Mlipuko jijini Dodoma

clion dismas

Senior Member
Joined
Aug 6, 2017
Posts
185
Reaction score
169
Wanabodi

Mlipuko mkubwa sana wa neno la MUNGU unatarajiwa kushika kasi kuanzia leo tarehe 4 mwezi wa 5 hadi 25/5/2019 katika viwanja vya kanisa la waadventista wasabato dodoma kati.

USIPANGWE KUKOSA KUKUTANA NA NGUVU YA MUNGU KWA MAJUMA HAYA.

MASOMO YATAYO TOLEWA NI:-
1. AFYA NA KIASI
2. KAYA NA FAMILIA(KLINIKI YA NDOA NA NAMNA YA KUPATA MKE/MME MWEMA)
3. MAFUNDISHO MAKUU YA NENO LA MUNGU


Mgeni rasmi katika ufunguzi wa mikutano hii awe waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.


MADA KUU: "UZOEFU WA NGUVU YA MUNGU".
MHUBIRI: DR BARAKA MUGANDA
MUDA: SAA 12 JIONI MPAKA SAA 2 KAMILI USIKU.

FATILIA KUPITIA: ROCK FM DODOMA, STAR TV, HOPE CHANNEL TANZANIA, ADVENTIST WORLD RADIO NA MORNING STAR RADIO



USIPANGE KUKOSA MBARAKA HUU. NENO LA MUNGU LINA NGUVU ZAIDI YA UPANGA, BOMU NA NYUKLIA.

EWE MWENYE SHIDA YAKO MPELEKEE MUNGU PALE MSALABANI. LAKINI USISAHAU KUIOMBEA SERIKALI YAKO.

BARIKIWA NA BWANA.

( TAARIFA NILIZOPATA HIVI PUNDE, ALIYEFUNGUA MKUTANO NI MHANDISI MASAUNI MASAUNI, N/W MAMBO YA NDANI).
 
Mbona huyo mgeni rasmi kafungua mkutano mapema kabla ya saa 12 jioni kama ilivyokuwa imepangwa mkutano kuanza?
 

Kichaa wewe, mseme mnataka sadaka mchangiwe hata humu. Mzungu alituharibu sana ngozi nyeusi kutuletea dini nazo zikatupumbaza
 
Kwa mara ya kwanza nakutana na msabato muongo. Inakuwaje utudanganye kuwa kuna mlipuko Dodoma? Kwa nini unatumia njia za ujanja ujanja kuvuta watu kwa Mungu? This is totally wrong... Ilitakiwa angalau basi uandike 'Mlipuko'... Kuonesha kuwa neno mlipuko lina maana tofauti na maana halisi ya neno hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…