Mme wa mtu jana kayatimba milioni 5 zamtoka kizembe

Mme wa mtu jana kayatimba milioni 5 zamtoka kizembe

Haiondoi uzito wa kesi. Sio lazima ufanyiwe uhalifu kwenu. Wala sio lazima watu washuhudie ndio upate haki yako. Wapelelez ni kazi yako kuthibitisha hili
Kwa uzembe wa mapolisi wetu hum.
 
Huo ni utapeli, unyang'anyi na ujambazi na uhuni kama uhuni mwingine. Ugumu wa maisha usikufanye uwatumie wenzio kama ngazi, matokeo yake wakirogwa ama jamaa akaamua kuwafanyizia wataanza kulaumu. Sasa hata ukienda kisheria hapo kuna kosa gani?! Ni sheria gani inayowaruhusu kuchukua pesa kwa nguvu kwa mtu anaetembea na Dada yao wa miaka 27?! Aiseeh watu wamekua na roho ngumu sana sasa hivi
 
Hakuna Cha kesi hapo Tanzania kuna haki?? Hapo ni jino kwa jino tu nawewe unafanya umafia tu unamteka binti alafu unawaita hao ndugu zake unapiga visu vya shingo tu unapita hapo wami unawarushia mamba wamekondeana majini
 
Kesi nyeupe sana hiyo kifupi hakuna kaka wale Keke Hilo ni kundi la wahuni na huyo mwanamke ni part ya Hilo kundi
Uamuzi ni wake awapoteze kisheria au awapoteze kimazingara
 
hilo ni Tatizo la kuishi eneo lililojaa maskini wengi.

Pili kama wewe unapenda kubadili wanawake, usioe kabisa kwa ndoa.

Ili ubaki na single status muda wote, jamaa angekuwa hajaoa hao makaka wasingeweza kumfanya chochote
Naunga mkono hoja
 
Jana nilirudi mapema kutoka mishe mida ya saa 12 nikajimwagia maji nikaingia mtandaoni kuperuzi kidogo mpaka mida ya saa moja nikaenda kusali nikarudi nikakaa sebuleni kucheki move hapo imesha gonga saa 2 usiku.

Sasa kipindi naendelea kucheki move nikasikia kama zogo nyuma ya nyumba yangu nikapuuza nikajua ni watu wana pita,lakini kadiri muda ulivyo kuwa unasongambele zogo linaongezeka nikaona ngoja nitoke nje nione ni akina nani hao wanao fanya zogo karibu na nyumba yangu niwaletee noma.

Nimetoka nje nakuta gari aina ya subaru foresta imepaki pale,naona kuna jamaa mmoja nina mjua ni ajent mkubwa wa miamala ya kifedha mfano mpesa, nmb,crdb ila sijuagi anaishi sehemu gani bali mamjua kwa sababu ya kazi yake na hiyo gari ilikuwa ni ya kwake na ni mtu mzima kwa kumkadiria hapungui kwenye miaka 47 kupanda.

Pembeni namuona binti ambaye naye namjua ni karani kwenye shule moja ya kanisa na tunaishi ni naye kwenye mtaa mmoja na ni binti mkubwa tu ambaye hapungui kwenye miaka 27 ,pia na waona wanaume kama watatu wameshikilia mapanga ninawajua ni kaka zake na yule binti na pia kulikuwa na watu wengine wengi nadhani nao walikuja kuwa mashuhuda kama mimi.

Sasa kilicho kuwa kina endelea ni kaka zake na huyo binti wanadai kuwa huyo mshikaji ambaye ni wakala,eti anarubuni mdogo wao wa kike mpaka huyo binti amekuwa akikataa wachumba kwa sababu ya huyo mwanaume hali yakuwa yeye ameoa na ana mke.

Na wakawa wanadai eti atoe milioni kumi kama fidia ya kumpotezea mdogo wao muda tofauti na hapo watamchoma moto na gari lake,na mbaya zaidi watu wakawa wana zidi kujaa na wengine wakaanza kushabikia eti azitoe ili wakomeshe tabia za wazee kuchezea mabinti za watu,kiufupi yule wakala hakuwa na mtu upande wake.

Yule wakala akajitetea akisema jamani mm sina hela hapa ,kaka mmoja wa binti akasema usitufanye wajinga hela unazo kwenye gari toa hela tofauti na hapo tunakuchoma moto na gari lako hili unalo tumia kurubuni mabinti za watu.

Kaka mmoja kati yao akasema huyu mzee tukiendelea kutumia maneno ataona hatuko siliasi akamfuata yule jamaa aisee alimpiga bapa la panga yule jamaa nikaona anaweweseka na kuanguka chini ndo wakamzunguka wakaanza kumpiga mabapa ya napanga kiasi mengine yakawa yana mpalaza mpaka anatoa damu wakati hayo yakiendelea kufanyika balozi wa mtaa yupo anabungaa macho tu.

Dah yule mzee alipo ona cha kufia nini akaamue akubali tu kuwa kwenye gari ana milioni 5 lakini sio za kwake bali amezikopa sehemu kwa ajili ya kufanya mzunguko wa miamala wakasema sisi hilo hatulijui sisi tunacho kitaka ni pesa.

Dah huwezi amini yule mzee akaingia kwenye gari akatoa bahasha yenye maburungutu yenye noti za 10,000 matano akampa mmoja wapo wa hao makaka aisee niliumia utadhani hizo hela ni za kwangu.

Lakini pamoja na kupewa hizo hela wakawa wanangangania kuwa bado pesa zipo kwenye gari awape, mzee akajitetea kuwa jamani mm pesa sina labda kama mna akaunti niwatumie basi kwenye akaunt zenu jamaa wakakataa sijui hapo walihofia nini.

Sasa wakasemaje eti wavunje vunje vioo vya gari ili kufidia hiyo milioni 5 iliyo baki aisee hapo nikaingilia kati nikawaambia aisee mm sihitaji mfanye huu uharifu karibu na nyumba yangu mtaniletea matatizo kama mnataka kufanya hivyo nendeni sehemu nyingine,na nikamuambia balozi kuwa kitu kibaya kikija kufanyika kwenye nyumba yangu ww ndo utaubeba huu msala.

Baada ya mm kusema hivyo balozi akawasihi wale kaka zake na yule binti kuwa imetosha kwa hiyo milioni 5 iliyo mtoka atakuwa kajifunza basi washikaji wakapunguza mkali wakasema tumekusamehe kwa sababu tunamuheshimu balozi na ole wako tukuone hata unawasiliana na mndogo wetu tutakupeleka kaburini.

Basi zogo likaisha na watu wakatawanyika lakini yule mshikaji aliye tapeliwa akawa amesimama kama kapingwa na butwaa fulani hivi sasa tulikuwa tumebaki kama watu watatu tukawa tuna muhoji,akawa ana tuambia kuwa anahisi wenda huu ulikuwa ni mchongo kati ya binti na kaka zake kwa sababu binti alimpigia simu mida na saa 11 jioni kuwa wakutane baa fulani amtoe aut kitu ambacho alikuwa hajawahi kufanya miaka 3 ya mahusiano yao.

Baada ya kunywa na kumaliza walienda gest baada ya kutoka gest yule binti akamuambia yule mshikaji kuwa ampe lift ampeleke nyumbani na binti ndo alikuwa muendesha gari na hizo hela binti aliziona.

Na ni kweli kabisa maana kipindi hili zigo linaendelea binti alikuwa normal hakuonekana kupata taharuki juu ya kile kilicho kuwa kinaendelea ,na mbaya zaidi familia yao ina historia ya umafia maana baba yao alisha fungwa jera kwa kesi ya ujambazi kipindi cha jiwe.

Ila jamaa kasema hawajamaliza labda binti ahame mji tofauti na hatomuacha salama.
Kusema ukweli mm siungi mkono uzinzi lakini alicho fanyiwa huyu mzee kimeniumiza maana sikuona kosa lake kabisa.
Kwaiyo wenzenu tunavyotembeaga na mashine kiunoni mnatuonaga wajinga?
 
Back
Top Bottom