Mlete hapa mwenye moyo mgumu ajabu

Mlete hapa mwenye moyo mgumu ajabu

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,440
Reaction score
38,437
Habari

Haya ni baadhi ya matukio yalionipa mshangao, niliowahi kuskia ama kushuhudia, naomba tusaidiane kumleta mtu ama tukio linaloashiria mhusika kuwa na moyo mgumu ajabu.

  1. Kwangu lile alilolifanya Makonda ubungo, juzi juzi kwa jsw, ni la kipekee kabisa! Mpaka sasa naamini siamini! Kama inabaki vile vile, basi jamaa ana moyo mgumu ajabu.
  2. Nimewahi kumuona jamaa aliemuua babake kwa shoka, tena msikitini, katika swala ya alfajir! Huyu jamaa nilimuona wajabu ama ana moyo mgumu ajabu tangu siku hiyo.
  3. Wakati nipo chuo, niliwai sikia simulizi kuwa, kule Mzumbe Morogoro, yupo lecturer alimkamata mdogo wake (wengine walisema mke! ni simulizi) SUP, kisha muhusika akashindwa kusapua, akamla kichwa, na eti walikuwa wakiishi pamoja! kama ni simulizi ya kweli, basi huyu lecturer ana moyo mgumu ajabu.
  4. Naifahamu ndoa ambayo ilifeli dak ya mwisho, bibi harusi alikataa ndoa siku ya ndoa, huku kukiwa na kadamnasi ya watu! Bila kujua kilichomsibu bibi harusi, kwa uamuzi ule, mahali pale, tena kwa wakati ule, ana moyo mgumu ajabu.
  5. Nilisimuliwa kuwa, kuna nyumba ilikuwa inawaka moto, inateketea, baba wa familia, alifanikiwa kuwaokoa watu wake, kwa kuanzia na mkewe, mtoto wa kwanza, mtoto wa pili, dada wa kazi, mtoto wa tatu, baadae akaanza kuokoa assets mbali mbali, mwisho kabisa akamkumbuka paka wake, aliemsahau ndani! wasimulizi wanasema alipomfuata paka wake, yule jamaa hakurudi tena, moto ulimteketeza, kwangu mimi, jamaa alikuwa na moyo mgumu ajabu.

Kwa uhuru, hebu tuletee mtu ama tukio uliloshuhudia ama kusimuliwa linaloashiria mhusika kuwa na moyo mgumu ajabu.
 
Jamaa alimuua baba yake na kumnyonya damu yake kisa tu baba yake alikuwa anamkanya aache tabia ya wizi.....
............... ............ .........

Nilimshuhudia mdogo wangu akimuu mbu aliyemng'ata hadi mbu kafa kabisa
 
Mimi hili la walimu kuuliza haya maswali nimeshangaa kweli. Hebu soma

Hatuoni polisi wakiamriwa watumie mishahara yao kujenga vituo vya polisi, hatuoni mahakimu wakijenga mahakama, hatuoni waganga wakijenga hospital, hatuoni wanajeshi wakinunua silaha, hatuoni mishahara ya wahandisi ikijenga barabara, LAKINI MWALIMU mwenye mshahara kiduchu anaamriwa achangie tena bila idhini ujenzi wa maabara ili kutimiza ahadi ya sera za CCM, kodi unayolipa yafanya nini? Aiseee wana moyo mgumu kweli
 
Jamaa alileta taarifa ya kifo chake mweneyewe na watu tukasikitika kwa kumpoteza member mwenzetu, baada ya wiki mbili jamaa "alifufuka" aisee jamaa ana moyo mgumu kweli
 
hakika huu ni moyo mgumu uliotukuka mkuu
 
Jamaa alileta taarifa ya kifo chake mweneyewe na watu tukasikitika kwa kumpoteza member mwenzetu, baada ya wiki mbili jamaa "alifufuka" aisee jamaa ana moyo mgumu kweli

hahahah huyo moyo wake ni mgumu kuliko
 
Mimi hili la walimu kuuliza haya maswali nimeshangaa kweli. Hebu soma

Hatuoni polisi wakiamriwa watumie mishahara yao kujenga vituo vya polisi, hatuoni mahakimu wakijenga mahakama, hatuoni waganga wakijenga hospital, hatuoni wanajeshi wakinunua silaha, hatuoni mishahara ya wahandisi ikijenga barabara, LAKINI MWALIMU mwenye mshahara kiduchu anaamriwa achangie tena bila idhini ujenzi wa maabara ili kutimiza ahadi ya sera za CCM, kodi unayolipa yafanya nini? Aiseee wana moyo mgumu kweli

Naunga mkono hoja ya walimu.
 
Kwa kweli walimu wana mioyo migumu
 
Back
Top Bottom