Mliosema anaupiga mwingi, ngapi ngapi huko?

Mliosema anaupiga mwingi, ngapi ngapi huko?

Nina swali kwa wale anti 5th Regime ambao baada tu ya kumpoteza raisi wa aina yake,turufu ya kweli kupata kutokea toka kuasisiwa kwa taifa hili.

Lile kundi ambalo mlikuwa mkishabikia kuwa mama anaupiga mwingi vipi hali inakwendaje huko. Naombeni mtupatie mrejesho je, bado anaupiga mwingi?
Tunaongoza 5-0
 
CCM wanakwenda na upepo, ukivuma kwa kusi huko huko, ukivuma wa kisulisuli wanaruka nao..

walewale waliosema Magu anaupiga mwingi mno ndiyo walewale leo wamegeuka na kusema Mwenyezi Mungu kamchelewesha kumpa madaraka mama... yaani anaupiga wa hatarii - laah
 
Mama kaingizwe mkenge na Msoga,kuweka watu ambao ndo waliipeleka CCM shimoni.
Tusipende kuhamisha lawama na tupende kuchukua responsibility..., Kama anapotoshwa basi angalau shida / au kutumbukia shimoni tungetumbukia kwa anagalau kimo kilekile..., ila nadhani things are much much worse..., Kama ni kuuma hakuna kupuliza ni mwendo wa kutafuna tu.....
 
Tuache masihara, Pira analopiga Mama kwa muda mfupi ni balaa. Madarasa kila kona, Kusini,Kaskazini,Magharibi mpaka Mashariki...hakuna ubaguzi wa kanda au kabila. Barabara za lami za wilaya na mikoa zinaanza kuchipuka,zahanati na vituo vya afya alivyoacha Hayati Magufuli kumalizika vinamalizwa na vipya juu! So far she is good.
 
Mama anaupiga mwingi sana. Hata Bashite anajua asiyempenda kaja....Nape
unadhani Nape ana la kumfanya Bashite ?, Bashite hashikiki, na soon atateuliwa tu hata Sabaya hatomaliza miaka 5 jela
 
Tuache masihara, Pira analopiga Mama kwa muda mfupi ni balaa. Madarasa kila kona, Kusini,Kaskazini,Magharibi mpaka Mashariki...hakuna ubaguzi wa kanda au kabila. Barabara za lami za wilaya na mikoa zinaanza kuchipuka,zahanati na vituo vya afya alivyoacha Hayati Magufuli kumalizika vinamalizwa na vipya juu! So far she is good.
Ata kwangu bado namuona yupo vizuri.
 
Nina swali kwa wale anti 5th Regime ambao baada tu ya kumpoteza raisi wa aina yake,turufu ya kweli kupata kutokea toka kuasisiwa kwa taifa hili.

Lile kundi ambalo mlikuwa mkishabikia kuwa mama anaupiga mwingi vipi hali inakwendaje huko. Naombeni mtupatie mrejesho je, bado anaupiga mwingi?
Unaongea nn?
 
Acha porojo
 
WIZARA YA UTUMISHI KUTIMIZA AGIZO LA RAIS KWA WAKATI.

Na. James K. Mwanamyoto-Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama amesema ofisi yake imejipanga kupandisha mishahara ya Watumishi wa Umma kwa wakati kama alivyoelekeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani 2022 yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma.

Akizungumzia utekelezaji wa maelekezo ya kuwapandisha mishahara Watumishi wa Umma, Mhe. Jenista amesema ofisi yake itafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha ifikapo Julai, 2022 kila mtumishi wa umma anapata mshahara mpya. Hivyo amewataka watumishi wa umma kuwa watulivu wakati zoezi hili likiendelea kushughulikiwa na Serikali.

“Mimi na watendaji wangu tumeanza kupitia taarifa za Watumishi katika Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara ili kushirikiana na Wizara ya Fedha katika kukamilisha zoezi la kupandisha mishahara ya Watumishi wa Umma, itakapofika Julai 2022 kila mtumishi atakuwa amepata mshahara mpya kama ilivyoelekezwa na Mhe. Rais,” Mhe. Jenista amesisitiza.

Mhe. Jenista ameongeza kuwa ahadi ambazo Mhe. Rais amekuwa akizitoa kwa watumishi wa umma zimekuwa zikitekelezwa kwa wakati, hivyo jambo hili la mishahara litatekelezwa kama alivyokusudia.

Katika kuhakikisha mishahara ya watumishi wa umma inapanda kwa mujibu wa maelekezo ya Mhe. Rais, Waziri Jenista amewataka Maafisa Utumishi wote katika taasisi za umma nchini kuhakikisha wanatekeleza ipasavyo kila mwongozo utakaotolewa na ofisi yake kwa lengo la kukamilisha zoezi la upandishaji wa mishahara ya watumishi.

“Maafisa Utumishi hakikisheni mnatekeleza maelekezo yatakayotolewa na ofisi yangu kwa uzalendo na uadilifu wa hali ya juu kwani atakayekwenda kinyume hatua kali zitachukuliwa dhidi yake kwa kukiuka maelekezo halali ya Mhe. Rais,” Mhe. Jenista ameongeza.

Akizungumzia utekelezaji wa maelekezo mengine aliyoyatoa Mhe. Rais likiwemo la watumishi walioondolewa kutokana na vyeti vya kughushi, Mhe. Jenista amesema wameshafanya mawasiliano na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu ili jambo hilo nalo lifanyiwe kazi ndani ya muda mfupi kwa mujibu wa maelekezo ya Mhe. Rais.

Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan inasimamia na itaendelea kusimamia haki na stahiki za Watumishi wa Umma ili kuwajengea ari na morali ya utendaji kazi katika kutoa huduma bora kwa wananchi
 
Nina swali kwa wale anti 5th Regime ambao baada tu ya kumpoteza raisi wa aina yake,turufu ya kweli kupata kutokea toka kuasisiwa kwa taifa hili.

Lile kundi ambalo mlikuwa mkishabikia kuwa mama anaupiga mwingi vipi hali inakwendaje huko. Naombeni mtupatie mrejesho je, bado anaupiga mwingi?
Tatu bila,anataka kukunwa sasa hivi.
 
Back
Top Bottom