Mkuu wa nchi na ukimya kuhusu mawaziri

Mkuu wa nchi na ukimya kuhusu mawaziri

Ingekuwa hafanyi hivyo basi tusingekuwa na mizigo mawaziri chungu nzima ndani ya Baraza la Mizigo ya Mawaziri.

Kwa hiyo wewe unadhani uteuzi wa mawaziri unafanyika kama kuteua mabaunsa wa disco?
 
Uteuzi wa viongozi unahitaji umakini na pia kushirikisha vyombo na watu wengine. Kazi hiyo itafanyika baada ya sikukuu za mwisho wa mwaka.

...cha kushangaza na umakini wote huo wanakuja na magalasa mtupu...
 
muda c mrefu mtasikia mkuu anasafari ya kwenda usa kumpa heri ya mwaka mpya obama
 
Teh teh...akiwatangaza sasa hivi watadai mshahara wa dec. Anangoja mwanzo wa mwezi.

Umakini ni muhimu jamani, ukizingatia muda uliobaki na mchache sana. Mkuu akifanya pupa litavunjwa tena baada ya miezi michache,

Au mnataka mkuu awe na rekodi ya kusafiri mara nyingi...na kuvunja baraza la mawaziri mara nyingi!!
 
Kwenye uchaguzi/uteuzi wa mawaziri....sitaki kuamini kuwa tatizo ni RO/Mkuchika......tatizo ni Mfumo mzima unaotumika kuchagua/kuteua na ambao unaotetewa/piganiwa na CCM........Watani zetu wa jadi (Kenya) hilo suala wameshaliweka sawa......juzi juzi tu Rais Kateua tume......Mahakama wakaipiga chini.......hakuna free ride kwa Rais......
 
Sasa ni takribani wiki moja na siku toka mawaziri watatu kusimamishwa na mmoja kujiuzulu kutokana na ripoti ya tokomeza majangili. Katika mawaziri hao kuna ambao wananchi walishawatilia shaka katika utendaji wao wa kuwahudumia wananchi. Kuna mawaziri wengine ambao kwa namna moja au nyingine shutma na hata viongozi waandamizi katika chama chao wamewatolea uvivu na kuwaambia kuwa ni mizigo na hiyo ni kabla ya rais kutengua uwaziri wa hao mawaziri wanne.

Swali langu ni kwamba, je! Rais hadi mda huu hana mawaziri wengine ambao tayari alishawafikiria? Au bado yuko mapumzikoni kama mwenzake Pinda aliyesema hawezi kuongea kwa mda huu. Au hajaona mbunge yeyote anayekidhi vigezo vya uwaziri?

Naomba kujuzwa kwa nini hakuna taarifa yoyote kuhusu swala la mawaziri.

haraka haraka haina baraka,akifanya papara akaleta mawaziri wabovu nyie nyie mtarud tena hapa kulalamika
 
Subiri, rais bado ana mshtuko aloupata baada ya kupewa majibu ya vipimo vya afya yake huko US.
 
mawaziri wote hawatakaa wasahau sikukuu ya mwaka huu,yaani presha kwao inashuka na inapanda,hawajui nani atabaki nani ataachwa nasikia na yule wa ......naye anatakiwa kubadilishwa eti ni kweli?
 
haraka haraka haina baraka,akifanya papara akaleta mawaziri wabovu nyie nyie mtarud tena hapa kulalamika

kwa mtazamo wako wewe tukimpa mwezi mzima anaweza kuja na wachapakazi? Je! Ni kwa mda gani wananchi walishaanza kulalamika? Alichukua hatua gani tokea kipindi hicho? Au bado hajamaliza safari zake. Hivi amesharudi nchini kweli?
 
amesharejea na mambo ya muda wa maamuzi kwa serikalini ni siri,hilo tunalijua na tumezoea,kwaio yeye ndo anajua ni lini atateua hao mawaziri
 
Baada ya mawaziri kuachishwa kazi kama nijuavyo mwangalizi wa wizara husika huwa ni naibu waziri. Mda huu ni takribani mwezi mzima tokea rais atengeu utendaji wa baadhi ya mawaziri. Wiki iliyopita waziri wa maliasili na utalii alikuja na maneno yake kuhusu ripoti iliyowaondoa baadhi ya mawaziri. Je! Rais haoni uharaka wa kutuletea mawaziri watakao simamia rasilimali zetu? Mbona ameweza kuapisha mabalozi aliowateua haraka ilhali maliasili zinazidi kuteketea? Jana taarifa imekuja kuna faru kauawa je hilo yeye alimgusi. Au kuna agenda nyuma ya mgongo wake
 
Back
Top Bottom