Mkuu wa Wilaya Newala amuwajibisha aliyesababisha kifo cha mjamzito kwa uzembe

MASIGA

Senior Member
Aug 29, 2015
130
281
Mkuu wa wilaya ya Newala Mhe Aziza Mangosongo amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Mji Newala,kumsimamisha kazi Mganga Mfawidhi wa wodi ya wazazi katika Hospitali ya wilaya ya Newala Abdalah kipeta ili kupisha uchunguzi kufuatia tukio la kufariki mama mjamzito hivi karibuni kutokana na uzembe wa kutompatia huduma za matibabu kwa wakati.


Mhe Mangosongo ametoa agizo hilo Jana wakati akizungumza na watumishi wa Afya na wajumbe wa bodi ya Afya kwa lengo la kuwahimiza kufanya kazi kwa weledi na kuwahudumia wagonjwa bila ubaguzi na kwa moyo wa upendo.

Amesema kitendo cha waaguzi kutowajali wagojwa na kuwatolea kauli mbovu na ukosefu wa dawa kumesababisha wagonjwa wengi kutojitokeza kwenda kupata huduma za afya na hivyo kufanya mapato ya hospitali hiyo kushuka tofauti na ilivyokuwa huko nyuma.

Aidha ametoa agizo kwa Mganga Mkuu chitopela chitopela kuhakikisha mapungufu yaliyojitokeza katika hospitali hiyo yanafanyiwa kazi hususani kutumia fedha nyingi katika kununua dawa na vifaa tiba.

#SerikaliIpoKazini #NewalaTupoKazini #TunatekelezaIlani #TunawatumikiaWananchi #TupunguzeVifoVyaMamaNaMtoto
#JPMTena2020

IMG-20181003-WA0048.jpeg
 
Back
Top Bottom