Mliooa mnaupata wapi ujasiri huu?

Mliooa mnaupata wapi ujasiri huu?

Mfano mrahisi tu ukiwa na hamu sana na wali ndondo alafu siku ukaja kufululiza kula mwezi mzima baada ya hapo hamu ya wali ndondo itapungua au kuisha kama sio kupata na aleji kabisa
 
Muishinao kwa akili [emoji131], Hili nineno la kimaandiko ukilichukulia juu juu utaliona la kawaida sana, ila ukilichimbua kiundani utaona UKUBWA WA NENO HILI, mta nuniana mtanyimana TUNDA mtagombana lakini mwisho wa siku - rudi nyuma ukumbuke- MUISHI NAO KWA AKILI [emoji16]
 
Sawa huwezi kufanya hivyo kila siku.Ndo mnataka kusema mtu analala hivyo mwezi bila kumgusa mkewe! bila ya sababu za msingi kama ugonjwa ,kulea n.k?.Sidhani kama ntafanya hivyo.nb:Sijaoa
 
Lengo la kulala ni kupumzisha mwili baada ya shughuli za kutwa. Ya nini kusumbuana?😄
 
Kuna kanuni moja kwenye uchumi ya marginal utility. Kwamba kutosholezwa kwako na huduma fulani kunapungua kadri unavyoongeza zaidi huduma hiyo na hamu ya huduma hiyo au kitu kufikia zero hata negative.

Mfano ni kama una hamu ya kula kuku au chungwa. Kipande cha kwanza huwa ni kitamu sana lakini kadri unavyokula vipande zaidi ladha inaanza kupotea na mwishowe unajikuta hutamani kula tena na hata unaweza ona unakula takataka.

Usimtafune kila siku mke wako ipo siku au mume utaharibu mambo. Unafikiri kwa nini ukiwa mpishi wa chakula kitamu huwezi faidi ladha yake wanafaidi wasiojua hata kupika na kukusifia wakati wewe unaona kawaida. Ipo hivyo kwenye ndoa. Mkijuana mtajua namna ya kuhakikisha hamchokani
 
Jogoo hasimami hapo,mpaka apewe stata; ndio maana wako hivyo.
 
Ishi maisha yako wewe kama wewe usiangalie maisha ya watu wengine.
 
Back
Top Bottom