Mlipuko mkubwa watokea kwenye Kanisa Katoliki Arusha, watu kadhaa wajeruhiwa

Status
Not open for further replies.
matangazo yamelejea baadae yakakatika tena mtangazaji anasema kuna mtu alikata mawasiliano hii nazani mwendelezo wa hujuma ili lema asisikike hewani mulongo na watu wake wanahusika sana
 
(1) Hand grenades zinapatikana kwa urahisi Tanzania? Ziko habari za washambuliaji kukimbia na basi dogo (hiace). Polisi wafikirie kuna mtandao na sii mtu mmoja amehusika.

(2) Balozi mzima akiwa kwenye shughuli ya watu wengi hakuna ulinzi wa kiserikali? Walinzi hawangemwona mshambuliaji kama ni kweli kuna mtoto alimwona akapiga kelele za mwizi?

(3) You can rule out M23. Hawana motive ya kushambulia kanisa Arusha. Lazima kuwaza motive kwanza.

(4) Jukumu kubwa la polisi ni kulinda raia na mali zao? Walitekeleze vizuri, na wakamate wahusika wa kweli. Kukamata kama walivyomkamata yule Mkenya wa Ulimboka haikubaliki. Si vema kutangaza tu kwamba wanamshikilia mtu mmoja ili kuturidhisha, lazima awe na uzito kikweli.
 
Haikuwa hitilafu mtangazaji wa arusha anasema kuna mtu kazima mawasiliano...lakini yamekatika tena!!
 
Ndugu WanaJamvi;

Kwa muda sasa kumekuwa na hoja mbali mbali juu ya uhalali wa uwepo wa Ubalozi wa Vatican hapa Tanzania. Katika hili kuna, kuna pande kuu mbili zinazokinzana - wanaopinga na wanaounga mkono kama ifuatavyo:-

(1) Wanaopinga: wanajenga hoja kwamba kwa kuwa Vatican ni nchi ya kidini (Kikatoliki) na kwa kuwa, kwa mujibu wa Katiba, Tanzania haina dini hivyo sio sahihi kwa "nchi" hiyo kuwa na ubalozi wake hapa nchini. Wengine wanaenda mbali zaidi kiasi kwamba hawataki kukubali Vatican ni nchi. Hata hivyo "wanalegeza" masharti kwamba kama Vatican ina ubalozi wake hapa basi ni halali kwa Tanzania kama nchi kuwa mwanachama wa taasisi za kidini kama OIC. La kushangaza hapa ni kwamba kwao uhalali wa Ubalozi wa Vatican utakuwepo endapo Tanzania itakuwa mwanachama wa hizo taasisi za kidini vinginevyo sio halali.

(2) Wanaounga mkono:hawa wanajenga hoja kwamba; kwanza Vatican ni nchi huru, yenye mamlaka kamili, na inayojitegemea kwa mujibu wa tafsiri sahihi ya neno "nchi" lilivyo na linavyotambulika kimataifa. Na wanaenda mbali zaidi kwamba sio tu kwamba Vatican ni nchi bali inatambulika hivyo rasmi na UN. Hivyo, kwa hoja hii, ni sahihi kabisa Vatican na Tanzania kuwa na mabalozi wanowakilisha nchi zao.

MLIPUKO WA LEO:

Kati ya viongozi wakuu wa Kanisa waliokuwepo kwenye shughuli ya leo kule Olasiti, Arusha, ni Balozi wa Vatican nchini Tanzania ambaye pia ana hadhi ya Askofu Mkuu. Hivyo zimeanza kuzagaa habari pengine kutokana na ukinzani wa baadhi ya makundi kutotaka Vatican kuwa na ubalozi wake hapa nchini, kuna uwezekano pia mlengwa mkuu alikuwa Balozi husika. Mimi sijui, ila kama GT tudadavue na hili.

LAWAMA:

Lawama pia zimeanza kuelekezwa kwa serikali kwa kutochukua hatua madhubuti na kwa wakati pindi zinapotokea chochoko kama hizi katika jamii. Kwa mfano, hili la upotoshoji wa uhalali wa Ubalozi wa Vatican hapa nchini propaganda zake zimeenezwa kwa muda mrefu sana kwa njia mbalimbali kama mihadhara, ibada, na hata kwenye media mbalimbali. Badala ya serikali kutolea ufafanuzi wa uhalali wa huo ubalozi, imekuwa kimya bila kujali athari za baadaye za propaganda hizi chafu pengine kwa falsafa ya "ni upepo tu utapita". Je, ni kweli serikali inastahili lawama katika hili?

HITIMISHO:

Je, kama serikali ikitekeleza madai YOTE ya haya makundi, kuna uwezekano wa chokochoko hizi kukoma na hivyo nchi yetu kuwa ya amani na utulivu kama ilivyoachwa na waasisi wetu? Lakini je, walengwa wa haya matukio ni wakatoliki peke yao? Au ni pamoja na makundi mengine? Haya matukio yana uhusiano wowote na siasa za nchi yetu? Mimi sijui, nalileta kwenu wakuu.
 
kumbe kuna mtu alizima mashine za radio maria wakati Lema anaongea hapo Arusha
Mtangazaji Mahonge Godfrey kasema na wkt akiongea ikazimwa tena.
nani huyo mwenye mamlaka ya kuzima mtambo wa radio hapo Arusha kama sio usalama?
labda hawakutaka tusikie kauli ya Lema.
 
Sio moto wa hotuba, bali wameona ni upuuzi kuingiza siasa kila sehemu.

naubaliana na ww, anatuhamisha mawazo kwenye ishu muhimu, leo amechemka zaidi yena. Inabidi aende shule kusoma communication skills
 
Wakuu ghafla Mbunge wa Arusha akiongea ametoweka hewani na sasa nyimbo zinapigwa nani mwenye taarifa za tukio hili toka eneno la tukio?Wameogopa maoni yake?
Itakuwa ni order kutoka juu!. Lema anahesabika kuwa tishio la amani kila akifika tuu mahali kwenye mikusanyiko ya watu!. Wasimkatisha, angeweza kurelate hilo tukio na kwa kuisingizia serikali ya CCM kushindwa kutimiza wajibu wake wa ulinzi na usalama wa raia na mali zao!, hivyo kuiponza CCM ambayo inapendwa sana Arusha na Moshi, ipunguzwe kupendwa!.

Hata ningekuwa mimi studio za Redio Maria, ningemkata!. Amemponza mkuu wetu wa mkoa wa Arusha, kila anapopita, anaonekana kituko!.Lema akiendelea hivi, wanaweza hata kumtumia "vijana!".
Pasco.
 
Matukio haya yote ikiwemo swala la matokeo ya
kidato cha nne kutangazwa na Mh Lukuvi kuwa
tume inashauri yafutwe na hili la Leo la Mlipuko wa
Bomu kwenye kanisa la Katoliki Parokia ya Urafiki
Olasiti mkoani Arusha ni zengwe la kutaka
kuwaondoa watanzania katika ukweli juu ya hotuba iliyotolewa wiki iliyopita na Kambi ya Upinzani
Bungeni juu ya Ujangili uliokisiri humu nchini na
kuhusishwa na Viongozi wa ngazi za juu
Serikalini,,,,,,,



Bado tunasisitiza kuwa Kinanaaaa, Weka Mbali na Tembo
huku tukiendelea kutafakari tukio la leo ni huzuni sana lakini watanzania tusahau kuwa Tembo wetu wanazidi kuhangamia kwa kukosa watu wa kuwalinda na pia TWIGA wetu wana safirishwa.
 
Kuna taarifa kutoka eneo la tukio kwamba Mulongo alichafua hali ya hewa tena akasema 'kufa ni kitu cha kawaida'
 
Leo Lema kachemka, sikutegemea angekuwa na jazba kiasi hicho. Huwezi ukatoa conclusion kirahisi kiasi hicho kwenye public.

weka kasemaje acha ku generalize kila kitu.... weka hapa alicho sema.
 
BAADA YA KUJA UISLAM NA UKRISTO -- SIKU HIZI HAKUNA :

wapare, wamakua, wahaya, wasukuma nk. - - - NA VIPI UKIJA KUSIKIA KWAMBA CHANZO CHA MLIPUKO NI HITILAFU TU YA UMEME? ..... #MDINI - Ni yule anayeanza kuuzungumzia.... shame on You

Yes, ni kweli kabisa, jamaa aliingia kanisani amebeba itilafu ya umeme akairusha ndani ndio mlipuko ukatokea na kujeruhi/kuua watu, una akili sana wewe.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom