Mlipuko wa ugonjwa wa uti wa mgongo waua 120 DRC

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Mlipuko wa ugonjwa wa uti wa mgongo au meningitis umetangazwa kaskazini- mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Mpaka sasa watu zaidi ya 120 wamekufa kutokana na ugonjwa huo.

Mgonjwa wa kwanza nchini DRC aliripotiwa Julai.

Zaidi ya watu 100 wamepata tiba wakiwa nyumbani au vituo vya afya.

Mlipuko huo umekuwa mgumu kukabiliana nao kwa kuwa jamii inauhusisha na uchawi, shirika la afya duniani (WHO) limeiambia BBC.

Sampuli zilizotumwa Ufaransa zimebaini kuwa bakteria wanaohusika na mlipuko huo wanaweza kusababisha janga kubwa.

Watu wengi wamekufa na jamii inapaswa kulaumiwa kwa kushindwa kuwajibika.

Badala ya kutafuta tiba, baadhi ya watu wamekuwa wakitoka sehemu moja kwenda nyingine wakiwa na matumaini kuwa ugonjwa huo hautawafuata.

Serikali ya DRC na WHO wametuma vikosi vya watumishi wa afya kaskazini mashariki mwa jimbo la Tshopo ili kukabiliana na hali hiyo.

Baadhi yao hawana uwezo na wako katika hatari kwa milipuko ya mara kwa mara haswa wakati wa kiangazi - kutoka Januari hadi Julai.

Meningitis, ni ugonjwa ambao unaweza kusababisha kifo, unaambukiza kutoka kwa mtu mwenye maambukizi kupitia matone, akipumua au akikohoa.
 
Daah hii nchi sijui ni lini tu itakuja kua salama ikatulia kabisa bila vita na maradhi makubwa makubwa ya mlipuko, MUNGU azidi kuwalinda wa Congo.
 
Mlipuko wa ugonjwa wa uti wa mgongo au meningitis umetangazwa kaskazini- mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Mpaka sasa watu zaidi ya 120 wamekufa kutokana na ugonjwa huo.

Mgonjwa wa kwanza nchini DRC aliripotiwa Julai.

Zaidi ya watu 100 wamepata tiba wakiwa nyumbani au vituo vya afya.

Mlipuko huo umekuwa mgumu kukabiliana nao kwa kuwa jamii inauhusisha na uchawi, shirika la afya duniani (WHO) limeiambia BBC.

Sampuli zilizotumwa Ufaransa zimebaini kuwa bakteria wanaohusika na mlipuko huo wanaweza kusababisha janga kubwa.

Watu wengi wamekufa na jamii inapaswa kulaumiwa kwa kushindwa kuwajibika.

Badala ya kutafuta tiba, baadhi ya watu wamekuwa wakitoka sehemu moja kwenda nyingine wakiwa na matumaini kuwa ugonjwa huo hautawafuata.

Serikali ya DRC na WHO wametuma vikosi vya watumishi wa afya kaskazini mashariki mwa jimbo la Tshopo ili kukabiliana na hali hiyo.

Baadhi yao hawana uwezo na wako katika hatari kwa milipuko ya mara kwa mara haswa wakati wa kiangazi - kutoka Januari hadi Julai.

Meningitis, ni ugonjwa ambao unaweza kusababisha kifo, unaambukiza kutoka kwa mtu mwenye maambukizi kupitia matone, akipumua au akikohoa.
Majanga yote ni yao
 
Makoloni ya WAFARANSA NA TABU WAPITIAZO....

Angalia "FRANCOPHONE" zote utamaizi kitu.....

Ni hivi.....

Kule Lancaster walipokuwa wanajadili makoloni ya afrika,wafaransa walitoa masharti juu ya UHURU WA HIZO NCHI.....

Mosi,uwekezaji wa raslimali zote baada ya uhuru(katika makoloni) wasipewe "WAZUNGU WENGINE" isipokuwa wao....

"Raia" wa makoloni hayo Watakuwa wanapewa "VISA" ya kuingia UFARANSA vile wajisikiavyo......

Hapa wala hakuna la kufurahisha na kupigia makofi kwani "RAIA HAO WAKO WALIOKO HUKO UFARANSA"

Swali je wanafanya SHUGHULI GANI ZA KIHESHIMA KAMA WAFARANSA WENYEWE?!!!

Jibu......

Ni tofauti na "wahindi ,wapakistani" walioko UINGEREZA(koloni lao)....wao wameweza kupata elimu kubwa ,kuwa wafanyabiashara wakubwa,wanasayansi na madaktari wa kupigiwa mfano...kubwa zaidi kuwa WANASIASA NA VIONGOZI WAKUBWA KATIKA SERIKALI YA UK(mfano uwaziri na mameya...London)....Mathalani WAKONGOMANI walioko UFARANSA wala hawajafika "levels hizo".....

TANBIHI:-

Jiulize ni kwanini katika bara la afrika ni nchi mbili tu ambazo hazijawahi kufanyika MAPINDUZI(Coup d'etat)?!!

1)Afrika ya kusini

2)Senegal

Senegal nayo ni "FRANCOPHONE" ,je sababu zipi zimewatofautisha na wenzao?!!

THIS IS YOUR HOMEWORK.....

#SiempreTanzania
#NakupendaTanzania
#NchiKwanzaKablaYaUhaiWangu

ADUMU MILELE CHIFU MKUU HANGAYA🙏👊💪
 
Sasa wewe ukiambiwa ule panya utakula? 😅😅😅 au umetafsiri kwa akili za weekend?
🤣🤣Mkuu Panya wanaliwa sana na ndugu zetu "wamawia" na huko "far east"...je umeshawahi kusikia kuna milipuko ya magonjwa kama hapo DRC?!!!
 
DRC again? Tatizo hawa wanakula hata visivyoliwa, wanakosaje sasa hii milipuko
DRC wanakula sana nyama ya Sokwe na Nyani, yaani kwao ndiyo kama mbuzi, ngombe au kondoo.. Ukiwa DRC kua makini sana na ulaji wa nyama zinazouzwa na wazawa..
 
Vip china na asia kwa ujumla wake,akina nyoka,wou,nyau na vinginevyo
 
Makoloni ya WAFARANSA NA TABU WAPITIAZO....

Angalia "FRANCOPHONE" zote utamaizi kitu.....

Ni hivi.....

Kule Lancaster walipokuwa wanajadili makoloni ya afrika,wafaransa walitoa masharti juu ya UHURU WA HIZO NCHI.....

Mosi,uwekezaji wa raslimali zote baada ya uhuru(katika makoloni) wasipewe "WAZUNGU WENGINE" isipokuwa wao....

"Raia" wa makoloni hayo Watakuwa wanapewa "VISA" ya kuingia UFARANSA vile wajisikiavyo......

Hapa wala hakuna la kufurahisha na kupigia makofi kwani "RAIA HAO WAKO WALIOKO HUKO UFARANSA"

Swali je wanafanya SHUGHULI GANI ZA KIHESHIMA KAMA WAFARANSA WENYEWE?!!!

Jibu......

Ni tofauti na "wahindi ,wapakistani" walioko UINGEREZA(koloni lao)....wao wameweza kupata elimu kubwa ,kuwa wafanyabiashara wakubwa,wanasayansi na madaktari wa kupigiwa mfano...kubwa zaidi kuwa WANASIASA NA VIONGOZI WAKUBWA KATIKA SERIKALI YA UK(mfano uwaziri na mameya...London)....Mathalani WAKONGOMANI walioko UFARANSA wala hawajafika "levels hizo".....

TANBIHI:-

Jiulize ni kwanini katika bara la afrika ni nchi mbili tu ambazo hazijawahi kufanyika MAPINDUZI(Coup d'etat)?!!

1)Afrika ya kusini

2)Senegal

Senegal nayo ni "FRANCOPHONE" ,je sababu zipi zimewatofautisha na wenzao?!!

THIS IS YOUR HOMEWORK.....

#SiempreTanzania
#NakupendaTanzania
#NchiKwanzaKablaYaUhaiWangu

ADUMU MILELE CHIFU MKUU HANGAYA🙏👊💪
Mmmh, kwa nini Hamza baada ya magaidi kudhibitiwa Kule mtwara /msumbijj akaenda kuua ubalozi wa ufaransa
 
Back
Top Bottom