Mliopo kwenye ndoa mna kazi sana

Mliopo kwenye ndoa mna kazi sana

Ungemjibu hivi, unampenda kwa sababu anayemfanya apendeze sio wewe, na kwa sababu hakai na wewe kwa muda mrefu mnakuwa hamchukizani au kuhisi harufu za shombo zenu.
Hawashei majukumu common ya familia. Mnachozungumzia nyie mkikutana ni ngono na furaha tu. Mkikaa pamoja lazima mtakerana tu, so endeleeni kufurahiana nje ya ndoa tu.
 
Mbona msela mmempopoa sana, kafeli wapi ba ndugu?????
Kati ya wote waliosoma thread, wewe umesoma na kuielewa. Hongera sana mkuu.

Kuna vijitu vimesoma, havikuelewa, vikaanza kumpopoa mjumbe bila sababu.

Alichokiandika jamaa ni kuwa, mwanamke amemwelewa jamaa. Lakini hakusema aliombwa pesa wala mwanamke hakusema atamwacha mume wake akaolewe na jamaaa, hapana. Kazungumzia kupendwa tu.

Kuna wake za watu wana akili zao. Hata ateswe vipi kwenye ndoa yake, hamwachi mumewe. Atakachokifanya ni kutafuta mahali pa kupata faraja tu huku akikomaa na ndoa yake.

Hapa ndipo aliposema jamaa alikuwa wapi maana amemwonesha upendo kupita wa mumewe. Anajuta akiwaza kama angemfahamu penzi la jamaa, basi ndiye angekuwa mwanandoa mwenza wa kudumu. Lakini kwa sasa haiwezekani kwani alishaolewa na mwingine.

Tujifunze kabla ya kulaumu au kukosoa.
 
Kuna wadau wakisoma ulichoandika mioyo yao unakua km unawaunguza na Pasi ya Mkaa,
 
Tuna tabia ya kusema mwanamke akichepuka ni malaya, lakini hatumhukumu mumewe kwa tabia zake dhidi ya mkewe.

Nitoe mfano wa ndoa ya jamaa ninaye mfahamu. Mkewe alikuwa cool sana. Mwanamke aliyejitoa kwa mume yeye na mali zake.

Mwanaume alikuwa na mtoto kabla ya ndoa yao. Mwanamke alimpokea na kumlea kwa upendo wote. Mshahara wa mwanamke anausimamia mwanaume kwa 100%.

Pamoja na upole huo kwa mume, kupewa hela ya matumizi ikawa shida, mume kwa wiki kulala ndani akijitahidi sana mara mbili.

Mwanaume hashikiki, ni vimada kila kona. Mke na watoto wamechakaa mavazi kama mke na mume si watumishi.

Ilifikia wakati, mume analala nyumba ya tatu tu hapo lakini atafika nyumbani kubadilisha nguo wakati mkewe akiwa kazini. Akijisikia kumpa huduma ya ndoa ni mara moja kwa wiki au upite mwezi bila tendo la ndoa. Ninamaanisha.

Kweli katika mazingira hayo mwanamke aamue liwalo na liwe, awe na mchepuko, atalaumiwa nani hapo?

Mwanaume kama umeamua kuoa basi mthamini mkeo na wanao. Mpe heshima ndani na nje ili akutambue kama mume na asijute kuolewa kwako.

Sikatai, wapo wanawake wenye tabia mbaya. Hata apewe huduma zote bado atachepuka na kuhonga wanaume kwa pesa za mumewe. Hao nao ni fungu lao. Lakini mwanaume usiwe sababu ya mkeo kuwa malaya.
 
Baada ya kutembea na huyu mwanamke kwa muda sasa, leo ananifungukia hivi:

"Kabla sijaolewa nilitamani sana ndoa. Ila sijui kwanini baada ya kuingia kwenye ndoa, ndio anatokea mwanaume mwengine ambae ananipenda zaidi kuliko mume wangu.

Najiuliza kwanini sikumuona huyu mwanaume siku zote? Malcolm, ulikua wapi siku zote..?"
Kumbe wewe ndie jogoo unatunyandulia wake zetu!,Acha.
 
Back
Top Bottom