Mkuu wa Wilaya Karagwe amchapa vibao raia

Mkuu wa Wilaya Karagwe amchapa vibao raia

Hii imetokea huko kwenye wilaya wakati raia huyo anahojiwa na DC mbele ya polisi DC akamchapa kibao raia mwema

Je, kwanini polisi wasimkamate DC palepale kwakuwa ameshambulia?

Sent using Jamii Forums mobile app

Hivi ni kwanini Sisi Watanzania huwa tunapenda tu ' Kuhukumu ' upande mmoja tu wa jambo kila mara linapotokea?
 
Hivi ni kwanini Sisi Watanzania huwa tunapenda tu ' Kuhukumu ' upande mmoja tu wa jambo kila mara linapotokea?
Hata kama walivamia msafara wake, yeye kama kiongozi hakupaswa fanya hivyo kwa maana tayari alikuwa mikononi mwa polisi angeacha sheria ichukue mkondo wake.

Kila siku wanawambia raia wasichukue sheria mkononi kwa kitendo chake basi raia uwa wanakuwa sawa wakimpiga na kumuua jambazi au muaharifu
 
Rais wa Inchi akimpika mke wake ni HABARI,
Raia wa kawaida akimpiga mke wake si habari na anakuwa kwenye kutimiza majukumu yake.

Kibaka wakipigana watu hushangilia na kuona jambo la kawaida.
 
Hivi ni kwanini Sisi Watanzania huwa tunapenda tu ' Kuhukumu ' upande mmoja tu wa jambo kila mara linapotokea?
kuna hukumu zingine zipo wazi, haihitaji kuundiwa tume wala unyafuzi wa ivyo, kosa ni kosa tuu na hata yangekuwa mawili haihalalishi la kwanza.
 
Umekurupukia wapi wewe Hiki ulichoweka akieleweki
Kabisa kabisa, hasa katika suala la Ma DC kujichukulia sheria mkononi, tungependa tujuwe ni DC gani, wilaya gani, sehemu gani, raia gani? Nasi tuisambaze na kuwatuhumu kwa udhulumu wa haki..
 
Huyu DC ajawahi kuwa luteni au kanali wa jeshi letu pendwa? maana mtukufu huwapenda zaidi hao kuwapa pande!
 
Hii imetokea huko kwenye wilaya wakati raia huyo anahojiwa na DC mbele ya polisi DC akamchapa kibao raia mwema

Je, kwanini polisi wasimkamate DC palepale kwakuwa ameshambulia?

Sent using Jamii Forums mobile app

Umekurupukia wapi wewe
Hiki ulichoweka hakieleweki
Ni kweli mleta maada umekurupuka.
Kamilisha habari ueleweke.
Wilaya gani? DC anaitwa nani? Ilikuaje akamchapa raia?
Au weka hata katu-video tukuelewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ni kwanini Sisi Watanzania huwa tunapenda tu ' Kuhukumu ' upande mmoja tu wa jambo kila mara linapotokea?
Hebu rudisha busara yako maana siku hizi siyo Gentamycine Wa kawaida sijui umekuwa tetracycline? Hivi Dc kumpiga raia vibao unataka tubalance nini labda. Kuna uhalali wowote katika mazingira yoyote Dc kufanya hayo madudu? Siku hizi sikuelewi mkuu.

ACHA nikae KIMYA...!
 
Huyo jamaa kampeleka mtoto wake mgonjwa kwenye kituo cha afya Kayanga. Alipofika hakumkuta mganga yoyote. Akaamua kwenda nyumbani kwa mganga maana nyumba ya mganga ipo hapo hapo.

Akamkuta mganga amekaa akamweleza shida yake, mganga akaenda akamuona mgonjwa bila ya kumhudumia akaamua kurudi kwake. Jamaa akasubiri zaidi ya saa nzima mganga haonekeni. Akarudi tena kwa mganga akamkuta mganga amekaa anaangalia TV. Jamaa kwa hasira akamtembezea mganga kichapo kisha akamhamishia mgonjwa wake kwa Dr. Maiko.

Mganga kaenda kushitaki kwa mkuu wa wilaya. Mkuu wa wilaya kaandamana na polisi wakamkamata hiyo jamaa ndio sokomoko linaloendelea hapo

C&P
 
Huyu huyu DC ameonekana pia akimchapa viboko mfugaji huko Kashanga, Karagwe.
 
Back
Top Bottom