jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 35,950
- 29,532
Mimi sio mpinzani wa wapinzani halali na waadilifu!
Naleta mada hii kwa mjadala wa kiistaarabu na kizalendo kabisa.
Kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu 2015 tumeshuhudia twists and turns za aina yake kwa wanasiasa na wanazuoni mbalimbali lakini pia kwa mara ya kwanza tumeshuhudia Upinzani wa Tanzania chini ya mwamvuli uliotoboka wa UKAWA ukijaribu kwa mbinu zote zile ziwe halali au haramu ili kuinusa Ikulu ya Magogoni bila mafanikio.
Kubwa ni lile la kubadili gia angani na kujaribu kuaminisha umma wa watanzania kuwa kile kilichoitwa najisi kwa miaka mingi ati sio najisi tena !
Ni wazi kuwa mwenendo huu wa upinzani Tanzania uliwashangaza wengi wa wananchi na pengine wakaamua kuuadhibu kwa kuukosesha ushindi kulinganisha na matarajio!
Swali la msingi ni kwamba baada ya upinzani kuamua ku-take risk ya aina yake na kuangukia pua je tumebakia na upinzani wa namna gani?
Kwangu mimi naona baada ya kujinajisi na kujiharamisha sioni tena nafasi ya upinzani katika kuishauri serikali ambayo imeingia madarakani kwa kujinasibu kupambana na ufisadi na ukosefu wa uadilifu.
Hakuna namna serikali adilifu inaweza kushauriwa au kusikiliza ushauri kutoka kundi la wasio waadilifu au waliotetea ufisadi.
Kwa sasa upinzani wa Tanzania uko katika mkwamo mkubwa!
This is Sad but truth!!
Karibuni kwa hoja na sio vihoja.