Mkuu wa Wilaya ya Arumeru aamuru kukamatwa kwa waandishi

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru aamuru kukamatwa kwa waandishi

[HASHTAG]#KamataKamataYaViwanda[/HASHTAG]
 
Huyu bwana mdogo ni aina fulani ya vi.la.za waliofika hapo walipo kwa kujipendekeza CCM
Ni mdogo sana hajawahi hata kuwa kenge(monitor) wa darasa.

Hicho cheo kimemzidia sana sana sana!!Anapagawa na saluti na kunyenyekewa,hajui kuwa vyeo hivi ni vya kupita na kuna maisha baada ya hapa Arumeru.Walikuwepo kina Hawa Ngurume,toka Kinondoni mpaka Mbarali,wababe na wanazaba watu makofi,lkn leo wapo chini ya futi sita.

Nakumbuka huyu dogo alikuwa anasoma na vijana wangu pale Tegeta Secondary,tena ni ungaunga tu wa elimu na HKL yake,na alisoma kinafiki pale Tegeta shule ya Wazazi wa CCM....Namuonea huruma sana kwa laana anazochuma wakati angali kijana.

Bwana mdogo tenda wema,hujui kesho yako!!Madaraka ni ya kupita
Awamu hii viongozi ni washamba flani na walevi wa madaraka hawajui tu duniani twapita yatupasa kutenda haki kwa wote na sio kuonea wengine. Huyo DC ni limbukeni na hapo anajiona kafika na hajui kuwa sio wote waanzao mbio humaliza, sasa angepata cheo kikubwa kuliko hicho ingekuwaje, tena hivi vyeo vingefutwa tu pamoja na vya u RC.
 
Hata wewe umeolewa,jisitiri.Tuliooa tunajua huwezi kumtofautisha DC wa Arumeru,RC wa Arusha na wa Dar.Fikiria nje ya sanduku lilofunika ubongo kama upo.
Kinena ni Goomble mwenyewe
 
Leo wandishi wa habri wawili amekamatwa na jeshi la polisi na kupelekwa kituo cha polisi cha usariver waandishi hao ni wa radio sunrise na mwandishi wa gazeti la habari leo sababu kuwa mkuu wa wilaya ya arumeru amekataza kuandika habari bila kibali kwake .
 
Nakumbuka maneno ya mtumishi wa Mungu; Mwalimu Mwakasege kuhusu watu wanaoonea wenzao!
 
mie naona dalili za kuchafuka aisee kwa nchi yoote, siku hawa jamaa wakiamka sijuivtutakimbilia wapi aisee kwa wanayofanya, wasione ni mambumbumbu, fyokofyoko wanaianza wenyewe, Yarab tunusuru waja wako, siku wakiamka eeeh
 
Back
Top Bottom