Mlipuko tena Arusha, jeshi la Polisi watuhumiwa

hasason

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2012
Posts
1,648
Reaction score
1,542
[h=3]MLIPUKO TENA ARUSHA, JESHI LA POLISI WATUHUMIWA[/h]

Taarifa ambazo zimetufikia kupitia kituo cha WAPO Radio FM zinaeleza kwamba kuna bomu limelipuliwa kwenye kanisa katoliki la Mtakatifu Karoli, Ruanga huko USA River jijini Arusha, ambapo wanakwaya takriban 6 wamejeruhiwa.

Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo zimetufikia, zinaeleza kwamba watuhumiwa ni jeshi la Polisi, na kwamba walirusha kitu kinachosadikiwa kuwa bomu - lililojeruhi 6, ambapo 4 kati yao wameruhusiwa baada ya matibabu kwenye hospitali ya Mission na ya Wilaya ya Arumeru.

Majira ya saa sita na nusu, waumini walidai kuona gari la polisi likipita kwa kasi, na lilipowakaribia walistuka mlipuko ukiwarusha pembeni, ambapo walijikuta na majeraha na usoni, mapajani na maeneo mbalimbali ya mwili. Kisha baada ya hapo gari ilisogea mbele na kuanza kurusha mabomu kwa watu wowote iliokutana nao.

Hadi sasa inaelezwa kuwa uchunguzi umeshaanza kufanyika, huku Kamanda Liberatus Sabas akikataa kuzungumzia zaidi suala hilo. Alipotafutwa na WAPO Radio FM, hakueleza kwa kina, lakini akasema kuwa sio suala la kwaya kama ambavyo imeelezwa, bali ni wakinadada wawili na kwamba hawezi kuzungumza zaidi, bali kesho (Ijumaa) atatoa taarifa rasmi na iliyo kamili kwa vyombo vya habari.

Alipoulizwa kuwa kama ni kweli jeshi la Polisi linatuhumiwa kuhusika, alisema kuwa atazungumza kesho kuhusiana na tukio hilo. Tukio hili limetokea ikiwa ni siku mbili zimepita tokea kuapishwa kwa Inspekta Jenerali wa Polisi mpya, Ernest Mangu ambaye amechukua nafasi ya IJP Said Mwema aliyestaafu.

Source: Gospel Kitaa.
 
Ni kweli hata Mimi nilikuwepo na kushuhudia polisi wakirusha bomb maeneo ya raia waliotoka kanisani tena bila Fuji yeyote !
 
Mh.Nchimbi arudishe kazini kujibu hili kabla ya kutimuliwa tena
 
tukiambiwa na watu watatu zaidi itaondoa shaka. manake members wa jf walivyo wengi arusha mpaka sasa thread za bom hazijafurika!!!!!!
 
Kwa hiyo unataka kutuambia polisi wetu ni vichaa au?

Hapo gongo haijaruhusiwa mnapost vitu kama hivi ikiruhusiwa itakuwaje?
 
ni keeling hata Mimi nilikuwepo na kushuhudia polisi wakirusha bomb maeneo ya aria waliotoka kanisani tena bila Fuji yeyote !

inaonekana simu yako ilikuwa charge manake toka saa sita mpaka saa hizi ndo unajitokeza!!!
 
Wanamlenga nani hawa polisi and why always these happen in Arusha
 
Ukiangalia kwa undani sana kuna mapungufu katika habari hii,unakwenda kufanya ugaidi halafu unatumia vyombo vya usafiri vinavyokutambusha wewe ni nani),wakati kwa arusha kuna magari kibao ys kukodi au magari binafsi ya hao polisi,just thinking loud!
 
Plse, Don't tell us our police are eager to kill innocent citizens while robbers, gun murder and elephant killers are celebrating their archievement.
Wananchi tunachokozwa, Ama that's new "Operation TOKOMEZA"
 
Polisi wa jiji la Arusha ni majambazi wa kutupwa,hakuna kitu wanafanya zaidi ya kuwaza namna ya kuingiza pesa kwa namna yoyote ile,ni hatari sana kudeal na police wa jiji la Arusha hasahasa central ni msala wa hatari.
 
Ni kweli hata Mimi nilikuwepo na kushuhudia polisi wakirusha bomb maeneo ya raia waliotoka kanisani tena bila Fuji yeyote !

kwani waliomuua Kombe, waliowaua wachimba madini wa kule moro, na waliowaua wale vijana walevi Ar etc na wenzao ambao wanasubiri nafasi yao wamepona ?

We kawaambie wenzio waache jisafisha kipuuzi kwa kutaka jenga scene nyingine ya kumsingizia mwingine ili kuunganisha na mengine itawakost sana.

Wajifunze namna ya kuleta amani pengine raia watakuwa wamesahau horror..binadamu kaumbwa kuachana na hasira akipewa time.Lakini this way polisi wanazidi wakumbusha watu hadi uchaguzi watu waanze ahamasishana kuhusu hili..then ahsir ayao itakuwa ktk kura.
 
Ukiangalia kwa undani sana kuna mapungufu katika habari hii,unakwenda kufanya ugaidi halafu unatumia vyombo vya usafiri vinavyokutambusha wewe ni nani),wakati kwa arusha kuna magari kibao ys kukodi au magari binafsi ya hao polisi,just thinking loud!

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, E. Nchimbi aliliambia bunge katika kikao kilichopita kwamba serikali haina mpango wa kuunda Tume ya kuchunguza mabomu ya Arusha, Think aloud why? Je, serikali iko kwa ajili ya nani?....Hapa duniani mtakuwa wajanja lakini mbele za Mola ninyi ni wajinga tu.
 
ikiruhusiwa tutakuning'iniza kichwa chini miguu juu angalau zidondoke chenchi chenchi za rambirambi tuziwakilishe kwa muhusika.

hahaha Leo naona umeamka vibaya mkuu. hawa vijana wetu hawa tabu sana...
 
[h=3]MLIPUKO TENA ARUSHA, JESHI LA POLISI WATUHUMIWA[/h]

Taarifa ambazo zimetufikia kupitia kituo cha WAPO Radio FM zinaeleza kwamba kuna bomu limelipuliwa kwenye kanisa katoliki la Mtakatifu Karoli, Ruanga huko USA River jijini Arusha, ambapo wanakwaya takriban 6 wamejeruhiwa.

Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo zimetufikia, zinaeleza kwamba watuhumiwa ni jeshi la Polisi, na kwamba walirusha kitu kinachosadikiwa kuwa bomu - lililojeruhi 6, ambapo 4 kati yao wameruhusiwa baada ya matibabu kwenye hospitali ya Mission na ya Wilaya ya Arumeru.

Majira ya saa sita na nusu, waumini walidai kuona gari la polisi likipita kwa kasi, na lilipowakaribia walistuka mlipuko ukiwarusha pembeni, ambapo walijikuta na majeraha na usoni, mapajani na maeneo mbalimbali ya mwili. Kisha baada ya hapo gari ilisogea mbele na kuanza kurusha mabomu kwa watu wowote iliokutana nao.

Hadi sasa inaelezwa kuwa uchunguzi umeshaanza kufanyika, huku Kamanda Liberatus Sabas akikataa kuzungumzia zaidi suala hilo. Alipotafutwa na WAPO Radio FM, hakueleza kwa kina, lakini akasema kuwa sio suala la kwaya kama ambavyo imeelezwa, bali ni wakinadada wawili na kwamba hawezi kuzungumza zaidi, bali kesho (Ijumaa) atatoa taarifa rasmi na iliyo kamili kwa vyombo vya habari.

Alipoulizwa kuwa kama ni kweli jeshi la Polisi linatuhumiwa kuhusika, alisema kuwa atazungumza kesho kuhusiana na tukio hilo. Tukio hili limetokea ikiwa ni siku mbili zimepita tokea kuapishwa kwa Inspekta Jenerali wa Polisi mpya, Ernest Mangu ambaye amechukua nafasi ya IJP Said Mwema aliyestaafu.

Source: Gospel Kitaa.

IJP Mwema
 
Kwa hiyo unataka kutuambia polisi wetu ni vichaa au?

Hapo gongo haijaruhusiwa mnapost vitu kama hivi ikiruhusiwa itakuwaje?

lukosi, kwa hili shirikisha kichwa kidogo, lipe walau muda tupa ukweli !
 
Back
Top Bottom