Utafiti: Waganga wa jadi (washirikina) wanaongoza kuishi maisha marefu kwa maeneo ya vijijini

digba sowey

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
7,896
14,358
Amani iwe nanyi wapendwa,

Katika dunia hii huwezi kuukataa ukweli kuwa kuna nguvu za nuru na nguvu za giza.
Nguvu hizi hutenda kazi sawa kulingana na imani ya mhusika. Katika dunia hii binadamu hofu yake ipo juu ya kifo tu ndio maana kuna mahospitali na wanganga wa tiba asilia huku lengo likiwa kupambana na madhara ya magonjwa ambayo hupelekea vifo.

Katika utafiti wangu nilijikita katika kuangalia ni watu gani wanaongoza kwa kuishi maisha marefu kwa maeneo ya vijijini, ukweli ni kuwa waganga wa jadi katika maeneo niliyo fanyia tathimini wameonekana kuwa na umri mkubwa, wengi wao niliokutana nao umri wao ulikuwa kuanzia miaka 70 na kuendeleo, zaidi nilkuja kustaajabishwa nilipofika kwenye familia ambayo mkuu wa familia ni bibi wa miaka 106 huku akiishi na mdogo wake wa miaka 89.

Mkuu wa familia ambayo ni bibi ni mganga wa jadi mashuhuri na anaogopeka sana kijijini hapo, maeneo ya utafiti wangu yalikuwa ni Mikoa ya Lindi (Liwale) ambapo nilifika hadi maeneo ya ngende kwa Bibi Njimwite mama wa umri unaokadiriwa kufikia miaka 90.

Pia nilifika mikoa ya Mwanza wilaya za Sengerema na Magu, Shinyanga nilifika wilaya ya kahama pekee huku Simiyu nilifika maeneo ya Busega hasa Nassa na pia wilaya ya Bariadi.

Maeneo yote hayo nilikuwa natembelea nyumba za raia wa kawaida na waganga wa jadi, kwa upande wa wananchi wa kawaida nilikuta familia nyingi eidha kuna baba pekee au mama huku sababu za hayo zilitajwa kuwa ni vifo na wengi wao walionekana kufariki kabla ya kufikia miaka 70.

Katika ziara zangu zote hizi nilikuwa nazifanya kwa lengo la kutaka kufahamu ikiwa nguvu za giza zipo na kama zipo je zinauwepo wa kufanya yale tunayo yasikia? ,swali langu lilikuja kujibiwa pale nilipofika katika kijiji cha Mwangh'wenge - Busega (Simiyu) kwa mzee mashuhuri anaye julikana kwa jina la Kidali babu wa miaka 80, babu huyu yeye alinipaka dawa Fulani machoni ambayo ilinifanya kuona yasiyoonekana.

Hivyo kwa utafiti wangu mdogo umenifanya niamini kuwa vifo vingi ambavyo binadamu hufa si vile Mungu alivyotupangia Bali vingi ni akili za binadamu, lakini pia Mungu hawezi kuwa muongo maana alisema miaka yetu katika dunia hii ni 70 au pengine 80 ,sasa iweje Mungu achukue roho ya mja wake katika umri wa chini ya miaka 70, lakini pia nilikuwa nafuatili umri wa kuishi kwa kila nchi, nilistaajabu nilipoona nchi ya Japan ambapo life span yao inafikia hadi miaka 90.

Ijulikane kuwa kwa maeneo yote hayo nilifika nikijifanya kama mteja au mtu anayetafuta huduma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati fulani wakati nafanya kazi za utafiti vijijini, nilimuona Mzee ambaye baadae nilikadiria ana miaka 100 na zaidi kulingana na mazungumzo yake na historian alizonipa kuhusu Wajerumani, Waingereza na baada ya Uhuru na jinsia walivyoishi maisha ya uwindaji na vyakula vyao.

Baadae nikaja gundua yule Mzee ni 'mtaalamu wa kuleta na kuzuia mvua' na wanakijiji walimuheshimu kwa hilo.
 
Nini kinawafanya waishi maisha marefu kuliko sisi RAIA wa kawaida
Wakati fulani wakati nafanya kazi za utafiti vijijini, nilimuona Mzee ambaye baadae nilikadiria ana miaka 100 na zaidi kulingana na mazungumzo yake na historian alizonipa kuhusu Wajerumani, Waingereza na baada ya Uhuru na jinsia walivyoishi maisha ya uwindaji na vyakula vyao.

Baadae nikaja gundua yule Mzee ni 'mtaalamu wa kuleta na kuzuia mvua' na wanakijiji walimuheshimu kwa hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom