figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,720
- 55,852
Mkuu wa wilaya ya Bunda Bi.Lidya Bupilipili,mkuu wa kikosi cha JKT 822 KJ Rwamkoma Meja David Msakulo na viongozi wa usalama wa JKT na JWTZ wamenusurika kifo baada ya boti walilokuwa wamepanda kuzama wakati wakikagua maeneo ya kufugia samaki eneo la Bulamba ktk Ziwa victoria wilayani Bunda.
Viongozi hao ambao walikuwa na ujumbe kutoka UNDP wameokolewa na vijana wa JKT na JWTZ wanaosimamia mradi huo mkubwa wa JKT wakiwa umbali wa zaidi ya mita mia mbili toka nchi kavu.
Taarifa toka eneo la tukio zinasema viongozi na maafisa hao wote wako salama na sasa wanarejeshwa nchi kavu.
Chanzo: ITV