Mliowahi kunisaidia humu JF Mungu awabariki sana. Nazidi kuwashukuru

Superleta

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
466
538
Habarini za Jamiiforum ndugu zangu mimi ni nzima na buheri wa afya tele namshukuru Mungu sana

Waswahili wanasema "wafadhilika wapundaka" ikiwa na maana kuwa "asiyekumbuka fadhila hafadhiliki huyo".

Nina kila moyo wa kushukuru jamiiforum sana tena kwa moyo wangu wote kusema kweli nikiri kwa kinywa changu kuna kipindi nilikuja humu kuomba msaada ukweli ni kuwa nilikua na hali mbaya kweli sijawahi kupitia kipindi kigumu kama cha mwaka jana kati ya December mpaka February

Wapi naweza kukopeshwa 50k au 100k nina shida nayo kiukweli

Nilipita kipindi kigumu sana mateso yake hayaelezeki sijui hata nifafanue vipi misukosuko ilinipiga hadi maji nikaita mma lakini humu kuna kipindi nilipost nahitaji msaada wengi walidhani labda nilikua tapeli lakini haikua hivyo lakini wana haki ya kuhisi hivyo kwasababu ulimwengu wa sasa watu wamekua sio wa kweli hususan mtandaoni na wapo wanaotapeli watu ila mim kipindi kile daaah

Siwezi kumsamehe milele, ameyaharibu maisha yangu pakubwa sana

Pia kulikua na uzi niliandika kipindi kile nikiomba msaada wa shilingi elfu 3 (3000) maana nilikwama kabisa sikua hata na hamsini na sikua hata na matumaini ya kupata hata 50 kwa week kadhaa zilizokuja kwa kipindi hicho ila mliniamini mkanisaidia sana mkanibebaah daaah siwezi kusahau kabisa nikisahau nitakua sina shukurani lakini nawashukuru sana.

Wapo walionishauri sana kuhusu hali yangu nawashukuru sana,wengine waliguswa kabisa wakanipa msaada mkubwa sana nawashukuru sana tena sana mungu azidi kuwapa mahitaji yenu ya kila siku.

Mlinifariji wakati wa dhiki na kipindi kigumu na sisi waafrika tumekua hatuna desturi ya kukumbuka fadhila au msaada ila mimi nitaendelea kukumbuka milele wanasema rafiki wa kweli huonekana wakati wa shida na dhiki

Nawaza sana wale walionisaidia wasingenisaidia kwa kipindi kile ingekuaje?Waliniokoa sana mungu awabariki sana na azidi kuwapa kila mtu mtakachoomba

Asanteni sana tena sana leo hii namshukuru mungu kwasasa mambo sio mabaya napambana mambo yanaenda navyotaka kwani kwasasa nimeshajua ramani ya dar kuzisaka kama kawaida huku nakomaa na kitabu kwa kweli hata sijui nitoe neno gani maana kuna wakati nikijitazama nilipofika najiuliza na kujishangaa "hivi ni mimi kweli?" ...."hivi ni mimi nina hichi na hichi?"Nawashukuru sana tena sana.

Nitazidi kuwaombea mzidi kusonga mbele na zaidi mfanikiwe kwa kila jambo maana daaah mliniokoa sana ndugu zangu

Sitoacha kukumbuka milele na nitazidi kuwaombea nyote.
 
Ni vizuri na inapendeza kuona aliesaidiwa kafanikiwa, na wewe uje kusaidia wengine.
 
Umefanya jambo jema kushukuru. Lakini jambo moja kwenye huo uzi wako hapo kuhusu Mjomba.

Umeshindwa kabisa kusamehe. Nakushauri mkuu samehe jambo alilo kutendea mjomba. Samehe na potezea ili ufungue milango yako ya baraka.

Ni kweli mjomba alikudhurumu na alikutendea vibaya ila hata maandiko ya dini yanasisitiza saana tusameheane.
 
Nilishamsamehe tayari kaka
Umefanya jambo jema kushukuru. Lakini jambo moja kwenye huo uzi wako hapo kuhusu mjomba.

Umeshindwa kabisa kusamehe. Nakushauri mkuu samehe jambo alilo kutendea mjomba. Samehe na potezea ili ufungue milango yako ya baraka.

Ni kweli mjomba alikudhurumu na alikutendea vibaya ila hata maandiko ya dini yanasisitiza saana tusameheane.
 
Back
Top Bottom