RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Mkuu wa wilaya ya Mkalama mkoani Singida, Christopher Ngubiangai, amemsimamisha kazi Afisa Afya wa Wilaya hiyo, bwana James Ndembo, kwa muda usiojulikana kufuatia wizi wa zaidi ya shilingi milioni 19.
Ngubiangai amemtuhumu Ndembo kwa wizi wa fedha hizo zilizotengwa ili kutoa elimu kwa wananchi juu ya magonjwa yasioambukizwa. Amedai kuwa Ndembo alitoa fedha kiasi cha shilingi 25,151,430 benki na kuzihifadhi kwa mweka hazina wa Manispaa ambapo amekuwa akichukua kiasi cha pesa katika nyakati tofauti kwa ajili ya matumizi binafsi.
Ndembo alijaribu kukimbia lakini amekamatwa na sasa yuko chini ya ulinzi.
Ngubiangai ameonya watumishi wa umma dhidi ya wizi wa fedha za umma, tabia ambayo inakwamisha maendeleo. Amesema watakaobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.