SoC02 Mlo kamili kwa afya bora

Stories of Change - 2022 Competition

bruno malago

New Member
Aug 16, 2022
4
3
MLO KAMILI KWA AFYA BORA.

Mlo kamili, ni mlo ulio na aina ya makundi ya chakula tofauti tofauti, vyenye virutubishi bola, ambavyo hupatia mwili afya iliyo bora. Mlo kamili unaudwa na makundi ya chakula mengi na tofauti kulingana na kiwango cha virutubishi Kwa kila kundi la chakula lilivyo navyo.

Makundi ya chakula ambayo yanakamilisha mlo bora ni kama yafuatayo fat( ni kundi lenye vyakula ambayo asili yake ni mafuta; mfano mafuta ya alizeti, mafuta ya samaki, karanga), protein (ni kundi lenye vyakula vyenye protini Kwa wingi; mfano nyama, maziwa, mayai, na samaki), carbohydrates (ni kundi la tatu lenye vyakula vyenye asili ya mazao ya nafaka; mfano ngano, mchele, ulezi, na mahindi).

Vitamin na madini (ni kundi la nne lenye vyakula vyenye asili ya mboga mboga na matunda; mfano mchicha, karoti, chainise, sukuma wiki, tembele, ndizi, papai, chungwa,tikiti maji na parachichi). Haya makundi manne ndiyo yanayo kamilisha mlo kamili na kwenye jamii yetu inatakiwa yazingatiwe ili kuweza kuwa na afya iliyo bora.

Kiwango cha makundi ya chakula ambayo mtu anatakiwa kutumia ili akamilishe mlo bora na afya bora ni kama ifuatavyo; vitamin na matunda 40% , protein 25%, carbohydrates 25% na fat 10%.

Mlo kamili ili uweze kuwa na faida katika mwili, inatakiwa kufuata njia zifuatazo;
1. Kula vitamin na matunda Kwa wingi
2. Kula Kwa kiasi vyakula vyenye asili ya mafuta
3. Kula protein Kwa wingi
4. Usitumie chumvi nyingi wakati wa Kula
5. Kunywa maji mengi kila siku.

Faida ya kuzingatia mlo kamili ni kama zifuatazo;

1. Mlo kamili husaidia kujenga mwili
2. Mlo kamili huupa mwili nguvu zidi ya magojwa
3. Mlo kamili huupa mwili ngozi nzuri na yenye afya
4. Mlo kamili husaidia kukua Kwa haraka.
 
Back
Top Bottom