Mkuu wa Wilaya Tarime vijijini na viongozi wa kata mbalimbali wanafaa kuwajibishwa kwa uzembe wa kutotoa taarifa ya uwepo wa nzige wilayani humo

incredible terminator

JF-Expert Member
Aug 1, 2016
2,229
3,525
Habari za mdaa huu wakuu, Natumaini kuwa Jf ni sehemu ambayo pia ni huru ambapo taarifa mbalimbali zinakuwa gathered na kushughulikiwa,

Wiki iliyopita nilipata bahati ya kusafiri kikazi kwenda Mkoani Mara, Kusema kweli nilichojifunza niligundua watu wa mkoa wa Mara ni watu wakarimu sana,

Pia ni mkoa wa kuvutia sana Natural vegetation yake na land fertile vilinichanganya zaidi kusema kweli kwa mda mchache niliokaa mkoani Mara nimepata kufurahia sana na nimepata kujifunza kwa mkoa huu wenye sifa na umaarufu huku nchini ikiwemo sifa ya uwepo wa watu wakatili ila binafsi hili sikuliona nilichokiona ni ukarimu wao tu,

To the point, Nilibahatika kupita katika vijiji kadhaa vinavyoaminika vipo katika wilaya ya Tarime Vijijini, Ambavyo ni, SIRARI, KUBITERERE NYAMHONDA, IBOKOHO, KIONGERA, MATAMANKWE, KIKOMORI NYABIRONGO, NCHOKI, KOROTAMBE,

Pia nilibahatika kuvuka Wilaya hii kwa uchache kidogo nikafika wilaya ya ROLYA napo nikaingia baadhi ya vijiji, kama SHILATI, IKOMA, KINESI na vingine nimevisahau,,,,, ila hivi vijiji nilivyoorodhesha hapa ndio vijiji vilivyo mpakani Mwa Kenya na Tanzania,
Pia hapa niligundua kuna kauzembe flani ivi pale Migration boda ya sirari maana kuna mwingiliano wa kiholela sana pale mpakani hili nililiona nilivyofanyiwa surprise ya kwenda Kenya bila kujua yaani nilivushwa mpakani kiholela pasipo kuambiwa na kilichonistua ni baada ya kuona Bendera ya Kenya ikipepea upande niliopo hakika sikujua kama nimevuka mpakani kiholela kiasi kile..upande wa pili wa Mji wa sirari waliniambia panaitwa ISBANIAH kama sikosei nadhani wenyeji watarekebisha ila huu ni upande wa pili wa mji wa sirari ambao upo KENYA

Ila cha kushangaza ndani ya mda niliokaa wilayani hapo nimeshuhudia wanainchi wakihangaika kupulizia dawa mashambani mwao wenyewe wakidai ibuko la wadudu aina ya nzige ambao kwa sasa ni tishio kwa mazao yao, lakini cha kushangaza hadi sasa serikali IPO kimya kana kwamba hawana taarifa juu ya ibuko la wadudu hao ambao waonapukutisha kasi za mazao ya wakulima wilayani humo,

Ningeiomba serikali yangu ya Mheshimiwa SSH kuwagiza kikosi cha uchunguzi dhidhi ya vijiji hivyo ili kuwasaidia wanainchi kwa kadhia hii ambayo mda sio mrefu tutashuhudia njaa Kali mkoani humo.

NAWASILISHA.
 
Mkuu nzige uliwaona live kabisa,maana siki hizi hata mahindi huwa yanapuliziwa dawa shambani halafu unasema ulivushwa mpaka kinyemera ulikuwa umewekwa kwenye box au
 
Mkuu nzige uliwaona live kabisa,maana siki hizi hata mahindi huwa yanapuliziwa dawa shambani halafu unasema ulivushwa mpaka kinyemera ulikuwa umewekwa kwenye box au
mkuu waende wachunguze ndio maana nimeleta taarifa pia kuvushwa inamaana mwenyej wangu hakuniambia kama ninavuka mpaka ila tulikuwa katika movement tu kujikuta naoneshwa bendera na nikagundua nimevushwa mpaka kwa surprise
 
mkuu waende wachunguze ndio maana nimeleta taarifa pia kuvushwa inamaana mwenyej wangu hakuniambia kama ninavuka mpaka ila tulikuwa katika movement tu kujikuta naoneshwa bendera na nikagundua nimevushwa mpaka kwa surprise
Basi sema ulivuka bila kujua, sio umevushwa.
 
Back
Top Bottom