Mlio safiri na Reli ya TAZARA Tupeane mrejesho

chija

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
276
65
Ambao mmesafiri na reli ya TAZARA Tupeane Uzoefu na kutupia Picha kidogo si mbaya
 
InstaSave.jpeg
 
Baada ya masaa kadhaa kutoka stesheni ya Dar utaingia mbuga ya Serous wanyama kibao, baada ya hapo utaingia Udizungwa ukiwa makini utawaona mbega weupe, ukisha pita Mlimba ndio starehe inaanza kwa wale wapendao uoto wa asili, ma-tunnels, madaraja marefu, milima na misitu ya kupandwa. Ndani ya treni utaoga, kuna buffet & restaurant just to mention a few.... enjoy your journey.
 
Kwa hiyo nauli Ni Bei gani dar mbeya na Ni daraja gani unakuwa comfortable...

Je Kuna beers yaani pombe humo?
 
SGR iende Kigoma kwanza kwa ajili ya kusafirisha mzigo mwingi unaokwenda Congo. Mzigo wa Rwanda ni mdogo na yule Bwana K- game is there to stay and trust me mizenguo itakuwa mingi hapo baade.
Value for money tutaipata Congo na si kwa Mr. Tall.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna treni mbili moja inatoka dar-kapiri mposhi siku ya jumanne na kufika Kapiri mposhi siku ya ijumaa. Hii treni ni ya Tanzania personally sijawahi kupanda naskia ni mbaya na ya kizamani na inaharibika sana njiani hivyo sishauri mtu kupanda.

Then kuna treni ya pili hii inaondoka Dar ijumaa saa 9:30 alasiri na kufika Kapiri mposhi siku ya jumapili. Hii ni treni ya Zambia ni nzuri, safi. Na wazungu wengi wanapenda kuitumia. Hii naweza kishauri watu wapande.

Kwenye treni kuna vyoo/bafu maji ya kuoga chakula pombe etc.

Kuna madaraja ma 4

First class ina vitanda vinne. Na kila behewa lina choo/bafu. Ni class nnayoipenda na unakua comfortable sana.

2nd class hii ina vitanda 6. Kuna choo/bafu. Personally siipendi kwasababu unakua umebanwa hamna space hukai kwa raha.

Sitting class kama siti za kwenye bus. Siti 2 mnaangaliana.

Sitting 2nd class hii kuna viti vya kuegemea lkn vipo kama ma bech . Hii sishauri mtu apande lkn kama huna pesa ya kutosha we komaa.

Abiria wa 1st anaruhusiwa kutembelea classes zote lkn abiria wa class za chini haruhusiwi kwenda sehemu

Sent From Galaxy S20 Ultra
 
Nimekumbuka enzi hizo trip za dar to mang’ula(2007-2009)Trip kama 3 hivi nenda rudi(6) nakumbuka kisaki pale nadhani wale wengine ni ndege pori na nyama pori kwa uchu wa nyama unakula tu. Kuna juice fulani niliziotea zinatokea zambia tamu kinyama(kwangu mimi) ila huku sikubahatika kuzipata.

Sehemu yoyote kwenye usafiri wa treni ni nadra mnoo mie kutumia usafiri wa gari labda kuwe na sababu nyingine za msingi.

Usafiri wa treni ni raha mnoo. Njia ya reli ya kigoma(dar tabora) ndio nimetembea zaidi.
 
Hv kahiyo inayotumia siku tatu safarini huko maporini maji yanatoka wapi😂😂 isijekuwa yaleyale ya bill gates na utakatishaji haramu.

NB: ndege na tren ndio usafiri ambao sijawahi kuutumia tangu nikiwa mdogo ila gari, fisi (sorry mabibi na mababu wachawi ndotoni, just kidding) meli, pikipiki (kwa mara ya kwanza kabisa nilipanda pikipiki mwaka 2010 katika maisha yangu, dada angu alikuwa ananiringishia sana hizi pigo za kupanda pikipiki toka miaka ya 90 tukiwa wadogo mpaka tulipoacha maringo) baiskeli n.k ila katika usafiri wote huu hapa duniani naamini kuna vitu sitakuja kujaribu hata kujifunza kuendesha. Meli, ndege (hii najua ni rahisi sana jua kuchomoza kusini na kuzama mashariki kuliko mimi kugusa usukani wa ndege) na tren. Japo huwa nafurahia sana zile video za you tube za marubani na makaptein maana sidhani kama jamaa huwa wanawaza kupigwa fine na vibao vya 50 pamoja na kutembea na za kubrashia viatu.
 
Nimehamasika! Mambo yakiwa sawa mwisho wa mwaka huu nitajaribu usafiri huu
Dar mpaka tunduma then napanda basi huyooo mpaka swax
 
Mwageni nondo ninampango wa kusafiri na family kwa treni mnamo December
 
Tazara express, first class na TRC Deluxe 2nd class, ukipanda hutajuta

.............................................
Stay home, stay safe
Corona kills
 
Back
Top Bottom