Bongo zikamwagika (kumbukeni lile tukio Morogoro).
 
chagu wa malunde,

Kiukweli hatujawa wajinga kwa kuhadaiwa na nidhamu serikalini, ufisadi,elimu bure Kama inavyozungumzwa midomoni lakini ukipeleka mtoto shule ndiyo utajua ni elimu bure au bule.

Hivyo wenye akili zetu ziwe za nyumbu mambo tunayaona hatujalala usingizi tunajua maendeleo ni Nini na porojo ni Nini bila kusahau propaganda ni nini.
 
...Isiwe ikawa ni hulka tu ya kamanda mkuu kuwa anafurahi watu wakipigwa risasi (walalahoi) maana kwa amri aliyoitoa mkuu wa nchi na yeye anasema ataingia kwa lazima kumwaga sera huenda damu za watu ambao hata hawanufaiki na siasa za Bongo zikamwagika (kumbukeni lile tukio Morogoro).
Ili kamanda wa anga apate picha za kuwapelekea wazungu ili wamsaidie kushika dola.
 
Back
Top Bottom