Mlitudharau na kutucheka leo mnatuona mashujaa!!

Mlitudharau na kutucheka leo mnatuona mashujaa!!

Chinga One

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
11,493
Reaction score
12,453
Mlituona maskini,hatuja soma,tumelala,hatuna uelewa,tulipokuja dar kutafuta unafuu wa maisha mkatuita 'wamanchinga' eti leo mnatuona mashujaa n unafiki.

tulisafir kwa wik 2 kuja dar kwenye barabara ya tope kwa miaka 50 na hamkutujari wala kututetea,tulikaa gizani kwa mda mrefu kwa kukosa umeme wa uhakika,eti leo mnatuambia 'tutaishi kama ulaya' kisa gas na mnataka kuipeleka dar! ni kuto kututhamini.

mlipo amishiwa mtwara kikazi mligoma kuja mkadiriki hata kuacha kazi kisa mtwara hakustahili kuishi watu,iweje leo eti 'wana mtwara tuko pamoja mpaka kieleweke' ni unafiki.

mliita mtwara ngome yenu ya kupatia kura,leo tunadai haki yetu mnatuona wahaini,chura,mambumbu, mnatupiga mabomu na kutuua kisa mshakula 10% ni dhuluma na unyanyasaji.

wakati nyie mlikua mnakunywa soda kwa sh 150,sis mtwara sh 600,huko kwenu kilo ya nyama ilikua sh 1000 huku mt sh 3000,hapo bado unga,mchele n.k eti leo tumepewa neema mnadai mtwara wabinafsi gas ya watz wote,basi njoni mtwara tuifaidi sote ikiwa huku huku.

GAS MTWARA.COM
 
Huu uchungu ni juu ya udhalimu wa serikali ya ccm kwa watu wa mtwara na lindi, hapa wakubwa kuna ukweli mtupu juu ya haya maelezo ya huyu bwana juu ya gesi na madhila wanayopata watu wa kusini baada ya mtafaruku mkubwa unaoendelea kule mtwara, ila serikali kama bado wana utu angalau kidogo basi wasikilize hawa watu maana ni kweli madai yao yana logic.
UKWELI NI KWAMBA TUMEFIKA HAPA KWA SABABU YA UDHALIMU WA SERIKALI YA CHAMA CHA CCM
wana Mtwara naombeni sana muwe kitu kimoja kwa kipindi hiki kigumu kwa mustakabali wenu ila naombeni sana tulinde umoja wetu wa kitaifa

Mlituona maskini,hatuja soma,tumelala,hatuna uelewa,tulipokuja dar kutafuta unafuu wa maisha mkatuita 'wamanchinga' eti leo mnatuona mashujaa n unafiki.

tulisafir kwa wik 2 kuja dar kwenye barabara ya tope kwa miaka 50 na hamkutujari wala kututetea,tulikaa gizani kwa mda mrefu kwa kukosa umeme wa uhakika,eti leo mnatuambia 'tutaishi kama ulaya' kisa gas na mnataka kuipeleka dar! ni kuto kututhamini.

mlipo amishiwa mtwara kikazi mligoma kuja mkadiriki hata kuacha kazi kisa mtwara hakustahili kuishi watu,iweje leo eti 'wana mtwara tuko pamoja mpaka kieleweke' ni unafiki.

mliita mtwara ngome yenu ya kupatia kura,leo tunadai haki yetu mnatuona wahaini,chura,mambumbu, mnatupiga mabomu na kutuua kisa mshakula 10% ni dhuluma na unyanyasaji.

wakati nyie mlikua mnakunywa soda kwa sh 150,sis mtwara sh 600,huko kwenu kilo ya nyama ilikua sh 1000 huku mt sh 3000,hapo bado unga,mchele n.k eti leo tumepewa neema mnadai mtwara wabinafsi gas ya watz wote,basi njoni mtwara tuifaidi sote ikiwa huku huku.

GAS MTWARA.COM
 
Umenena yaliyomema, na umeongea kwa hisia kali. Na kwa kuongezea hapo, wamesahau hawa watu, tulikuwa tunashindwa kurudi likizo nyumbani kwa sababu siku za likizo zote zilikuwa zinaishia njiani. Keki yao walikuwa wanakula wenyewe, hii yetu tunataka kuhakikisha usalama wake. Hatutakula yote lakini wenyewe tupewe KIPANDE KIKUBWA. AMEEEEEEN
 
Adui yenu na. 1. ni CCM, korosho wanawaibia kupitia mfumo wa stakabadshi ghalani na gesi wanataka kwenda nayo nzimanzima.
Niweke kumbukumbu sahihi ambayo watu wengi ikiwemo vyombo vya habari aidha kwa kujua au kutokujua wanapotosha.

Si kweli kwamba Mtwara hawataki gesi itoke, shida yao inatoka toka je? Serikali nendeni mjadiliane au wekeni mkataba wazi ili wabunge wote ikiwemo hao wa CCM toka huko Mtwara na Lindi wakasaidie kuelimisha umma, sasa kama hata wabunge hawajui kilichoko kwenye mkataba si ndo maana kila mtu anasema la kwake?
 
ina logic sana hii post.....I think viongozi inabidi waisome hii na kuitafakari......if we are not carefully southern sudan problem will be on our side now.....it is something very logic and true
 
The world population is growing at venom rate,
Resources are shrinking at uncontrollable rate, nothing is ever enough for a man...!
It is to my attention hata Chinga wameamka? Jomba nchumali uchimumunye wala uchiteme nchale inakuhusuuuuu!
 
HAAA FACT sasa ndo wanatuona wa Mtwara Juuuuu?nakumbuka nilishaenda Mtwara mwaka 96...tulibeba na maji na vyakula..vya akiba njiani... maana hakukuwa na hata kihoteli njiani ..kufika rufiji..tukahitajika kuspend the night kisa muda wa kivuko ushapita ..mabasi yanaoenda ni yale yaliyochooka likikugusa tu Tetenus
 
nafikiri serikali ikae chini na watu wenye busara waupate ukweli,maisha siyo dar peke yake,naamini kwa upumbavu wa chama tawala wangeweza kusema mlima Kilimanjaro uamie dar kwani ndo panafikika kwa urahisi,mambo ya gesi yafanyikie mtwara ili nao wapate maendeleo.serikali inakera kwelikweli.
 
Wana JF naomba nijibiwe hili Swali kwa umakini na kuendelea kuilinda haka kaamani kalichobakia kuelekea Saa ya ukombozi.Nimekumbuka Kile kitabu cha things fall apart cha Marehemu Chinuo Achebe
 
Kwa miaka nenda rudi, Mtwara mmekuwa mkinufaika na rasilimali za Alimasi ya Mwadui, (Kumbuka Alimasi huchimbwa Mwadui, na TAN-CUT ALMASI iko Iringa), Mmenufaika na dhahabu toka Buzwagi, Mmenufaika na fedha za utalii toka Serengeti, na kila Mkoa ulipopata gawio la Taifa, Mkoa haukukataa kuzipokea kwa kuwa zinatoka nje ya Mkoa. Leo Mtwara kuna gesi, basi mnaona gesi ni yenu, wakati mkinufaika na vya wenzenu, mliona vitamu. Poleni sana, GESI ITATOKA. iwe kwa kheri au kwa shari. Na ninyi onjeni mrahaba wa 0.03%. KIDUMU CHAMA.
 
hivi hakuna viongozi wanaosoma haya mabandiko!na kama wapo mbona wanakuwa wagumu kuelewa?
 
Jamani basi kila mtu arudi kwao wa kanda ya kusini warudi kusini wa kanda ya kaskazi warudi kwao wa mashariki na magharibi nao warudi kwao Dar ni ya Wazaramo. I mean kila mtu arudi kwenye mkoa wake? period. Wachaga TURUDI KWETU KILIMANJARO MAANA NDIO TUMEJAZANA SANA DSM tukijifanya ndio kwetu halafu ikifika desemba tunaenda likizo kilimanjaro. Huenda sisi ndo chanzo cha vurugu za mtwara. So kila Mtu arudi kwenye mkoa wake. Wenye asili ya dar wabaki dar nambari moja ni Wazaramo. wengine wote wakuja? na wapemba warudi kwao pemba!
 
Pole sana mleta thread, lkn tambua kuwa mikata ishasainiwa na 10% ishaliwa! Mnatarajia nini?
 
Wakiweza tu nayo kui-pack kwenye makontena, tutaisahau....
 
Uzi mzuri sana kama watu wangekuwa wanasoma humu masuruhisho yangekuwa yanapatikana mara moja, wanachodai wana Mtwara si kikubwa sana kama serikali itagundua lakini wao wanangalia matokeo ya fujo (ni vizuri kwa usalama) lakini pia yatokano na fujo ni ya muhimu pia maana wakati mwingine ukiyajua inakuwezesha hata kupata namna ya kuwajibu wananchi na mwisho wa siku mambo yanaisha
 
Back
Top Bottom