Mlinzi wa Gwajima kortini Kisutu

Mlinzi wa Gwajima kortini Kisutu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,741
gwajima+picha.jpg

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima (kushoto) akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.

KWA UFUPI
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Wilfred Dyansobera kuwa baada ya kuomba mahakamani hapo hati ya wito ya kumuita mshtakiwa George Mzava (43) Aprili 17, jana alijisalimisha akiambatana na Wakili Peter Kibatala.

Mlinzi wa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima jana alijisalimisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka mawili ya kukutwa na bastola aina ya Berretta pamoja na risasi 20 kinyume na sheria.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Wilfred Dyansobera kuwa baada ya kuomba mahakamani hapo hati ya wito ya kumuita mshtakiwa George Mzava (43) Aprili 17, jana alijisalimisha akiambatana na Wakili Peter Kibatala.

Kweka aliiomba mahakama imruhusu amsomee mashtaka ili Mei 4 aunganishwe katika kesi inayomkabili Askofu Gwajima, msaidizi wake, Yekonia Bihagaze (39) na Mchungaji Georgey Milulu (31).

Akimsomea hati ya mashtaka, Kweka alidai kuwa Machi 29 katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni A, akiwa na wenzake Bihagaze na Milulu walikutwa na bastola aina ya Berretta yenye namba ya siri CAT 5802 bila ya kuwa na kibali cha mamlaka inayohusika na silaha na milipuko.

Alidai kuwa washtakiwa hao walifanya kosa hilo kinyume na Kifungu cha 32 (1) na cha 34 (1)(2) na(3) cha Sheria ya Silaha na Milipuko, Sura ya 223 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010.

Wakili huyo wa Serikali, aliendelea kudai kuwa siku hiyo ya tukio, Mzava akiwa na wenzake hao walikutwa wakimiliki isivyo halali, risasi tatu za bastola pamoja na risasi 17 za bunduki aina ya shotgun.

Mshtakiwa huyo baada ya kusomewa mashtaka hayo aliyakana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi bado haujakamilika.

Mshtakiwa aliachiwa kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kuwa na mdhamini mmoja anayeaminika ambaye alisaini hati ya maneno ya dhamana yenye thamani ya Sh1 milioni.

Ijumaa iliyopita, Askofu Gwajima na wenzake wawili walipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka mawili na mawakili wa Serikali, Tumaini Kweka na Shadrack Kimaro.

Askofu Gwajima anadaiwa kutoa lugha chafu kwa Mwadhama Polycap Kardinali Pengo na kuacha silaha risasi tatu za bastola na 17 za bunduki aina ya shotgun katika mikono isiyo salama. Wote walikana mashtaka yote.

Kibatala aliiomba Mahakama hiyo kumruhusu Askofu Gwajima ajidhamini katika kosa la kwanza na Hakimu Wilfred Byansobera alikubaliana na upande wa utetezi na kumpa masharti ya kutoa Sh1 milioni ya ahadi.

Kosa la pili aliloshtakiwa na pamoja na wenzake, Biyagaze, Mzava, Milulu, Askofu Gwajima aliwekewa dhamana ya Sh1 milioni na Wakili Neema Masawe.

Chanzo:Mwananchi
 
Hawa policcm wanavyohangaika na huyo gwajima si wakamshughulikie joka la makengeza lililopiga risasi mbele ya kadamnasi
 
Sheria ifuate mkondo bila kupepesa,majambazi/wauza madawa/wahamiaji haramu, wengi wamejificha katika kivuli cha dini...hii haikubaliki.
 
Sheria ifuate mkondo bila kupepesa,majambazi/wauza madawa/wahamiaji haramu, wengi wamejificha katika kivuli cha dini...hii haikubaliki.

Wale walio beba fedha za escrow kwa kutumia magunia, na wale wa epa, mbona sheria haitumiki kuwashitaki?
mnaonea wanasiasa na watumishi wa Mungu, naamini kanuni iliyo tumika Nigeria Octoba mwaka huu mjiandae
 
Mpaka baba wa watu alizima lkn avoamka tuu bado wanae aisee daaah....
Kashajua kosa lake wamsamehe tuu...
 
Mimi si mfuasi wa huyu jamaa,lakini kwa hili ni matumizi mabovu ya Rasmali tulizo nazo.

...........Kova kama anapita pita humu naomba hyo kesi muitoe,ila mjiandae mtakaposhindwa kufunguliwa kesi ya madai,madai hayo yatalipwa na kwa kodi za wananchi.

Kama ZOmbe alishinda kesi dhidi ya tuhuma za mauaji.SiDhani kama kesi hiii POlisi watashinda,wanasheria wanajua hamna kesi hapo.
 
Hawa mapolisi njaa na choko mbona Albino kila siku walikua wanauawa na hamu hatua kali zilizo chukuliwa kukomesha hyo tabia wezi wakubwa mapolisi mnawafahamu lakini mnawaacha, upuuzi na kufurahisha wanasiasa ndo mnaona la maana na upinzani pambaaaafu.. Sana mnajua kufuatilia upinzani tu.
 
Polisi wa nchi hii hawana akili hatakidogo huwezi kupokeq amri ya kipumbavu nawe ukqitekeleza huku ukijuwa madhara take Kwa taifa

Sasa huyo Gwajima ngoja atakavyowashinda mahakamani na yeye afungue kesi yake ya madai, bado sijajuwa hizo pesa mtakazomlipa mtazitoa wapi?

Nasubiri niione mpaka mwisho hii sinema ya bure .

Jamani nani amuongeze Mkuu wa kaya akili kidogo aongezee, iliaache kupambana na Mungu
maana katika historia hakuna aliyepambana na kanisa la Mungu akashinda
 
policcm mna mambo mengi makubwa mmefyata mikia ila hili la kipuuz ndo mpo juu ila nimekumbuka wa mgombea urais wa pengo ndo anaewatuma nini?
 
Wale walio beba fedha za escrow kwa kutumia magunia, na wale wa epa, mbona sheria haitumiki kuwashitaki?
mnaonea wanasiasa na watumishi wa Mungu, naamini kanuni iliyo tumika Nigeria Octoba mwaka huu mjiandae

Tuoneshe hao ni akina nani. Au unakiherehere tu?

Hujaona waliokula fedha ya Ruge? mpaka maaskofu ndani? au hilo hulijuwi?

EPA watu wanatumikia kifungo, hulijuwi hilo?
 
Mimi si mfuasi wa huyu jamaa,lakini kwa hili ni matumizi mabovu ya Rasmali tulizo nazo.

...........Kova kama anapita pita humu naomba hyo kesi muitoe,ila mjiandae mtakaposhindwa kufunguliwa kesi ya madai,madai hayo yatalipwa na kwa kodi za wananchi.

Kama ZOmbe alishinda kesi dhidi ya tuhuma za mauaji.SiDhani kama kesi hiii POlisi watashinda,wanasheria wanajua hamna kesi hapo.
wewe ni mfuasi wake, kwanini usiache ifike mwisho ili kama anaonewa awashitaki, kama haonewi apate haki yake, yeyote anaesema kesi ifutwe hapendi utawala wa sheria na haki, sisi wote kwenye shiria ni sawa
 
Tunesha hao ni akina nani. Au unakiherehere tu?

Hujaona waliokula fedha ya Ruge? mpaka maaskofu ndani? au hilo hulijuwi?

EPA watu wanatumikia kifungo, hulijuwi hilo?
chadema_chenge.jpg
mafisadi wote walioiba pesa za umma wajiandae kwa hukumu hii.
 
Lema aliposema hii nchi inaendeshwa kama gheto watu hawakumuelewa bado tutashuhudia mengi aliyepigwa risasi hadharani yupo lakini mlinzi wa Gwajima yupo kortini kuhojiwa kwa kukuta na silaha huu ujinga unanyika tanzania tuu.
 
Back
Top Bottom