Mliomshauri rais mmempotosha

Mliomshauri rais mmempotosha

Buldoza

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2013
Posts
2,307
Reaction score
986
Rais kama binadamu mwingine, kuugua kwake si jambo la ajabu. Tumeshuhudia mara mbili rais akianguka kwenye mikutano ya hadhara ni zaidi ya miaka tisa sasa hata baada ya hapo hatujawahi kitangaziwa ni ugonjwa gani unaomsumbua rais wetu.

Imekuwaje leo, amefanyiwa upasuaji kwenye sehemu za siri za mwili wake ndipo waibuke watu na kuutangazia umma ugonjwa huo? Je hii si kumdhalilisha kiongozi?

Kama nia ilikuwa ni ku-divert attention ya watu toka wizi wa Escrow na kuhamia kujadili rais alikuwa na Tezidume, basi huo mpango umefeli vibaya sana.

Je waliobuni wazo hilo hawakujua kwamba hili suala la Escrow limeshavuka mipaka na kwamba linafuatiliwa na mataifa makubwa sasa na si rahisi kulizima kwa michezo ya kitoto kama huo?

Je imekuwaje rais nae akubali kujitoa kafara ya faragha yake ili kulinda ufedhuli wa Escrow kama hausiki binafsi au mwanafamilia wake?

Hii ni aibu. Rais kwa hili naye inampasa ajipime.
 
Hahahahahaaaaa umenena vyema sana
 
Mimi nikiwa mganga wa kienyeji nilishangazwa sana kwa daktari aliyemtangaza Rais wangu kuwa hatakuwa dume tena kwa sababu tezi dume limeondolewa na kubaki na tezi jike. Kutangaza jambo kubwa la namna hii si tu ni aibu lakini pia lilimdhalilisha Rais wangu na kumhurumia mama salma kuhusu maisha yake ya ndoa ya baadae Jambo kama linapotangazwa kuhusu Rais wetu inatakiwa utolewe na ufafanuzi wa kina tezi dume maana yake ni nini na athari na faida zake kwa binadamu kuwa nalo au kulikosa ni nini na si kwa namna mlivyofanya ninyi.
 
Hili lakuanika ugonjwa Wa Mh. Rais Halikunifurahisha. Na waliobuni strategy hiyo lazima waadhibiwe. Sina uhakika kama Lina uhusiano na ESCROW ila kama kunahusiano basi waliobuni mkakati wenyewe ni wahuni na wasiyo na chembe hata moja cha utu na uadilifu.
 
Na kama nia ilikua ni kutuelezea ugonjwa wa rais, mbona hawakutueleza wakati anaondoka nchini kwenda kufanyiwa opesheni kama ilivyokuwa kwa Mwalimu Nyerere? Au madakatari wake walikuwa hawajui anachouguwa Mheshimiwa? Au Ugonjwa ulianza ghafla akiwa safarini?
Na kama haitoshi huu utamaduni wa kutoa namba ya simu ya rais ili watu wamtumie salamu za pole ni kichekesho kingine cha karne.
Hivi hawa watu wamemwonaje Profesa?
 
mimi mwenyewe sikupenda ugonjwa wa rais kuwekwa hadharani na ukichukulia sehemu ulipo ugonjwa wenyewe!!lakini nakuhakikishia jk himself gave a consent,.si unamjua bwana misifa.
 
wakuu hapa mmenena sio vizuri wamefanya kwanza adabu hakuna nakuendelea kutaja au kujadili ugojwa wa binadamu mwenzako bila kusikitika ikikupata utafurahia,nakuambia
 
Kisheria huruhusiwi kutoa siri ya mgonjwa hadi yy mwenyewe atoe go ahead,(CONSENT). Sasa rejea kipindi kile Mwakyembe ameugua ule ugonjwa wa kuumuka mwili mzima; hakuna aliyeruhusiwa au kwa kibali chake tu ndo iliruhusiwa kuutangaza huo ugonjwa, kumbuka polisi walivyokurupuka kusema kuwa SIO SUMU, kumbuka reaction ya mwakyenbe, sasa kwa hii ya JK. yy ndiye aliruhusu, nachelea kuihusianisha na ESCROW account ingawa TANZANIA kila kitu kinawezekana.
 
Hahahahahaaaaa umenena vyema sana

Mkuu Elli kama hali ndio hiyo sitaona ajabu ikiwa hivi tena
ImageUploadedByJamiiForums1416135889.866414.jpg
 
Last edited by a moderator:
Afichae maradhi kifo humuumbua.

Kuhusu kuanguka kwa Rais, ulikuwa na uchovu na mchoko wa kufanya kazi bila kupumzika vya kutosha. Hilo lilisemwa au hukulipenda?
 
Kisheria huruhusiwi kutoa siri ya mgonjwa hadi yy mwenyewe atoe go ahead,(CONSENT). Sasa rejea kipindi kile Mwakyembe ameugua ule ugonjwa wa kuumuka mwili mzima; hakuna aliyeruhusiwa au kwa kibali chake tu ndo iliruhusiwa kuutangaza huo ugonjwa, kumbuka polisi walivyokurupuka kusema kuwa SIO SUMU, kumbuka reaction ya mwakyenbe, sasa kwa hii ya JK. yy ndiye aliruhusu, nachelea kuihusianisha na ESCROW account ingawa TANZANIA kila kitu kinawezekana.

Mkuu hapo ndio umedhibitisha kuwa uhusiano upo. Maana kwa jinsi alivyo msanii aliamua ugonjwa utangazwe ili wakati huu wa sakata hilo aonewe huruma na asihusishwe nalo. Ni sawa na mtu unayemdai na akapata msiba, hata kama hauhusiani na deni atahakikisha unaufahamu msiba huo ili kupunguza makali ya kumdai.
 
Daaa yani wanamsema rais vibaya pole jk wetu make ugonjwa kila MTU unampata ila wasaidiz wako ndio wanakuzalilisha
 
Afichae maradhi kifo humuumbua.

Kuhusu kuanguka kwa Rais, ulikuwa na uchovu na mchoko wa kufanya kazi bila kupumzika vya kutosha. Hilo lilisemwa au hukulipenda?
nyie wapambe Wa jk kila kitu mbapinga
 
Afichae maradhi kifo humuumbua.

Kuhusu kuanguka kwa Rais, ulikuwa na uchovu na mchoko wa kufanya kazi bila kupumzika vya kutosha. Hilo lilisemwa au hukulipenda?

Basi wangeanguka wengi! Au alikuwa anafanya kazi ya kubeba magunia mpaka akachoka kiasi hicho? Mkubali tuu kuwa afya yake ni mgogoro na sio jambo la ajabu kwa mwanadamu.
 
Afichae maradhi kifo humuumbua.

Kuhusu kuanguka kwa Rais, ulikuwa na uchovu na mchoko wa kufanya kazi bila kupumzika vya kutosha. Hilo lilisemwa au hukulipenda?

Huo ugonjwa aliupata ghafla akiwa safarini? Na methali uliyoitumia haina uhusiano na kuwaambia watu kwamba umefanyiwa operesheni ya busha labda, maana yake ni kukaa na ugonjwa kwa siri bila kwenda kutibiwa kwa kuhofu watu wasijue.
Huo uchovu unakuwaga siku ya kwanza tu ya kampeni?
 
hivi mkapa si alipokuwa anaumwa mguu si magazeti yaliandika pia
 
Back
Top Bottom