Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,092
- 34,903
Sitaki kuamini sababu damu ya hedhi ni sumu mbya mno,tone moja tu linaondoa uhai wa mtu
​
‘ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni'. Usemi huu umethibitika hivi karibuni baada ya mlokole mmoja, Ruth Mwakalinga, mkazi wa Matejo, Arusha kumnywesha damu ya hedhi mwanaye, Easter Deodat.
Akizungumza na Risasi Jumamosi jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Easter alisema kuwa, wazazi wake walimfanyia kitendo hicho kwa tamaa ya kumiliki mali.
"Baba na mama waliamua kunifanyia hivyo kwa lengo la kunipumbaza akili ili niwe ndondocha na wao wawe matajiri," alisema.
Easter alisema kuwa, siku ya tukio alitoka ndani kwa lengo la kutupa uchafu baada ya kupata siku zake (hedhi) lakini alistaajabu mama yake huyo wa kambo alipomfuata na kumzuia ili arudi ndani.
"Nilipoingia ndani aliniuliza nimebeba nini mkononi, nikamwambia sina kitu, cha kushangaza aliniambia niuchukue uchafu huo kisha niikamulie damu hiyo kwenye kikombe alichonipa," alisema Easter huku machozi yakimtoka.
Msichana huyo aliendelea kueleza kuwa, baada ya kuikamulia damu kwenye kikombe, aliambiwa aendelee na kazi zake. Kesho yake asubuhi aliitwa chumbani kwa mama yake na kulazimishwa kuinywa damu hiyo.
Baada ya kuinywa alipoteza fahamu na alipozinduka alijiona akiwa tofauti na siku nyingine. Tangu siku hiyo alikuwa anatokwa na damu kila sehemu yenye uwazi.
Mkasa kamili wa kisa hicho utausoma ambapo utaona jinsi Easter alivyonusurika kupelekwa mochwari baada ya kupoteza fahamu kwa siku nne mfululizo.
Pia utaona ulokole wa mama yake aliyempaka mafuta sehemu za siri akidai ni ya upako baada ya kupewa maagizo na mchunguji wake wa kanisa moja huko Arusha.
Hizi story huwa ni za kutunga ajili ya kutumika katika ushuhuda.ni marketing strategy ya wachungaji kuvuta wateja.
Kama alinyweshwa damu ya hedhi akiwa mbinti mwishoni anataja mmewe.lini kaolewa hapo?
MLOKOLE AMNYWESHA DAMU YA HEDHI MWANAYE-4...
ILIPOISHIA
Kitendo cha kukiri huko kukawa salama kwake na mara alizinduka baada ya siku 4 na kila aliyekuwa kwenye wadi hiyo walikimbia wakidhani ni mzimu.
Easter alisema mama yake alimchukua na kumrejesha nyumbani akiwa katika hali nzuri kidogo lakini kila alipopata hasira, damu ilikuwa ikimtoka.
Mwishoni mwa mwezi uliopita, Easter aliamua kwenda kwa Mchungaji Mstaafu Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambikile Masapile ‘Babu' kwa ajili ya kupata kikombe.
Alisema, alifanikiwa kupata kikombe hicho na kujiona ana hali nzuri. Akiwa njiani kurejea Dar, alianza kujisikia kichefuchefu na kisha kutapika damu.
Easter alisema baada ya kufika nyumbani kwao, alikaa kama wiki moja hali ikawa mbaya na alianza tena kutokwa damu mwili mzima kisha akapoteza fahamu.
SASA ENDELEA...
Baada ya kupoteza fahamu, mume wangu aliomba msaada kwa majirani na ndipo walipoamua kupiga simu kwa Askofu na Nabii, Nicolaus Sugeye wa Huduma ya Neno la Upatanisho iliyopo Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maombi.
Nikiwa katika hali ya kupoteza fahamu , jirani yangu mmoja alichukua simu yake na kuiweka sikuoni mwangu. Kwa mbali nilisikia sauti ya maombi sikujua ni yanani, kumbi wakati huyo mtumishi wa Mungu Suguye alikuwa anaomba kwa njia ya simu hiyo. Ghafla nilizinduka na damu iliyokuwa inatoka mwilini iliacha.
Baada ya kunyanyuka mume wangu na rafiki yake walinichukua na kunipeleka kwa Askofu na Nabii Suguye kwa ajili ya kuombewa na katika hali ambayo siwezi kuielezea mpaka sasa, baada ya kukutana na mtumishi huyo wa Mungu na kuombewa hakika nilipona kabisa.
Tatizo hilo lililokuwa linanisumbua kwa muda mrefu nashangaa lilipona siku moja mpaka nataoa ushuhuda huu mimi ni mzima wa afya.
Lakini kabla ya kupata uponyaji huu, nilipelekwa Loliondo kwa Babu kwa ajili ya kunywa dawa inayosadikika inaponya magonjwa sugu.
Nilifanikiwa kunywa dawa hiyo nikiwa na hali mbaya huku mume wangu akifikiri kwamba sitarudi salama nyumbani.Daada ya kupata kikombe hicho, hali yangu ilionekana kuimarika nikawa natembea kama kawaida huku mume wangu akionekana mwenye furaha kubwa.
Safari ya kurudi Dar es Salaam ilianza, lakini nikiwa njiani ghafla nilianza kusikia kichefu chefu kisha nikaanza kutapika damu. Kila aliyekuwa akiniangalia alitokwa machozi kutokana na hali yangu kuwa mbaya.
Kila mmoja alisema lake huku mume wangu akionekana kukata tamaa na hali hiyo kwani ilikuwa haipiti wiki moja lazima hali hiyo initokee.
Namshukuru Mungu mume wangu alionesha upendo wa dhati kwani alikuwa nami bega kwa bega. Kwa kifupi nasema kwamba uponyaji wangu ulipatikana mara baada ya kupata maombi kutoka kwa mtumishi wa Mungu Askofu na Nabii Nicolaus Suguye.
Kikombe cha Babu wa Loliondo hakikunisaidia kwani nilikuwa nimefungwa na nguvu za giza kutoka kwa wazazi wangu. Msomaji huu ni mkasa wa kweli.Ester aliomba nitoe namba yake ili mwenye mashaka azungumuze naye. Namba yake ni 0713618820. ''MWISHO''
Unahitaji kuwa mjinga hasa kuamini story za namna hii. Kuna sehemu hapo inasem 'dakatri akaniambia utakaa katika hali hii kwa mwezi mzima' hivi dakatari anawezaje kujua damu itaacha kutoka kwa mwezi mzima? Kwanza na wewe MziziMkavu, ilikuwaje mpaka mwanaume ukaanza kusoma Risasi? Habari kama hizi huwezi kuzikuta kwenye magazeti yenye akili zake.Hizi story huwa ni za kutunga ajili ya kutumika katika ushuhuda.ni marketing strategy ya wachungaji kuvuta wateja. Kama alinyweshwa damu ya hedhi akiwa mbinti mwishoni anataja mmewe.lini kaolewa hapo?
Bibie Penelope History ya ukweli kama unataka kuamini jaribu kupiga simu hii namba muulize huyo bibie (Ester aliomba nitoe namba yake ili mwenye mashaka azungumuze naye. Namba yake ni 0713618820)Kama hi stori ni ya ukweli,basi huyu mama hakua mlokole sema alitumia ulokuole kuficha makucha yake na mambo aliyokua anayafanya
Hizi story huwa ni za
kutunga ajili ya kutumika katika ushuhuda.ni marketing strategy ya
wachungaji kuvuta wateja.
Kama alinyweshwa damu ya hedhi akiwa mbinti mwishoni anataja mmewe.lini
kaolewa hapo?