John Joseph Pombe Magufuli hakutaka wala hakuwazia kuwa Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania. Wiki ya Mwisho ya May 2015 kama sijakuosea alienda kukagua Maendeleo ya Daraja la Kigamboni akasema anataka liishe na lizinduliwe na Dr. Jakaya ili asije Rais mwingine akajifanya yeye ndie kalijenga!!!!
Siku Dr. JAKAYA akimtambulisha Rasmi kuwa Mgombea wa Chama July 12, 2015 Dodoma anasema yeye( Jakaya) ndie aliemwambia JPM akachukue form za Urais nae Magufuli akamuuliza atatosha? JK akamwambia kachukue kutosha au kutokutosha kwako itajulikana Dodoma. Dr. Magufuli hakujiandaa kuwa Rais ni jambo la wazi na hilo linaweza kuwa jambo litakalomsaidia kufanya vizuri, ukijiandaa unakuwa na Makundi mengi sana yanayokusaidia yakitegemea fadhila, makundi hayo yamemsumbua sana JK.