Huyu jamaa amesahau mkuu alichofanya wizara ya afya? Hatamtengua CAG ili aone mwisho wakeNafikiri bwana mkubwa mjengoni pale anatatizo fulani, na kama atakosa ushauri mzuri basi tutegemee kuyaona mengi sana katika kipindi chake kichache kilichobaki kuliko tuliyoyaona muda uliopita.
Ukimcheki toka ule uchaguzi wa ndani wa ccm, alionekana kuwa mkali mpaka akamzimisha kwa muda mwenzake kwa kumtandika bakora, lakini cha kushanganza baada ya kuingia mjengoni akaendelea kujisifia kuwa kwao ugogoni kutumia bakora ni sahihi na aliendelea kujisifu badala ya kuomba msamaa kwa kosa alilomfanyia mwenzake.
Vitisho viliendelea tena, kwa Zitto, kwamba angeweza hata kumfungia asitinge mjengoni hata kwa kipindi chote cha miaka mitano. Mifano mingine ni hili la akina Mdee na Lema.
Kwa hali ya kawaida, sidhani kama hili linaanzia hapohapo Mjengoni, kuna uwezekano mkubwa sana lina relate na family matters, yaani kama haupo na furaha kutoka nyumbani kuanzia watoto wako, mweza wako na wanaokuzunguka basi ni vigumu sana muda mwingine kuweza kumudu kazi za kiofisi. Sisi wa maofisini tunayaona haya kila siku.
Kuhusu hili la Prof, litamsumbua sana ndugu huyu kwa sababu ya msimamo wa Prof na ndiyo maana anafanya juu chini hata kumchonganisha na ndugu Rais ili jamaa aachie ngazi na iwe furaha yake na pengine atasimama pale Mjengoni na kusema kazi amemaliza na kujisikia wa furaha zaidi. Lakini what will be next kama hasipojiuzuru? Je kejeri juu ya Prof zitaendelea ama atatafuta angle nyingine na hata ya kukwamisha shughuli za Serikali kiasi kwamba Prof atoke tu.
Ingalikuwa ndani ya mjengo kungalikuwapo na idadi ndogo sana ya wale wa ndiyo basi ningalishauri wamuondoe ndugu huyu kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani nane.