"Mmeagiza Tujiajiri — Lakini Mnatumaliza"

"Mmeagiza Tujiajiri — Lakini Mnatumaliza"

PlataOPlomo

Member
Joined
Jun 14, 2025
Posts
35
Reaction score
25
#JusticeForPeachyVillage #SamiaTusikie #TanzaniaYaHaki #StopCorporateImpunity #Uchaguzi2025 #TunakufaKimya

Mama Samia Suluhu Hassan —
Mmehimiza Watanzania tujiajiri. Tujitume. Tuvumilie.
Sisi Peachy Village Company Ltd — tulitii. Tukaamini. Tukawekeza kila kitu tulichokuwa nacho.

Benki ya CRDB — kwa kutumia jina letu bila ruhusa yetu wala maamuzi ya bodi — walifungua akaunti bandia kwa jina la kampuni yetu.
Hakukuwa na saini.
Hakukuwa na maombi.
Hakukuwa na power of attorney.
Na kwa akaunti hiyo haramu:
✅ Tumepoteza mamilioni (TZS 607M+)
✅ Tumekosa tenda
✅ Tumepoteza wateja
✅ Biashara yetu imekufa.
Lakini leo — tumevunjwa.
Na si kwa kosa letu.

Tukaenda BoT — Bank of Tanzania.
Walikubali CRDB walikosea.
Lakini hawakutuambia fidia.
Wala hawakutusaidia.
Na leo?

CRDB wanatushitaki sisi — kwa kesi waliyoisababisha wao!
Hili ni jinai la kiutawala.
Huu ni ukatili wa mfumo.

Na tunapolalamika — tunatishwa kimya kimya.
“Fanyeni biashara, siyo kusingizia,” mtu mmoja alituambia.
Mama, huu ni ujumbe wa kilio.
Mama, tunapiga magoti.
Mnatuambia tujiajiri. Lakini tukijaribu kujikwamua — tunapigwa mtama mbele ya vyombo vya haki navyo vinatazama.
Tunakuomba — ingilia kati. Usikie kilio cha SME zilizovunjwa kwa mikono ya taasisi kubwa.
Kama sisi tumeweza kufanyiwa hivi, bila msaada — nani atakuwa salama kesho?

Mama, tunaomba HAKI. Si huruma.

Haki ya kufidiwa. Haki ya kusikilizwa. Haki ya kulindwa.
Tumeandika. Tumepeleka ushahidi. Tumevumilia.
Lakini sasa tunalia hadharani.

#JusticeForPeachyVillage
#SamiaTusikie
#TanzaniaYaHaki
#Uchaguzi2025
 
Attachments

Mungu awaongoze, but jaribuni kutumia wanasheria kwenye hili katika kupata solution, huyo mama hasikii la mtu kwa sasa
Shukrani, lakini kumeshindikana kote na ndio maana tunawahusisha waTanzania kwa sababu kelele zetu huwa ni msaada tosha.. Naomba support ya kushare na kutag ili tuweze kutendewa HAKI . Tunanyaraka na ushahidi uliojitosheleza.
 
Swala linaloitwa Haki kwenye nchi hii ya Tanzania? Ni kama msamiati mpya Taasisi ni kama hazitambui, Watu wanaonewa Sana wanapokwa Sana Haki zao, lakini Yana Mwisho! Vyombo vya Haki havitoi Haki, Pazeni sauti yamkini msaada utatokea na kupata Haki zenu
 
Kwa wana sheria kumeshindikana vipi, maana mtu ukiwa na mgogoro unahaki ya kwenda mahakamani kupata haki yako, tafuta wanasheria wazuri. Pia unaleta malalamiko yako kwa watanzania kwa kutumia lugha wasiyoifahamu vizuri , ngumu sana kufikia lengo
 
Poleni.

Ila hii tasrifa imeanzia katikati,

Haijaeleza nyie mnajishughurisha na nini.
Tatizo lilianzia wapi,
Ilikuwaje CRDB wakafanya hivyo
N.k
 
Jambo hili ungelipeleka kwenye jukwaa linalosomwa na watu wengi kama jukwaa la hoja mchanganyiko
Shukrani, lakini kumeshindikana kote na ndio maana tunawahusisha waTanzania kwa sababu kelele zetu huwa ni msaada tosha.. Naomba support ya kushare na kutag ili tuweze kutendewa HAKI . Tunanyaraka na ushahidi uliojitosheleza.
 
Labda mahakamani mnapoteza mda.

Mngeanza na press conference ya msisitizo kwenye media then video clip mshare tiktok .

Kichwa cha habari kiwe : CRDB wametutapeli.

Muhimu muwe na ushahidi wa kutosha. CRDB watawatafuta wenyewe

Ubwela ubwela!!!
 
Alafu kingine ukiachana na Polepole , unataka mh. Rais asome na hiyo username Plata o plomo Au?
 
Swala linaloitwa Haki kwenye nchi hii ya Tanzania? Ni kama msamiati mpya Taasisi ni kama hazitambui, Watu wanaonewa Sana wanapokwa Sana Haki zao, lakini Yana Mwisho! Vyombo vya Haki havitoi Haki, Pazeni sauti yamkini msaada utatokea na kupata Haki zenu
Shukrani , Tunaomba Msaada wa Kupaziwa Sauti huenda kelele zikiwa nyingi Mitandaoni huenda wakasitisha na kutenda inavyopaswa ili kutupatia HAKI zetu.... Kama Kuna UOVU unapangwa au kutengenezwa basi waone Aibu na wenye Hatia . Mitandao mbalimbali pia itakua ni sehemu ya msaada pamoja na kutag bank husika na Samia Suluhu Hassan..
 
Swala linaloitwa Haki kwenye nchi hii ya Tanzania? Ni kama msamiati mpya Taasisi ni kama hazitambui, Watu wanaonewa Sana wanapokwa Sana Haki zao, lakini Yana Mwisho! Vyombo vya Haki havitoi Haki, Pazeni sauti yamkini msaada utatokea na kupata Haki zenu
Shukrani , Tunaomba Msaada wa Kupaziwa Sauti huenda kelele zikiwa nyingi Mitandaoni huenda wakasitisha na kutenda inavyopaswa ili kutupatia HAKI zetu.... Kama Kuna UOVU unapangwa au kutengenezwa basi waone Aibu na wenye Hatia .

Mitandao mbalimbali pia itakua ni sehemu ya msaada pamoja na kutag bank husika na Rais Samia Suluhu Hassan.

TUNA NJIA NYINGI ZA KUWAFANYA WAWAJIBIKE IKIWEMO KUANDAA UTARATIBU WA WATEJA NA WATU WOTE WENYE MALALAMIKO YENYE USHAHIDI ULIOSHIBA TUKAKUTANA KWA PAMOJA NA KUELEZA UMMA KADHIA NA UTWEZAJI WA HAKI NA KUWAONYESHA KUWA SOTE HATUKO SALAMA KAMA HATA WANAOPASWA KUSIMAMIA HAKI NA KUWAJIBISHA HAWAWAJIBISHI NI VIPI USALAMA WA AMANA ZA WATEJA ZITAKUA SALAMA KUTOKANA NA MATENDO YA KINYUME NA TARATIBU.

TUAMKE TUUNGANE KUKOMESHA UNYANYASAJI, UTWEZAJI NA KUTOWAJIBIKA KWA WATOA HUDUMA WOTE NAOMBA NIONGOZE HILI GURUDUMU KWA NIA NJEMA NA MAPENZI MEMA YA NCHI YETU KWA SABABU HATUWEZI KURUHUSU WATU WACHACHE WAAHARIBU TASWIRA YA NCHI NA SERIKALI YETU HASA KATIKA SUALA LA UTAWALA BORA.

HATA KUWA MBALI NA HUDUMA FULANI KWA SABABU ZENYE MASHIKO NI SEHEMU YA KUONYESHA KUGUSWA NA UKIUKWAJI NA VIASHIRIA VYA KUTOWAWAJIBISHA WATOA HUDUMA WANAOKWENDA KINYUME NA UTAWALA BORA NA UWAJIBIKAJI HASA WANAPOKOSEA.
 
Labda mahakamani mnapoteza mda.

Mngeanza na press conference ya msisitizo kwenye media then video clip mshare tiktok .

Kichwa cha habari kiwe : CRDB wametutapeli.

Muhimu muwe na ushahidi wa kutosha. CRDB watawatafuta wenyewe

Ubwela ubwela!!!
Tupo tayari kushirikiana na yeyote atakaetusapoti kwa namna yoyote katika kutekeleza mawazo mazuri ya namna hii , kwa sababu media hazitupi ushirikiano pamoja na kutuma SHAHIDI na wengine wanataka pesa , Kama Kuna yeyote anaeguswa na yupo tayari kutuunganisha na online tv au tiktokers wenye followers wengi tupo Tayari kushirikiana nao.
 
Labda mahakamani mnapoteza mda.

Mngeanza na press conference ya msisitizo kwenye media then video clip mshare tiktok .

Kichwa cha habari kiwe : CRDB wametutapeli.

Muhimu muwe na ushahidi wa kutosha. CRDB watawatafuta wenyewe

Ubwela ubwela!!!
Tupo tayari kushirikiana na yeyote atakaetusapoti kwa namna yoyote katika kutekeleza mawazo mazuri ya namna hii , kwa sababu media hazitupi ushirikiano pamoja na kutuma SHAHIDI na wengine wanataka pesa , Kama Kuna yeyote anaeguswa na yupo tayari kutuunganisha na online tv au tiktokers wenye followers wengi tupo Tayari kushirikiana nao.
 
Kwa wana sheria kumeshindikana vipi, maana mtu ukiwa na mgogoro unahaki ya kwenda mahakamani kupata haki yako, tafuta wanasheria wazuri. Pia unaleta malalamiko yako kwa watanzania kwa kutumia lugha wasiyoifahamu vizuri , ngumu sana kufikia lengo
Kaka nashukuru kwa ushauri wako, LAKINI PIA soma vizuri mtiririko wote , kwa sababu mahakamani pia tulishafika na KESI ikaendeshwa katika mazingira ya upendeleo na ndio kilicho tufanya tuende BANK OF TANZANIA ambao wao pia wameikuta CRDB BANK PLC na Makosa na kuiamrisha kulipa , kwa sababu ya hukumu kutokua wazi kisheria tunakata rufaa BOT Kisha wanatakiwa watujibu ndani ya siku 21 ambazo Hadi sasa ni siku ya 80 wamekaa kimya kinyume na Sheria na ndio maana tunapaza sauti ili tujibiwe rufaa yetu kutokana na malalamiko yetu kwa sababu Hadi sasa Bank of Tanzania INATENDA kinyume na Sheria na popote Sheria inapopindishwa tambua Kuna UKIUKWAJI MKUBWA wa utawala bora. wa TANZANIA kuliko kutafuta Cha kukosoa ,napokea ushauri lakini pia tufocus kwenye tatizo na kusaidiana katika kutafuta HAKI.
 
Back
Top Bottom