Mlima Kilimanjaro waenguliwa ‘Maajabu ya Dunia’

BabuK

JF-Expert Member
Jul 30, 2008
1,845
329
MLIMA Kilimanjaro uliopo nchini na ambao ni mrefu kupita yote barani Afrika, umetupwa nje ya orodha ya Maajabu Saba mapya ya dunia yaliyotangazwa juzi usiku.

Mt. Kilimanjaro.jpg

Taarfia hiyo ilitolewa jana na Eamonn Fitzgerald ambaye ni msemaji wa ‘New Seven Wonders’ taasisi iliyokuwa ikiratibu upigaji kura kwa vivutio vipatavyo 28 dunia nzima, vilivyoingia fainali za ‘Maajabu Saba Mapya ya Asili.’

Fitzgerald alibainisha upigaji hafifu wa kura kutoka Tanzania ulishindwa kuupa nguvu mlima Kilimanjaro ambao hata hivyo ulikuwa ukikusanya mamilioni ya kura kutoka nchi zingine za Ulaya na Amerika kwa zaidi ya asilimia 95.

Bodi ya Utalii nchini (TTB) iliyokuwa ikiratibu kampeni za ndani za kuupigia kura mlima
Kilimanjaro, ilianza upigaji kura mwaka huu, ikiwa tayari imechelewa sana kwa mbio za kutafuta ‘Maajabu Saba’ mapya ya dunia, zilianza mwaka 2009.

Fitzgerald ameutaja ‘Mlima Meza’ (Table Mountain) ulioko katika Jiji la Cape Town, Afrika Kusini kuwa miongoni mwa maajabu saba mapya ya dunia.

Mlima Meza na Kilimanjaro ndivyo vilivyokuwa vivutio pekee kutoka barani Afrika vilivyofanikiwa kuingia kwenye fainali ya mbio hizo za kimataifa.

Hivi sasa maajabu mapya saba ya asili ya Dunia ni pamoja na msitu mnene wa mvua wa Amazon ulioko Amerika ya Kusini, Maporomoko ya Iguazu yaliyoko Argentina, Kisiwa cha Jeju kilichopo Korea Kusini, Mto wa Chini ya ardhi ujulikanao kama ‘Puerto Princesa’ ambao uko Ufilipino na Mlima Meza (Table Mountain) wa Afrika Kusini.

Source: HabariLeo
 
tehetehe mijitu ya TTB ililala usingizi ikaja zinduka too late km kawaida yetu shame on you TTB!
 
Sasa baada ya kura ndio watalii wengi wataenda SA kuuona. Mashindano mengine ni ya kichizichizi sana. Kilimanjaro itaendelea kuwa number one katika kuliingizia taifa kipato cha forex tena sasa wanahitaji kuongeza gharama za wale wanaotaka kuja kuupanda mara dufu kama hawataki waende Cape Town. Na wale wanaoingia kupita Kenya walipe mara tano zaidi.
 
The Provisional New 7 Wonders of Nature

amazon.jpg

halong_bay.jpg

iguazu_falls.jpg

jeju_island.jpg

komodo.jpg

pp_underground_river.jpg

table_mountain.jpg

AMAZON
HALONG BAY
IGUAZU FALLS
JEJU ISLAND
KOMODO
PUERTO PRINCESA UNDERGROUND RIVER
TABLE MOUNTAIN

The above are the provisional New7Wonders of Nature based on the first count of vote results on 11/11/11.It is possible that there will be changes between the above provisional winners and the eventual finally confirmed winners.The above provisional New7Wonders of Nature are listed in alphabetical order, not in any position or ranking.The voting calculation is now being checked, validated and independently verified, and the confirmed winners will be announced starting early 2012 during the Official Inauguration ceremonies.




The announcement of the provisional New7Wonders of Nature - YouTube
i should call this crap contest is new7wonders of SMS AND MAIL then NATURE
UNESCO doesn't recognize them so i will never trust this damn voting




Inatia kichefuchefu..Ni pale waziri Mkuu Mhe. Peter Kayanza Pinda Mizengo aliposikika katika milio ya simu siku moja kabla ya zoezi la kupiga kura kukamilika akiwataka watanzania wenzake muupigie kura mlima Kilimanjaro bila hata kuelezea kama hakuna gharama zozote za kufanya hivyo. Ya nini kupoteza muda na vocha zako?? (wengi ndivyo walivyodhani kutokana na viongozi wetu na Bodi ya Utalii kutokuwa makini katika zoezi zima).. Watanzania ndivyo tulivyo..tutaendelea kuwa hivi hivi...



 
ttb lazima tuwalaumu....... Maana wameanza kuupigia mlima kampeni in eleven hours........ Tabia ya kuzima moto sijui tutakuja kuiacha lini?!! Eti bado siku mbili ndiyo mama riz anaanza kutangaza kuupigia kura........ Naye pinda mtoto wa mkulima vivyo hivyo..... Zima moto style......
 
nilivyoona TTB imechelewa kufanya kampeni nikadhani wananjia ya kuchakachua!.
 
Kilimanjaro ili iweje?si bora hata ule mjusi wetu ulioko jerumani ungeweza kushinda.
 
Kweli viongozi wetu wazembe! Kwa nini hawakuwaeleza wananchi kuwa upigaji kura ulikuwa ni bure? Wanajua kipato chetu then unaambiwa tuma mesage kuupigia mlima kilimanjaro je vocha nimepewa? Mi mwishoni mwishoni kusema ngoja nitume na baadae nikagundua kuwa haikuwa na gharama yoyote. Hata hivyo Afrika kusini nadhani wamiliki wa simu ni wengi kuzidi Tanzania.
 
Watu walishajipanga kutafuna hela za kupokea ushindi.

Afu hiyo nayo ingejumuishwa kwenye ulaghai wa mafanikia ya miaka 50 ya uhuru.

Safi sana kwa kushindwa.
 
Back
Top Bottom