Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba chadema mmepigwa na dhoruba kali ambalo mtahangaika nalo kwa muda sana na kupoteza muda mwingi wa kutumikia wananchi na pia kujenga imani ya Chama chenu na viongozi wenu mbele ya Umma; Lakini yote ni sehemu ya siasa za ushindani katika demokrasia ya uliberali, kote, marekani n.k; Personal attacks ni sehemu ya mchezo wa kisiasa, ndio maana unaitwa mchezo mchafu, kwahiyo msilaumu CCM kwa hilo, kwani hata Chadema ni mabingwa wa personal attacks, kama sehemu ya mchezo huu mchafu;
Bila uangalifu, jambo hili litaipelekesha Chadema kwa muda mrefu sana, miezi sita, mwaka, huku Dr. Slaa akijikuta akitumia muda mwingi kujibu hoja hii badala ya kujadili masuala muhimu huko majukwaani; Ukichanganya na tetesi kwamba pia anataka kumsimamisha Josephine Jimbo La Kawe kwa nguvu, licha ya uwepo wa Mbunge mahiri Halima Mdee pale, there is a big chance kwamba Dr. Slaa's popularity itaporomoka kwa kasi ya ajabu, na pengine jina lake kuwa irrelevant katika political landscape of the country ifikapo 2015;
Vinginevyo yote ni katika kutumikia wananchi, Vyama ni njia tu; Hata Wassira, ambae ni moja ya nguzo kuu ya chama chetu cha mapinduzi leo, huko nyuma alihama chama na kuwa Mbunge wa Bunda kupitia NCCR mageuzi, akikishambulia Chama Chetu kwa hoja nzito majukwaani, leo hii wajumbe wa Mkutano mkuu wetu wa taifa (CCM), wanampa Wassira kura nyingi kuliko hata majina yanayotajwa kuwa na uwezo wa kubeba tiketi ya chama chetu ngazi ya Urais 2015; Sisi sote ni watanzania, vyama huja baadae;
Wanachadema, hizi ndio siasa za zama za leo, jipangeni;