Mlioachana na wake zenu wa ndoa, ushuhuda au ushauri wenu unahitajika tafadhali

Ktk vitu havibadiliki kwakuwa vimerithiwa ni kiburi, ktk ndoa nyingi magomvi mengi kabisa ni kiburi kwa mwanamke, kisirani kisicho na mwisho, ubabe na migomo baridi, kutokuheshimu mume, kutokujali mume.
Ushauri mkuu kama mazungumzo yamekosa kuleta amani, basi fikiria maisha yako na wanao na uache kbs kumfikiria mwanamke, mtelekeze kiaina ktk akili yako ili uweze kufanya mambo ya msingi yenye tija na maendeleo kwak9 na kwa wanao.
Mfanye kama mfanyakazi wa nyumbani bila kumwambia, usimnunie usigombane nae, usimchukie ila usimfikirie na usimpe nafasi akufikirishe. Sio kazi rahisi ila ukiifanya kwa muda utaimudu.
Mfano ukitaka sex na akagoma usichukie ukiamka asubuhi siku iwe sawa na usitake tena sex wala kuulizia mpaka ataanza kujistukia mwenyewe. Chochote utakachomwambia akigoma au kupinga muache fanya mwenyewe na usimtume tena kitu hicho, fanya aone kuwa kumbe unaweza bila yeye.
 
Unaongelea vitu vya kufikirika mkuu,

kunipenda sana haiwez kua tiketi ya yeye kashindwa kutekeleza wajibu wake Kama Mama au mke wangu ktk familia.

Maisha ya ndoa Ni Zaid ya Neno "nakupenda"

Tuna watoto wanatakiwa wale,wasome, wamjue Mungu, nidhamu n.k

Maisha ya ndoa hayawezi kwenda sawa Kama unayaishi maisha yale ya kwenye TAMTHILIA za KIFILIPINO.

Vinginevyo utakuja kusingizia Wachawi bure.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekuelewa,umetoa hoja iko vizuri Sanaa
 
Naona kabisa ndoa haina ahueni yoyote, migogoro haiishi na chanzo kikubwa ni ubishi na kiburi cha mke wangu na pia baba mkwe anaongea sana maneno ya kumjaza kiburi bintiye, hilo ndio linapeleka zaidi ndoa yetu mtaroni.

Kama kuna ushauri naomba.

Kama kuna ushuhuda naomba, jinsi ilivyo ngumu kukabiliana na mazoea mwanzo.

Ahsante.
Tafuta pesa heshima itarudi! Ukiona wakwe wanaingilia ndoa yako ujue huna mke hapo huyo anaweza hata kukuletea mimba ya nje ya ndoa, nakushauri ndoa isikusumbue elekeza malengo yako katika kutafuta pesa na ili usiwe na stress tafuta binti was kumpumulia ili ukiwa na haja za kupiga machine unafanya yako huko hafu unatudi nyumbani kimya tu, baada ya miezi kadhaa utamuona huyo mwanamke akinyooka na kurudisha penzi
 
hizi ni baadhi ya sababu ambazo humfanya mwanamke awe na kiburi ndoani:

1. Humshirikishi/unamficha baadhi ya mambo kuhusu kipato chako
2.Unampangia bajeti ya matumizi badala ya yeye kupanga
3. Unamchunguza sana hadi anahisi umemuona malaya hivyo muda mwingi ana kisirani juu yako
4. Humchochei vyema ukuni kama ilivyokua mwanzo wa mahusiano

Chunguza katika hizo sababu kisha uifanyie kazi kupata suluhu ya changamoto yako.
Siyo kweli hivi unajua kuna wanawake wanaolewa ili wapate address? Ukishaishi nae ndo unajua kuwa ni mtu was hovyo hukustahili hata kumchumbia? Ndoa sikuhizi inabidi udadisi historia namalezi ya mwenza wako wengine ni matatizo yanayojitembeza
 
Ila kitu kimoja mpaka sasa sijakielewa. Majority ya posts za malalamiko juu ya mahusiano na ndoa ni wanaume ndo huleta visa vyao humu. Je.. ina maana wanawake hawatendwi? Wanaume wote humu ni malaika?

Huwa naamini katika mahusiano hakuna mkamilifu. Nikikuelezea kisa changu na weakness za partner wangu lazima na mimi nielezee zangu. Sometimes naamini mtu unaweza ona wewe ndo uko sawa kumbe wewe ndo chanzo cha tatizo. Nadhani mkuu ni muda wa wewe kujitafakari. Naamini hatujakamilika ndugu yangu. Hebu rekebisha panaporekebishika.
 
Wanawake wakishikwa masikio na wazazi ,SHOGA zao au Ndugu zao wana tabia ya kukupima mizani mara kwa mara.

Yaani anaweza kukufanyia kitu cha ovyo Tena makusudi kabisa na asiombe msamaha ili tu akupime reaction yako.

Ukinyamaza Wala kutoonyesha kukasirishwa nacho, Basi anaona huo ndo UTARATIBU SASA.

Mfano: -
1. unaeza Rudi nyumban, ukakuta jukum ulilomwachia afanye hajafanya.
Na ukimuuliza anakujibu hivi
"Wee mwanaume nae skuhizi unakiherehere sana, Si nlikwambia ntafanya. Kwani siku si haijaisha?"

Kwa mwanaume, kuambiwa una "KIHEREHERE" Ni fedhea kubwa Sana.

Usipolikemea, siku nyingine atarudia Neno Lile like na utadharilika zaidi.

2.Mkeo Ni mama wa nyumbani.
Sasa Unaeza Rudi nyumbani umetoka kazini Njaa inauma na umechoka ukakuta mkeo hajapika, vyombo vichafu, nguo chafu na watoto hawajaoga.
Ukaskia anakwambia.
"Mme wangu mi napika na wee nisaidie Basi kuosha hivi vyombo"

Kwa mwanaume,
ukikubali TU bila kuhoji kwanini.
Ataona ndio utaratibu na utakua unaachiwa vyombo uoshe.

Mifano ipo mingi, ila wanawake wanatabia ya kutujalibu Sana wanaume.

Usiposimama imara,
Mkeo atakuja singiziwa amekupa limbwata kumbe TU wee ndo umeendekeza.


Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli,Kuna wanawake
wanakwaza hasa ilo la kutoka kazini njaa imekuuma balaa alafu unakuta ajakupikia chakula ndio Kwanza kapozi kwenye sofa anangalia tamthiliya,huku vyombo vichafu,ukijaribu kumwambia ndia kama vile umechokoza nyuki kwenye mzinga hapo lazima mwanaume ukwazike.Pia mwanaume inatakiwa ujue majukumu yake Kama kichwa Cha nyumba kuhakikisha pesa ya matumizi anaacha,mwanamke naye ajue wajibu wake Kama mama kupika,kufua,usafi nyumbani,kuosha vyombo na kadharika.sasa Hawa wanawake wana majibu balaa utasikia oooh nikufulie nguo Mimi sio mfanyakazi wa ndani ni mke.Kwa hiyo anapenda muda wote awe anatazama tamthiliya alafu mwanaume awe anafua au kupika migogoro mingi inasababishwa na kuingiliana majukumu,"TUSIINGILIANE MAJUKUMU".Mume atabaki kuwa Mume na mke atabaki kuwa mke.
 
Ni kweli,Kuna wanawake
wanakwaza hasa ilo la kutoka kazini njaa imekuuma balaa alafu unakuta ajakupikia chakula ndio Kwanza kapozi kwenye sofa anangalia tamthiliya,huku vyombo vichafu,ukijaribu kumwambia ndia kama vile umechokoza nyuki kwenye mzinga hapo lazima mwanaume ukwazike.Pia mwanaume inatakiwa ujue majukumu yake Kama kichwa Cha nyumba kuhakikisha pesa ya matumizi anaacha,mwanamke naye ajue wajibu wake Kama mama kupika,kufua,usafi nyumbani,kuosha vyombo na kadharika.sasa Hawa wanawake wana majibu balaa utasikia oooh nikufulie nguo Mimi sio mfanyakazi wa ndani ni mke.Kwa hiyo anapenda muda wote awe anatazama tamthiliya alafu mwanaume awe anafua au kupika migogoro mingi inasababishwa na kuingiliana majukumu,"TUSIINGILIANE MAJUKUMU".Mume atabaki kuwa Mume na mke atabaki kuwa mke.
Umeongea point sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jambo moja tu Naomba ulifuatilie, angalia mahusiano ya baba mkwe na bintiye. Hapa namaanisha mahusiano ya zaidi ya baba na mwana. You will thank me later
 
Mwanaume uliyeoa na kulipa mahali inayothibitisha kuwa mwanamke na wazazi wake wamekubali kuwa awe chini ya mamlaka yako usikubali kuweka vikao kujadili kiburi au fujo za mkeo.Ukiona dalili za kuwa amebadilika na anaanzisha ligi ndani ya nyumba yako,nakushauri mwanaume nawe ubadilike na usimjali kabisa endelea na mambo yako ya kutafuta maokoto.
Miezi sita baadaye ukiona habadiliki ama kiburi kinaongezeka,piga chini bila kuhitaji ushauri wa yeyote.
 
Naona kabisa ndoa haina ahueni yoyote, migogoro haiishi na chanzo kikubwa ni ubishi na kiburi cha mke wangu na pia baba mkwe anaongea sana maneno ya kumjaza kiburi bintiye, hilo ndio linapeleka zaidi ndoa yetu mtaroni.

Kama kuna ushauri naomba.

Kama kuna ushuhuda naomba, jinsi ilivyo ngumu kukabiliana na mazoea mwanzo.

Ahsante.
pole sana,ningeweza kukupa ushauri iwapo ungetoa maelezo ya kutosha kuhusu,tatizo lako

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom