Mlipuko wa bei Sukari kilo 3000, sembe kilo 2000

afsa

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
1,983
1,574
Wanabodi tuitendee haki nchi yetu na watanzania wenzetu wasio na uwezo wa kumudu gharama kubwa za vyakula hapa nchini kwa sababu ya uhaba wa chakula uliosababishwa na ukame.

Hapa kwetu kijijini tumelima zaidi ya majembe 3 kwa msumu huu bila mafanikio, yaani tulilima mara ya kwanza yakakauka, tukafyeka tukalima tena na tena lakini wapi.

Tumelima viazi lakini havijakomaa kwa sababu ya uhaba wa mvua. Sasa hapa kwetu kijijini debe la mahindi ni elfu 25000 tena yameongezwa maji kidogo ili yavimbe. Wananchi tunahangaika. Mazao yetu yameharibika, wengi hatuna uwezo wa kumudu gharama za chakula.

Serikali ilete chakula angalau tununue kwa bei nafuu. Hatutaki vya bure ila Wafanyabiashara wanapandisha bei kihorera serikali hii ipo kimya.
Wazee wamesikika wakiilaani serikali na CCM kwa sababu ya kuwatelekeza wafe na njaa wakati waliipigia kura.

Ni huku kwetu usukumani hali ni tete sana. Sijui hali ya sehemu zingine ikoje.
Twafaaaaaaaaaaaaaaa
 
Na bado...bajeti ikisomwa kodi za kujenga reli utageuka shetani kabla 2020
 
naamini ni kipindi cha mpito tu hiki hali itarudi kama zamani baada ya muda
NAICHUKIA CCM kuliko hata dawa ya mseto ila magu ana upeo fulani na nchi hii nimeona kitu kwake japo naye ana mapungufu mengi tu
ila naamini atatupigisha hatua fulani ya maendeleo
TUVUTE SUBIRA tusiwe mtaji wa wanasiasa
 
Serikali haizungumzii kabisa huu mfumuko wa bei za vyakula..

Wao reli ya umeme na mindege tu.
Sasa sisi watu wa huku Namanyele hizo reli za umeme na mindege sijui itatusaidia nini!!?

Eti serikali sikivu.
 
Acha nchi inyooshwe....

Si ndio kamsemo ketu

Kanyaga baba kanyagaaaaa

Ukiongezea na hizi punguza pubguza....burudaaaaaani kabisa
 
Wanabodi tuitendee haki nchi yetu na watanzania wenzetu wasio na uwezo wa kumudu gharama kubwa za vyakula hapa nchini kwa sababu ya uhaba wa chakula uliosababishwa na ukame.

Hapa kwetu kijijini tumelima zaidi ya majembe 3 kwa msumu huu bila mafanikio, yaani tulilima mara ya kwanza yakakauka, tukafyeka tukalima tena na tena lakini wapi.

Tumelima viazi lakini havijakomaa kwa sababu ya uhaba wa mvua. Sasa hapa kwetu kijijini debe la mahindi ni elfu 25000 tena yameongezwa maji kidogo ili yavimbe. Wananchi tunahangaika. Mazao yetu yameharibika, wengi hatuna uwezo wa kumudu gharama za chakula.

Serikali ilete chakula angalau tununue kwa bei nafuu. Hatutaki vya bure ila Wafanyabiashara wanapandisha bei kihorera serikali hii ipo kimya.
Wazee wamesikika wakiilaani serikali na CCM kwa sababu ya kuwatelekeza wafe na njaa wakati waliipigia kura.

Ni huku kwetu usukumani hali ni tete sana. Sijui hali ya sehemu zingine ikoje.
Twafaaaaaaaaaaaaaaa
huu undugu na Mungu tumeuanza lini? hebu tujiulize watu wanne tu wanalima miwa yaani kagera suger mtibwa kilombero tpc na wanalisha sukari nchi nzima, halafu wakulima mil 30 hawawezi kulima mahindi ya kutosha, huu ni ujinga wa hali ya juu, bora tuwapatie hawa jamaa wanne mashamba namtaji walime mahindi yakulisha nchi nzima kuliko kukaa kulaumiana na mungu kila mwaka.
 
Shida ni mvua zilizochelewa. Naamini mambo yatabadilika muda sio mrefu
tatizo ni kilimo kuachiwa watu masikini wanaokaa kulaumina na Mungu kila siku, tunapaswa kuwa na mashamba madogo yanayolimwa kitaalamu na kutoa tija, hebu ona Israel na Saud Arabia wanalima mashamba madogo kwa utaalamu na wanapata mazao ya kutosha. Kwanini tusiwapatie Kilombero suger na Mtibwa hekta milioni moja kila mmoja na mtaji wa tril mbili walime mahindi na mchele wakutosha kulisha watanzania na kuuza nje badala ya watu mil 30 kulima kwa jembe la mkono na kumtegemea Mungu kwa mvua.
 
Tatizo la mfumuko wa bei limesababishwa na Raisi wa awamu ya Tano yeye kwakauli yake bila kua na aibu na wala kubakiza maneno akiwa amedhamilia kuwaumiza watanzania aliwambia wakulima wajipangie bei ya vyakula kwa kumaanisha kua bei ya vyakula ipande akiamini anawasaidia wakulima kumbe anauwa. Huyu ndo raisi wetu hatakimuombea hakuna mabadiliko yaani yeye anaamini kila anachokifanya kipo sawa
 
tatizo ni kilimo kuachiwa watu masikini wanaokaa kulaumina na Mungu kila siku, tunapaswa kuwa na mashamba madogo yanayolimwa kitaalamu na kutoa tija, hebu ona Israel na Saud Arabia wanalima mashamba madogo kwa utaalamu na wanapata mazao ya kutosha. Kwanini tusiwapatie Kilombero suger na Mtibwa hekta milioni moja kila mmoja na mtaji wa tril mbili walime mahindi na mchele wakutosha kulisha watanzania na kuuza nje badala ya watu mil 30 kulima kwa jembe la mkono na kumtegemea Mungu kwa mvua.
Kwa bajeti za kilimo zinazotolewa na serikali za CCM, hali itaendelea hivyo hivyo.
 
naamini ni kipindi cha mpito tu hiki hali itarudi kama zamani baada ya muda
NAICHUKIA CCM kuliko hata dawa ya mseto ila magu ana upeo fulani na nchi hii nimeona kitu kwake japo naye ana mapungufu mengi tu
ila naamini atatupigisha hatua fulani ya maendeleo
TUVUTE SUBIRA tusiwe mtaji wa wanasiasa
Ni kweli tuvute subira mpaka kilo ifike elfu 6 halafu itashuka mpaka mia tano.
 
naamini ni kipindi cha mpito tu hiki hali itarudi kama zamani baada ya muda
NAICHUKIA CCM kuliko hata dawa ya mseto ila magu ana upeo fulani na nchi hii nimeona kitu kwake japo naye ana mapungufu mengi tu
ila naamini atatupigisha hatua fulani ya maendeleo
TUVUTE SUBIRA tusiwe mtaji wa wanasiasa
Sasa hizo hatua anawapigisha kina nani wakati watu wanakufa na njaa
 
Back
Top Bottom