Mmegundua nini kuhusu ITV?

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
3,865
5,683
Nitaeleza kutoka hivi karibuni kurudi nyuma!

1. Siku hizi wanaripoti kweli kweli habari zihusuzo 'kuijenga' serikali. Natumia mfano wa leo kwanza;
‐ wameripoti 'kikamilifu' tukio la machinga aliyefariki wakati wa kuokoa mali zake. Mwandishi alitembea kweli kweli kufuatilia suala hilo huku akikomaa kusema amegongwa wakati anakimbizwa ingawa wahusika pale na kaka wa marehemu hawakukomaa sana kusema hivyo. Mwandishi alitembelea kila sehemu kwa juhudi kubwa huku waliohojiwa wote wakionekana kuwa na mawazo negative kwa gov.

‐ wameripoti 'machinga mwanza wakosa maeneo ya kufanyia biashara'. Lakini tulichoona ni kuwa machinga wapo katika maeneo yao yale yale isipokuwa kuna mpango wa kuwapanga sehemu 50 zilizoandaliwa na leo walikuwa na kikao na dc kuelezana hilo. Watu wachache waliohojiwa na itv ni wale tu walioonekana kukosoa mpango huo tu!

2. Wakati wa jpm (r.i.p) walikuwa wanaripoti habari zinazosifia serikali tu.

3. Wakati wa kikwete walikuwa wanaripoti kwelikweli habari zinazohusu 'kuijenga' serikali, sitosahau nilishuhudia siku moja kipindi cha malumbano ya hoja kama sikosei kikiongezewa muda kabisa. Siku hiyo kulikuwa na nape vs mnyika. Pia maandamano na migomo mbalimbali vilipewa coverage ya nguvu. Mtangazaji mmoja, Masako, aliyekuwa anaendesha kipindi cha kipima joto, alitamka maneno haya mbele ya waalikwa wawili (mmoja afande na mwingine raia) aliowaalika katika kipindi chake, 'ukweli ni kuwa........., ingawa afande hapa anajitahidi kutetea lakini huo ndo ukweli!'. Kauli hii ilishangaza kidogo sababu kama mtu wa media, tena aliyewaalika watu kupimana hoja hakupaswa kusimamia upande. Aliteleza hivyo sababu ndo ulikuwa msimamo wa kituo ulioonekana kipindi hiko.

4, wakati wa Mkapa (r.i.p) walikuwa wanaripoti zaidi habari zinazosifia serikali tu.

Hicho ndicho nilichogundua kuhusu itv. Chini ya mkapa, sikuwa mkubwa
 
Dini✓,

sio wa upande wao, na ndio hata humu Jf wajinga wengi Wana chuki hizo za kidini, usidhani wanamchukia kwa lipi, kwa utafiti wangu
 
Kipindi cha magu walianza ripoti migogoro ya wafugaji na wakulima hasa morogoro jamaa akawapiga mkwara

Tangu hapo sikuwahi sikia habari za migogoro tena
 
Nachojua Mimi ITV wana balance habari vizuri sana, hawana upendeleo.

Kuhusu awamu ya magufuli, hakuna ambaye angeponda serikali yake Labda ka mm a hajitaki
 
Back
Top Bottom